Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Ndoto za mabinti wengi ni harusi

Leo ni weekend muwaache watoto wa watu warelax, punguzeni magubu, hata mwanaume unapaswa kuyatambuwa majukumu ya mume na kikubwa msisahau ibada.

Ndoa nyingi zinavurugwa na shetani kwa sababu watu tunamsahau Mungu.
Hakuna Mungu.
Ndoa zinahharibiwa na sisi wenyewe
 
Kuna harusi ilifanyika mwaka jana, booonge la sherehe na ilikuwa gumzo as ilikuwa sherehe ya gharama, ndani ya miezi 8 tu ya ndoa, ndoa chaliiiii.
Na hapo tatizo ni mwanaume hata sio mwanamke, ikabidi mwanamke aikimbie ndoa.

Siku hizi sio wanawake wala wanaume wanaotambua maana ya ndoa ni wachache sana.
 
Leo ni weekend muwaache watoto wa watu warelax, punguzeni magubu, hata mwanaume unapaswa kuyatambuwa majukumu ya mume na kikubwa msisahau ibada.

Ndoa nyingi zinavurugwa na shetani kwa sababu watu tunamsahau Mungu.
Ameeeeen!
 
Oa au olewa na yule Mungu aliekusudia. Iwe kwa harusi au bila harusi mengine ni matokeo ya kukosekana mkono wa Mungu
 
Sasa kama mume unae na anakupenda shida iko wapi unahudumiwa. Acha utoto harusi sio ishu sikuhizi dhamira ilikuwa kutambuishana tu baina ya ndugu zenu ila sio kuspend mamilioni ya pesa bure tu.
 
It mean , wanaoishi bila harusi wana long survival kuliko waliopitia tukio la harusi
Some few times yes,maana kwa hulka ya mabinti wa siku hz wanavyopenda kuonekana nao wapo afu akatokea binti akakubali kufunga tu ndoa bila sherehe ya harusi, ameonyesha utayari sana ktk shida na raha...Ni mawazo yangu tu lakin, msije mkanipiga mawe
 
Wengi wetu tunapenda show off na kwa utafiti katika jamii niliyopo tunapenda sana sherehe ndo maana ndoa za kileo zimejaa malumbano yasiyoisha

Na kwa akili hizo ndo yaleee harusi leo baada ya mwaka wameachana

Wengi waliobariki ndoa naona kama wanayaishi maisha halisi ya ndoa
Mwanzo 24. Wazaz walimuuliza Rebeka, je utakwenda na mtu huyu,ndipo Rebeka akajibu, ndio niko tayari. Bas wazaz wakamruhusu kwenda na kijana na kuanza maisha mapya.. Ndoa inaanzia kwa wazazi jamani.... Leo unakuta kijana hana uwezo wa kufanya sherehe ya ndoa lkn bdo binti anakomaa harusi eti iwe kama ya fulani,,,,Tujifunze kukubaliana na hali halisi...na h ni kwa ndoa nyingi sana za kikristo..... Nawasifu sana waislamu,..
 
Leo ni weekend muwaache watoto wa watu warelax, punguzeni magubu, hata mwanaume unapaswa kuyatambuwa majukumu ya mume na kikubwa msisahau ibada.

Ndoa nyingi zinavurugwa na shetani kwa sababu watu tunamsahau Mungu.
Huyu shetani tumekuwa tukimtupia sana mzigo wa lawama adi huruma yani.......mwanadamu tambua wewe sio mnyama...unautashi wako
 
Maswali mengi y nini ukiolewa utayakuta huko huko yanini uwaze shida badala ya Furaha
Baba na mama tumewaona wanagombana

Kaka Dada zetu au majirani

Hayo yapo tu msingi shelaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
NDOTO ZA MABINTI WENGI NI HARUSI.
Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi.

Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku.

Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele.

Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon.

Ndio maana wengi wanakazana kuchangia harusi za wenzao na kushiriki hata kushona sare ili na yeye kwenye harusi yake wamchangie.

Inasikitisha sana kwamba wengi hawafikirii maisha ya Ndoa.
Hawajiulizi maswali ya msingi kama;
=> JE NIKO TAYARI KUWA MKE WA MTU?

=> NIKO TAYARI KUJIDHABIHU KWAAJILI YA FURAHA YA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUSALIMISHA MATAKWA YANGU KUFANYA MATAKWA YA MTU MWINGINE? (Surrendering my will)

=> JE' NIKO TAYARI KUWA MAMA NA KULEA FAMILIA?

=> JE' NIKO TAYARI KUPIGANIA NDOTO ZA MTU MWINGINE?

=> JE' NIKO TAYARI KUAMBATA IKIBIDI KUHAMA MJI NINAOPENDA NA KWENDA KUISHI NISIKOPENDA ILI KUTIMIZA NDOTO YA MUME WANGU?

*Niko tayari kuingia ukoo mwingine na kuufanya kuwa ukoo wangu, watu wake wawe watu wangu na Mungu wao awe Mungu wangu?

*Ikitokea umeolewa na Mume wako akapata shida ghafla mfano Ugonjwa na akashindwa kutunza familia, una mbinu gani mbadala ya kuendesha maisha yenu mpaka atakapopona na kusimama tena?

*Una uwezo wa kubeba majukumu kama Mama maana kuzaa ni jukumu lingine kabisa?

*Tabia yako vipi? Inafaa kuwa mke wa mtu? Au unahitaji muda kwanza na uhuru ujirushe ukichoka ndio utulie uolewe?

*Kuna msemo "Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke" ukijiangalia wewe una uwezo wa kumshauri mtu akafanikiwa? Na hilo tunalipima kwa kuangalia ni nini ambacho binafsi umefanikisha katika maisha yako.

*Moja jumlisha moja huzaa mbili, wewe una moja gani ya kuchanganya na moja aliyonayo mume wako mkazalisha mafanukio? Au unaenda kuwa Mama wa Nyumbani na mzigo.

Ulishwe, uvishwe, upewe kila kitu wakati hakuna unachozalisha?
Nadhani kuna mambo ya maana ya kufanya, kupanga na kujiandaa kabla hujawaza rangi ya harusi (Wedding colour), keki ya ngazi saba na hotel ya kwenda Honeymoon. Me nimemaliza.

Kwa usawa huu hakuna mwanaume anataka kuoa mzigo.

Usije ukaishia kufurahia harusi na baada ya mwaka ukaanza kutafuta Washauri wa Ndoa.

Think before U take Decision
Hakuna ndoa kwenye kizazi dhaifu katika kufikiri.
 
Back
Top Bottom