Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Wakikua wataacha tu utoto raha sana. Mfuate mwenye above 30yrs kama anawaza huo upuuzi.
HII NAYO IDEA ILA WENYE MIAKA ZAIDI YA 30 KUMBUKA NAO WAMESHAKATA TAMAA YA NDOA NA KUONA WASHAZEEKA MDA WAO UMEISHA🙂
 
Ulichoongea ni kweli hata mimi mara ya kwanza nlikuwa napenda sana kuolewaa ili tu nivae shela tu na vikorokoro yaani nkawa silali nawazaa umri umeendaa wenzangu wanavaa tu mashela....ila baada ya kuanza sasa kupitia sehemu mbalimbali na kusoma na kujichunguza mwenyewe nkagunduaa badooo.....
 
SIJUI KAMA WADADA WATACHANGIA HAPA

Watachangia kwa wale ambao hawatamwelewa alieleta mada alikuwa anamaanisha nini . Wao wanataka siku ya harusi ndio kipaumbele chao . Msafara mrefu wa Magari yakiwa yanasindikizwa na matarumbeta , wapitie mlimani city wafanye shopping , wapite beach kupiga picha . Waelekee ukumbini wakiwa wamepanda farasi . Wakae honeymoon hotelini kwa week wakati cha muhimu ni kuangalia majukumu ya maisha ndani ya ndoa
 
Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi. Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku. Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele. Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.

Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye [HASHTAG]#HARUSI[/HASHTAG] yake wamchangie.
Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;

=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?
=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)
=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?
=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?
=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?

*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?

*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?

*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?

*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?

*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.

*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo. Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.
Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo. Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.
[HASHTAG]#THINK[/HASHTAG] DEEP JIONGEZE
I AM DONE!!!
 
Sijasoma hii makala kichwa cha habari kinatosha.
Kama kuna binti ndoto zake siyo harusi kama anavyotuaminisha mtoa mada njoo pm tumzodoe.
 
Umesema kweli mkuu mana demu wangu ye hana stori nyingine zaid ya ndoa kila cku ndoa

Namwambia mama tutaishi vipi ilhali maisha yetu bado hayako poa ila yee ajui ilo........ eti tutalala ata chini il ndoa kwanza

Moyoni na sema uyu demu wahuni washamdukua akili sio kwa kuwaza uko ndoa duuuuuuuuuuuh
 
sisi ni waafrika tamaduni zetu bila ndoa uwe mwanamke au mwanamme hueleweki na jamii
 
Bora mwanamke alishwe avae kikubwa heshima kuna wanawake wana viburi mmh utatamani uue tu simpendi mwanamke mwenye kiburi
 
wanaume harusi hawazitaki wanaona unachezea hela.. wanawake ndio ndoto zao ...

na usawa huu wa magu sitachangia harusi yeyote hata ya ndugu yangu
 
NDOTO ZA MABINTI WENGI NI HARUSI.
Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi.

Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku.

Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele.

Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.

Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye harusi yake wamchangie.

Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;
=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?

=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)

=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?

=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?

*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?

*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?

*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?

*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?

*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.

*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo.

Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.

Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo.

Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.

Think before U take Decision
 
Ndo mafanikio na furaha yao iyo
 
Back
Top Bottom