Ndoa zina matukio jamani

Ndoa zina matukio jamani

Haswa za kizazi hiki.

Usaliti umekuwa kitu cha kawaida, magomvi kama yote, wengi wanafeki furaha ila ndani kunafurukuta. Matukio ya kutisha, najiuliza walewale waliokuwa wanacheza romantic songs sijui blues kwa hisia na upendo ndo hawahawa leo wanakimbizana na mapanga?

Wamechafukwa hawatamani kuonana tena, ndo hawa kila mmoja kamchoka mwenzake? Wanapigana wengine wanauana.

Ndoa imekuwa kifungo cha maumivu, nimeshuhudia wengi wakiteseka kihisia, kimwili, kiroho nk

Ndoa sio salama tena imekuwa njia ya kujipatia magonjwa ya kila aina, ukitaka magonjwa yote ingia kwenye ndoa na malaya asiejua kuridhika wala kutulia. Ndoa zimegeuka tanzi na mtego.

Hata ukiweka vigezo 100 lakini ukweli watu hubadilika kutokana ma situations zinazotokea maishani. Mpaka baba mchungaji anachepuka. Ukiyumba kiuchumi kidogo tu mwenzio kakukimbia. Ukipata hata ajali ukilala tu kitandani mwenzio anaomba talaka ama anahamia kwa mwingine.

UKITAKA KUINGIA KWENYE NDOA JIPANGE NA UWE NA ROHO NGUMU!
Mkuu mbona kama
"Unatufokea...
 
Ndoa ni jambo la kheri na changamoto ndio zinazofanya tunaishi japo sikuhiz ukiingia ndoan ni kama umeenda jela
Kuna mtu alsemaga ukiingia ndoani miaka hii hakikisha unajifanya akili zako sio timamu 😃😃
Ila ndoa raha kila mtu akiwa anajua thamani ya mwenzie.

Bahati mbaya watu sasa wanaishi nyumba moja ila wapo matumatu hawaaminiani tena.
 
Bro kutambua thamani ya mwenzio na to cherish it ni jambo linahitaji maamuzi yasiyo na unafiki ndani yake...
Tatizo ni wanawake ...Mwanamke anaweza kuishi na kuolewa na mwanaume ambaye hampendi labda kalazimishwa na wazazi ila mwanaume hawezi kabisa.


Mbaya ni kwamba duniani unajua tu mtu unayempenda na humjui anayekupenda.
 
Komenti yako ya kwanza nimeipotezea, ila sasa naona umedhamiria
Yaani kama unanisema mimi

Mimi huwa ninaamini ndoa inahitaji uingie na akili zako timamu, ila wewe unasema tusiingie na akili timamu

Usinivuruge tafadhali
😃😃Ndugu usifanye hilo kosa la kuingia na akili namaanisha unaoana na mtu hamfanani chochote hawez kuwa unavotaka Sasa ukitaka utimamu 💯 ndo utaharibu inabid nawe ulegeze fuvu 😂😂
 
Ndoa ni jambo la kheri matatizo ni sehemu ya maisha SEMA yanapozidi Inakuwa mateso so tuelezane ukweli kwani mnapokuwa wanandoa ninyi ni kitu kimoja tujitahidi kuzikumbuka ahadi zetu kuanzia kwenye uchumba Hadi ndoa.yale majina tuliyokuwa tukiitana wakati wa uchumba tusiyaache.mbna mambo yatakuwa vizuri tu.
Komenti tulivu sana.

Unajua hili suala la ndoa watu tunalikompliketisha sana.

Ni kweli ndoa za siku hizi zimekuwa ni delicate sana, na zina misukosuko mingi.
Lakini hii haina maana ndoa ni jambo lisilofaa.
 
Back
Top Bottom