Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,173
- 40,524
Habari za asubuhi wapendwa wana MUM.. ..
Leo nawasimulia nilichokiota usiku wa leo si kuwa mnitafsirie bali natamani nikilala leo iendelee ilipoishia leo. Naomba nianze simulizi kama ilivokuwa bila kuongeza wala kupunguza neno. Najua wengi husema ndoto ni matokeo ya ulichokiwaza wiki yote au siku moja kabla au ulochokiona au kukisikia au kumbukumbu tuu imeamua kujirudia.... kiukweli Nina miezi mitano sasa nikimaanisha tangu December mwaka jana -2016 sikuwa nimewailiana wala kuonana na mhusika mahsusi kama mhusika mkuu kwenye ndoto aka steringi.
Jana baada ya kazi za kutwa nzima nilirudi nyumbani mapema tuu kwenye saa 12 jioni nilikuwa nyumbani tayari. Baada ya muda nikatoka na kwenda mahali huko nilikaa hadi saa 7 usiku hivi ndo nikarudi kulala. Watu nilikuwa nao jana tuliongea zaidi habari za siasa na tulicheza mziki sana bila kugusia masuala ya mapenzi.
Saa nane narobo usiku ndo navuta shuka kulala. Sikuchukua zaidi ya dakika kumi usingizi ulinichukua na ndoto ikaanza.
Tulikuwa watu wengi kama kusanyiko flani hivi ambao baadhi walitakiwa kusafiri kama vile kusafirisha msiba kwenda kuzika mahali. Nami nilikuwa mmoja ya wasindikizaji bila kutambua msafara huo ni wa nani ila nilimtambua dada mmoja hivi kwa sasa anaishi marekani ni mweupeee ni mdada wa kinyaturu. Huyu tulikaa wote mtaa mmoja wakati tunaishi na wazazi wetu bongo.
Basi baada ya msafara kuondoka nikawa nasogea mahali maeneo hayohayo kulikuwa na mgahawa ambao una mitimiti mingii wakati naangalia pa kukaa, nikamuona jamaa... yeye hakuniona alikuwa anakula nyama kwa haraka haraka ilikuwa kitimoto zile mbavu. Akiwa anabirudika na msosi wake nikakosa hamu ya kula ghafla nikakumbuka historia.
Huyu bwana tulikuwa washikaji kisha tukawa marafiki kisha wapenzi ila hatukuwahi kuonana uso kwa uso nikimaanisha kuonana ana kwa ana. Tulikiwa na urafiki wa on and off ila tulielewana sana. Shida yetu moja kila mmoja wetu anajiskia anamaringo na ngumu kukishusha hivo tukinuniana hakuna anayemuanza mwenzie na ndo hadi leo tumepotezana mazimaaa huu mwezi wa tano sasa unaingia wa sita.
Sasa waweza elewa kwanini kwenye ndoto baada ya kumuona hamu ya kukaa kwenye mgahawa iliniisha na hamu ya kula ilipotea. Kiukweli yaweza kuwa yeye hakunipenda upeo niliompenda mimi... nilishindwa kujizuia hisia zangu ndomaana sikuwa radhi kuonana nae au hata kukaa meza ingine na yeye akiwa mgahawa huohuo. Sio kuwa nimemchukia hapana, naona bado nashindwa kujishusha na hii imetokea hadi kwenye ndoto nikaamua kumkwepa ili nikalie mbele.
Nikiwa naondoka ghafla akatokea kaka mmoja hivo nilisoma nae chuo tena huyu kaka alikuwa mlokole mrefu hivi, basi akaniona akaniita kwanguvu Kasinde kiasi kwamba yule jamaa yangu atakuwa alisikia. Nikageuka na kumuangalia akanisogelea kwa hatua kubwa tukaanza kusabahiana. Baada ya salamu ikawa tunaagana kila mtu aendelee na hamsini zake huku juyo kaka niliyesoma nae chuo akiwa mchangamfu kwelikweli. Nikatoa mkono wa kulia ili tuagane jamaa akatanua mikono yake na kunisogelea akimaanisha kunikumbatia..... looh ikabidi nirudishe mkono wangu na kupokea kumbato. Basi tukaagana na kuanza kutaka kuondoka.
Kumbe wakati jamaa wa chuo anasalimiana na mimi yule mtu wangu aliona tukio zima na alipoona tunakumbatiana akainuka kwenye kiti chake na mfupa wake wa mbavu mkononi na kuja kusimama nyuma yangu.
Mie baada ya kuona sekunde za kumbato zimefika nikawa najinasua kwa kurudi nyuma kama hatua moja ili tuagane kila mmoja aende kivyake wakati huohuo nikitaka kutoka eneo la tukio ili jamaa yangu asinione.
Ile najinasua kwenye kumbato na kurudi nyuma hatua moja nikamgonga jamaa yangu na mfupa wake kugeuka nyuma ni yeye looh nikaishiwa pozi. Palepale nikajihisi niko rojorojo horohoro sijiwezi sijitambui maana nilihisi tako langu liligonga usawa wa zipu yake na kuhisi kitu.
Yule jamaa wa chuo alipoona nimelegea kwa jamaa yangu na mfupa wake mkononi akasepa huku uso wake ukiwa hauna tabasamu tena. Baada ya hapo nikajishangaa nafuata amri tuu kila nnachoambiwa natii na kufanya bila shuruti. Nikashikwa mkono Kasie mie hadi kwenye meza yake akalipa bili na kaagiza chakula kingine akimaanisha chakwangu.
Akasema twende bila kujua tunaenda wapi, nikawa naelekea uelekeo wa kuondoka eneo hilo, akanipiga kibao cha mahaba cha matako na kusema heey mie niko hapa njoo huku looh kumbe alikuwa anakaa hoteli hiyohiyo yenye huo mgahawa. Akanishika mkono kuelekea chumbani tumefika hadi mlangoni Ile tunafungua mlango akaja mhudumu akasema naomba mje kuosha miguu yenu tafadhali. Vyumba vya hiyo hoteli viko kama vile cya ledger plaza hotel kama vijumba jumba juu na chini. Basi mie nikarudisha mlango nikawafuata huko kuosha miguu nikiwa sielewi maana yake ni nini. Nikaingizwa kwenye kidimbwi maji yake mausi jamaa yangu nae akaingia kisha kuna mahali tunapita upande wa kushoto ni ukuta na kulia pako wazi na chini kuna mto ukiteleza unadondoka. Nikaogopa kupita basi jamaa yangu akatangulia mie nikasubiri hapo weeh hakurudi. Funguo za chumbani kwake nnazo sioni mhudumu wala yeyote wa kumuuliza. Nikaenda kwenye kile chumba nikaingia ndani nikalala.... hadi panakucha nastuka niko kitandani kwangu mwenyewe huku alarm inaita nikachukia na kujaribu kulazimisha kurudi kulala ili niendelee kuota nimsubirie jamaa yangu aje waapi....
Usingizi haukuja na ndoto ukaishia hapo. Najua naota ndoto nyingi sana kila siku ila hadi hii nimeisimulia hapa kuna jambo...
Haya acha ibaki kuwa ndoto tuu, labda nyege zimenijaa..... Nawatakia nyote wikiendi njema.
Mniwie radhi kwa simulizi yangu ndefu wale mtaokwazika maana huwa siwezi kufupisha habari.