Ndoa za wake wengi katika ukristo

Ndoa za wake wengi katika ukristo

Wewe oa wanne kijana,ikiwa biblia imemuongelea huyo 'mshikaji' alizaa na wanawake wanne sasa why uwe na mashaka?achana na sheria za Italia,chukua maandiko ya mungu,fata nyayo za Jacob tu sasa maana hakuna namna...!
We jamaa fala sana hahaaa!!!!
 
Lakini mwisho wa siku akanyanyua mikono juu na kumkosea muumba wake
Wewe ulweso wewe manabii wenyewe watumishi Kama Jacob na elkana hawakutosheka na mke mmoja wakaoa wake wengi,ndo tusioe wanawake wengi wanaume wa 2018,??? hakuna mwanaume anayeweza kukaa/ kutosheka na mke mmoja dunia hii, hayupo na hatokuja awepo hata mumeo anachepuka sema tu hujajua,
 
Tuko chini ya agano jipya. Fata kilichopo ndani ya agano jipya na agano la kale libaki kukufundisha mambo ya zamani na historia. Ila kizazi chako kipo chini ya agano jipya. Kila laheri.
 
Tuko chini ya agano jipya. Fata kilichopo ndani ya agano jipya na agano la kale libaki kukufundisha mambo ya zamani na historia. Ila kizazi chako kipo chini ya agano jipya. Kila laheri.
Yesu hakuja kutengua torati Bali kutimiza
 
Uliyesema Mungu aliumba Adam na Eva tu , naona alikosea angeumba Adam wengi na Eva wengi kuepuka mtu kuzaa na dada yake
 
Ahsante kwa hii

Nimejifunza vingi
JE MUNGU ALIRUHUSU MATALA(MITAALA)?

Sehemu ya Pili

Karibu mwana wa Mungu tuendelee na sehemu ya pili ya somo letu. Tulikuwa tumefikia kuangalia mifano ya matala ndani ya biblia na matatizo yaliyotokea kwa matala hiyo kwa sababu ni kinyume na neno la Mungu.

Hebu sasa tuangalie kanuni za kibiblia ambazo zinaenda kinyume kabisa na matala au mitaala ndani ya jamii zetu hasa waaminio. Neno La Mungu:-
“ Kwahiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe…..” Mwanzo 2:23-24.

Mungu hakusema mwanamume ataambatana na wake zake. Alisema mume ataambatana na mkewe yaani hapo ni mtu mmoja mume na mtu mmoja mke.

Mtume Paulo anafananisha mume na mke kama Kristo na kanisa “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa” Efeso 5:23 halafu ukisoma kwenye kitabu cha efeso 1:22-23 inasema kuwa kanisa ni mwili wa Kristo. Kwahiyo kuna mwili mmoja tu (Efeso 4:4). Kristo anayefananishwa hapa alikuwa na kanisa , ndiyo maana efeso 4:4 inasema “mwili mmoja, Roho mmoja”. Paulo alimfananisha Kristo na kanisa kwa sababu Yesu alikuwa na kanisa moja tu, kadhalika mume anapaswa kuwa na mke mmoja tu. Hakuna sehemu biblia inasema mume mmoja na wake wengi halafu hilo jambo likawa sawa kwa Mungu.(Rudi usome sehemu ya Kwanza utaona)

Mathayo 19:3-9 inazungumzia kuhusu talaka. Yesu anaonesha kuwa Mungu hakutaka wana ndoa kupeana talaka, vile vile katika masuala ya matala Mungu hakuruhusu tangu alipomuumba mwanadamu wa kwanza. Mungu hataki mume awe na wake wengi au kwa lugha hajaruhusu matala, kinachoendelea ni sisi wenye tumejiamulia!!!!! Yesu anasema “mume atamuacha baba yake na mama yake na ataambatana na mke wake nao watakuwa mwili mmoja”
Yesu alinena kuhusu mwanamume (mmoja) na mwanamke (mmoja) kuwa mwili mmoja. Alisema kuwa ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja tu na sio mume mmoja na wake 10 au mke mmoja na wanaume 20!!!Hili ni kinyume na Mungu wetu na afanyaye haya atenda dhambi na ni chukizo kwa Mungu Baba Yetu.

1 Timotheo 3: inasema juu ya kiongozi kuwa ni mume wa mke mmoja, kadhalika mwanamke kwa mume mmoja, ambapo tunaweza kujiuliza kwanini isiwe ni matala, yaani awe ni mume wa wake wengi? Kwanini neno la Mungu limezuia matala? Ni kwa sababu Mungu HATAKI NA HAJARUHUSU MATALA!! Wafanyayo hayo wanatenda dhambi mbele za macho ya Mungu na hawapaswi kuwa viongozi wa dini au kanisa wala hawapaswi kuitwa watu wamchao Mungu au watu waliookoka wala waumini wa kanisa wala wafuasi ya Yesu Kristo. Kondo huijua sauti ya Bwana wake na kuifuata, je tumeisikia sauti ya Bwana wetu na kuifuata??

Kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili nimeongelea baadhi ya matatizo yanayoweza kusababishwa na matala, na pia hata yaliyowakuta wale walioishi maisha ya namna hiyo. Ndoa zao hazikuwa na furaha na waliacha kusudi la Mungu kwa kuendekeza tamaa za miili yao isiyoridhika na mume na mke mmoja au mke na mume mmoja.

> Kwanza, Uomvi na wivu mkubwa. Tunayaona haya kwa wanaoishi kwa matala hivi sasa. Unajua Yusufu aliuzwa na ndugu zake kuwa mtumwa Misri kwa sababu ya wivu uliotokana na matala, Yakobo alikuwa na wake wengi ugomvi na wivu ukaibuka

> Hakuna mwanamume atakayekuwa sawa kwa wake wengi, italeta shida kwa mmoja na matokeo yake ni dhambi kubwa kwa Mungu.

> Unawezaje kuwalea watoto katika adabu na maonyo ya Bwana kama ilivyozungumziwa na Efeso 6:4 wakati una wake 30 na watoto 50? Tuliona hili kwa Gidioni. Hata kama utaweza lakini Mungu alizuia tangu mapema!

> Matala itamsababisha mume kukengeuka na Mungu wake, na kutokuwa karibu na Mungu. Kumbuka hili kwa Sulemani!

Kwa mtu anayeishi kwa matala huyu sio mkirsto yaani hajaokoka na Yesu sio Bwana na mwokozi wake. Yesu alileta Neema duniani ya mtu kutambua kosa na kutubu.

Swali litabaki, Davidi nifanyeje kwa sababu tayari niko ndani ya matala na ninamtaka Yesu? Mwanadamu anapaswa kutambua kuwa amepotea na ametenda dhambi, halafu amwamini Kristo mwana wa Mungu (Marko 16:16, Inasema Aaminiye na kubatizwa ataokoka: asiyeamini atahukumiwa). Kufuata imani ya Kristo lazima kutubu (Matendo 2:30, Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipwa cha Roho Mtakatifu)

Tunapaswa kuzikana dhambi zote katika maisha ya mtu anayeishi kwa matala. Na katika ndoa zake za mitaala anapaswa kuwaacha wanawake wengine wote wawe huru isipokuwa mke wake wa kwanza au lugha nyingine mke mkubwa. Baada ya kutubu na kuacha, mtu huyo lazima amkiri Yesu maana biblia inasema, Warumi 10:10 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” baada ya ukiri huu wa imani sasa mtu huyu naweza kubatizwa, na ubatizo huu ni kuzikwa kwa mambo yote ya nyuma na mtu huyu anakuwa kiumbe kipya (Warumi 6:3-4) kwa ondoleo la dhambi. Hii ndiyo njia ya mtu anayeishi kwa matala anapswa kufanya ili kuwa mkristo na kuwa mfuasi wa Kristo.
Kwahiyo turudi kwenye kichwa chetu cha somo "JE MUNGU ALIRUHUSU MATALA(MITAALA)?" Jibu lake hapa bila kumung'unya maneno maneno ni kwamba Mungu hakurusu matala na yanayoendelea tumejiamulia wenyewe baada ya kumuasi Mungu.

Mungu akubariki sana,

Davidi Chacha
25th August, 2017
 
Adamu alikuwa anaishi na wanyama tu hivyo hakuwa na wakufanana naye zaidi ya nyumbu tembo na nyati
Ukisoma vizuri Biblia Mwanzo . Tafuta mwenyewe sikutafunii ' hapo Mwanzo Mungu aliumba mtu mume NA mke . Ukiendelea mbele utaona Mungu alimtoa Adam na upweke akampa usingizi mzito kisha akamtoa ubavu akapatikana mke . Na Adam alipomwona akafurahi akasema huyu ndio mke hasa katokana na ubavu wangu . Yule wa mwanzo alienda wapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa sawa kiuchumi , oa kadiri unavyojisikia ila utoe haki kwa wote . Achana na uwongo wa kanisa wewe piga harusi za kiserikali kwa kwenda mbele . Wenye mke mmoja wanafanya maajabu mtaani , nafuu tu wahalalishe hizo nyumba ndogo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Mungu alitoa mbavu ngapi kwa Adamu? Si alitoa ubavu mmoja tu, yaani Eva? Sasa kama unaamini ubavu wako ulitawanywa kwa akina "Eva" wanne basi oa wake wanne.
Hivi ni kweli Adam na Hawa ndio viumbe wa kwanza duniani,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom