Ndondocha na utajiri

mmmmh hatar sana hii...ni bora umasikin kuliko shirki ya namna hii...tujiepushe na haya mambo wapendwa cha msingi ni kufanya kazi kwa bidii na kumuogopa mungu kwani kudhulumu nafsi ya mwingine ili upate utajir hii ni laana iliyotukuka kabisa yaani..
 
Ningependa kupata definition ya 'ndondocha'. Yaani ndondocha ni mtunwa au mtu aliyezubaa,au nini. Ningependa kupata definition ili nijue kama inafanana na kitu chochote ambacho nimewahi kusoma.
Ni mtu anakuwa yupo yupo tu kama punguani si punguani, hana maamuzi binafsi hawezi fanya lolote ni kama kalemaa akili ndo maana wengi huwekewa wasaidizi karibu muda wote
 
Siku moja nilimsikia Mdogo wangu akiongea na simu na akawa anamwelekeza rafiki yake aliyempeleka kwa waganga kua yuko kwenye tafakuri amtoe nani?
Mama au bro (mimi)
Pum*bu zilipanda tumboni siku 6
Kwa Bahati mpaka sasa hakuna mtu katolewa
 
Mimi pia hili ni moja kati ya maswali mengi ambayo sijayapatiaga majibu

Sielewagi uhususiano wa haya mambo ya kufanya mtu ndondocha,msukule na kutoana kafara vinasaidiaje mtu kupata utajiri

Labda ntajaribu Google
 
Hakuna utajiri unaokosa masharti tatizo yasiwe mabaya....
Masharti ya nidhamu na kujali muda na kila sent sio mabaya
Bora Nikalime xx... Ila Kuna mambo Mengi sanaaa Behind mpk mtu anaamua kwenda Kwa mganga Kuchukua Utajiri wa namna Hiyo
 
Bora Nikalime xx... Ila Kuna mambo Mengi sanaaa Behind mpk mtu anaamua kwenda Kwa mganga Kuchukua Utajiri wa namna Hiyo
Kuna watu ni aggressive kwenye hili wanachojali ni kupata utajiri wa haraka bila kujali utapatikanaje na madhara yake ya baadae
 
Hata anamfanya nduguye kuwa ndondocha nae pia ni ndondocha...unaharibu akili ya mtu afu unapasua kichwa jinsi ya kupata pesa! Haribu afu ukae tuu bila shuguli ukiamka uwe unakuta mlundo wa pesa mchagoni
wewe kazi yako ni kula bata hadi kuku washangaeee
 
Huyo ni msukule sio ndondocha, kwakuwa ndondocha hahitajiki kufa na hufanywa ndondocha na ndugu yake wakati msukule ni mambo ya wachawi wanaweza kumchukua yeyote
Hapa umenijibu Mshana Jr swali ambalo nililokuwa najiuliza, tofauti ya ndondocha na msukule. Ila mkuu Kama unaweza fafanua zaidi tafadhari, Mshana Jr.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…