Kati ya watu wachache waliobakia ndani ya ccm niliokuwa bado nawaheshimu ni pamoja na huyu Agwe Ndugai Job. Bahati nzuri namfahamu huyu bwana kwani tulisoma naye Old Moshi. Alionyesha uwezo wa uongozi tangu enzi zile.
Ndiyo maana alipopata ubunge na sasa U-Naibu spika mimi sikushangaa. Lakini kwa jinsi alivyopeleka mambo jana: tukianzia na hoja ya Mch Mh Msigwa kuomba mwongozo, yaani badala ya kutoa mwongozo akarudia makosa yale yale ya Sitta kuwaita wapinzani eti Wanafiki. Hiki kibri kakitoa wapi Job Mbaruka??
Tukirudi kwenye issue ya Mh Mdee, alitumia ubabe wa hali ya juu, anamtisha Mh mbunge mwenzake anaruhusu wabunge kuropoka ovyo bila utaratibu. Alimtisha kwa kushika kile kitabu, sijui ndicho chenye kanuni, anamwambia asicheze na kiti, sijui anaweza kufanya maamuzi ambayo wapiga kura wake hawatamuelewa, na maneno ya namna hiyo.
Kwa kifupi Job kubali "mate" wangu uliteleza. Ingawa mtu mzima huona aibu kusema samahani (na hasa kwa mwanamke), naomba uwe wa kwanza kumwomba samahani mbunge mwenzako wa Kawe - Halima Mdee.
Vinginevyo sisi wapiga kura wako hatukuelewi. Au ni kaulevi fulani mnako wabunge wa ccm?? Au mnadhani 2015 ni mbali sana?? Au hapatakuwa na maisha tena baaba ya hili bunge?? Au mnadhani mtaendelea kuishi humo mjengoni baada ya mwezi wa 9??
Kama majibu ya maswali yangu hapo juu ni SIYO mnategemea tuangaliane vipi huku uraiani na hasa utakapofika ule msimu wa kuomba kura kurudi Mjengoni?? Kwa sababu naamini kabisa hata wewe Job bado unahitaji kurudi mjengoni 2015, au imetosha??
Na kwa ninavyokuona unakinyemelea kiti cha Makinda, kama sivyo kataa na ukanushe.
Mimi niseme tu kwamba CCM wanajimaliza wenyewe, yatakayotokea 2015 wala wasitafute mchawi, watajifanya kusahau lakini sisi waathirika wa wanayoyasema na kuyatenda sasa hivi tutawakumbusha, kwani waswahili walisema" Mla ndizi husahau lakini mtupa maganda hasahau kamwe".