Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Kuna kitu inaitwa one side love hii inatesa sana ndo maana ndoa za sasa hazidumu
 
Hii mada ni muhimu sana kwa wote wanaotarajia kufunga ndoa na siyo kwa mabinti tu hata wa Kaka wanatakia kujiuliza hayo maswali kabla ya kufunga Ndoa.
 
Nadhani kila mtu akijua nini anataka katika ndoa hili suala linakuwa rahisi sana for both men n women.
 
Wengi wetu tunapenda show off na kwa utafiti katika jamii niliyopo tunapenda sana sherehe ndo maana ndoa za kileo zimejaa malumbano yasiyoisha

Na kwa akili hizo ndo yaleee harusi leo baada ya mwaka wameachana

Wengi waliobariki ndoa naona kama wanayaishi maisha halisi ya ndoa
ni kweli kila msichana huwa na ndoto ya kuolewa?
 
ni kweli kila msichana huwa na ndoto ya kuolewa?
Ndio lkn sio kutaka sherehe ya kifahari hiyo ni aina nyingine ya ndoto

Wakati nakua niliota kuwa na mume na watoto hiyo Ndio ndoa sio kuvaa gauni la harusi na sherehe kubwa Hii mtoa mada ndo anayosema sasa yaani akili za ke anaielekeza kuwaza harusi tu pasipo kutafakari majukumu anayoenda kukutana nayo
 
Mbona huzungumzii upande wa pili maana siku hizi kuna wakaka wanaofanyiwa hadi bag party kama ilivyo send off
 
Ndio lkn sio kutaka sherehe ya kifahari hiyo ni aina nyingine ya ndoto

Wakati nakua niliota kuwa na mume na watoto hiyo Ndio ndoa sio kuvaa gauni la harusi na sherehe kubwa Hii mtoa mada ndo anayosema sasa yaani akili za ke anaielekeza kuwaza harusi tu pasipo kutafakari majukumu anayoenda kukutana nayo
Nimemwelewa sana mtoa mada na watu kama hao wapo.
speaking from experience, nili date mdada moja, sharti la kwanza alilonipa ni kwamba yeye anataka pete ya engagement ya 2m gauni la harusi 1m etc....

narudi kwa mtoa mada, vitu kama hivyo hapo juu siyo shida kumnunulia mkeo, shida inakuja, kuwa ni utayari.
 
NDOTO ZA MABINTI WENGI NI HARUSI.
Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi.

Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku.

Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele.

Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.

Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye [HASHTAG]#HARUSI[/HASHTAG] yake wamchangie.

Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;
=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?

=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)

=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?

=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?

*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?

*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?

*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?

*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?

*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.

*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo.

Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.

Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo.

Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.

Think before U take Decision
Harusi na Arusi ni vitu viwili tofauti.
"H" mara nyingi ni kanusho. Ana magari mawili. Hana gari hata moja
 
Nimemwelewa sana mtoa mada na watu kama hao wapo.
speaking from experience, nili date mdada moja, sharti la kwanza alilonipa ni kwamba yeye anataka pete ya engagement ya 2m gauni la harusi 1m etc....

narudi kwa mtoa mada, vitu kama hivyo hapo juu siyo shida kumnunulia mkeo, shida inakuja, kuwa ni utayari.
Hivyo alitaka kwenda kuonyeshea marafiki zake watoto wa kike akili zetu tunazijua wenyeww
 
Duu imenitouch napenda sana harusi Ila mpenzi Wang hatak ata kuzisikia kila nikigusia swala la harus kama alikuwa anacheka ananuna, anataka aje kutoa mahal tu nyumbn harus atak ananikela kwel ila ndo ivo kumwacha cwez
 
Back
Top Bottom