Ndoa za wake wengi katika ukristo

Ndoa za wake wengi katika ukristo

Biblia inasema hivi kuhusu ndoa...

1/Mungu aliumba mtu mume(Adamu) na kisha mtu mke(Hawa).

2/Mungu alimfanyia Adamu msaidizi(mke) wa kufanana naye.

3/Mwanaume ataachana na wazazi wake na kuambatana na Mkewe.

4/Na kwa sababu ya kuepuka zinaa, kila mtu awe na mke wake mwenyewe.

5/Mwanaume ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.

6/Apataye mke kutoka kwa Mungu, basi apata kitu chema.

7/Mwanaume amfurahie mke wa ujana wake.

8/Mwanaume na ampende mkewe, na mke anapaswa kumtii mumewe.

9/Alichokiunganisha(Ndoa) Mungu, mwanadamu hana mamlaka ya kukitenganisha.

10/Ndoa ni Agano la milele baina ya Mke na Mume, ni kifo tu kinachoweza kuwatengenisha.

12/Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Umezungumza vema sana, isipokuwa namba 10 kwenye umilele. Ndoa sio agano la milele nadhani ulitaka kusema mtu hapaswi kutengana na mwenza wake hadi kifo kiwatenganishe.

vv
 
Katika Biblia Jacob alifanikiwa kuzaa na wanawake 4, kupitia hao wanawake 4 akazaa nao watoto 13, na hapo ndipo yakapatikana mataifa 12 ya Israel, hili limekaaje? Sasa kama Jacob alikuwa na wanawake 4, kwanini na mimi nisiwe na wanawake 4?

Wajuzi wa biblia mje hapa, waislamu tafadhali sana msilete matusi wala chuki za kidini.

ndugu yangu usisome biblia kama unasoma kitabu cha stori, Yesu kristo alipokuja Duniani aliyafuta hayo yote usisome Mwanzo tu, kasome na vitabu vyote vya agano jipya, sasa wewe kaoe wanawake wa 4 uone kama mbinguni utaingia
 
ndugu yangu usisome biblia kama unasoma kitabu cha stori, Yesu kristo alipokuja Duniani aliyafuta hayo yote usisome Mwanzo tu, kasome na vitabu vyote vya agano jipya, sasa wewe kaoe wanawake wa 4 uone kama mbinguni utaingia
Dada faith kwani biblia inasemaje KUHUSU ndoa
 
Kweli sisi wakristo tumepewa agano jipya baada ya Kristo kufa msalabani.
Ndio maana hata zile adhabu za kule agano la kale hazitumiki tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kristo Yesu alikuja duniani sio kwa ajili ya kutengua torati bali kukamilisha torati.
“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, HATA YOTE YATIMIE” (Mathayo 5.17-20)
Tumaina la wakristo wote wali hai ni kwamba hatuesabiwi haki kwa njia ya sheria bali ni kwa neema ipatikanayo katika Kristo Yesu. Hii inamaanisha sheria zote zimefunikwa kwa Neema ya Yesu Kristo kwa njia ya msalaba na ufufuo. Bwana Yesu asifiwe sana kwa kutuokoa kutoka utumwa wa sheria.
 
JE MUNGU ALIRUHUSU MATALA(MITAALA) AU TUMEJIAMULIA?

Sehemu ya Kwanza

Bwana asifiwe mwana wa Mungu. Karibu katika somo lingine kuweza kuangazia baadhi ya mambo ndani ya jamaii
Matala au (‘mitaala’ kama ilivyozoeleka na wengi) ni ndoa zinahusisha mwanamume mmoja kuoa wanawake zaidi ya mmoja, yaani ndoa ya wake wengi. Kuna baadhi ya jamii hasa bara la Afrika, matala ni jambo la kawaida namakabila mengi Tanzania, na baadhi ya dini zimeruhusu matala lakini kwa maelekezo au vigezo kadhaa vya kutimiza.

Kwa sababu matala imekuwepo kwenye jamii yetu kwa muda mrefu basi watu wengi wanadhani ni sawa na kwamba hakuna shida. Hii sio sawa kabisa mwana wa Mungu, hatuwezi kukubali vitu kwa sababu tu eti vilikuwepo tangu zamani za mababu, na ukumbuke kabla hao mababu hawajakuwepo, Mungu alikuwepo. Ili jambo likubalike lazima Mungu alikubali,yaani lazima iwe sawa na neno, na usije kwangu eti ooooh David,mimi nimefunuliwa kuwa na matala(mitaala), nitakukemea na kibao kama kikikufikia basi Mungu atanipongeza.

Mbaya zaidi siku hizi hata wanawake wana ndoa za wanaume wengi, ajabu kabisa!Mungu atusamehe sana.
Mtazamo wa Mungu(Neno) ni upi sasa kuhusu matala? Ndoa ni taasisi iliyoasisiwa na Mungu hapa duniani. Mungu alimfanya mwanadamu wa kwanza, Adamu, ambapo neno linasema:-

“Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu….” Mwanzo 1:26

Mungu akaona sio vyema Adamu awe peke yake(Mwanzo 2:18), akamfanyia ‘Mke’ msaidizi. Mungu hakumfanyia Adamu “Wake” yaani “wives” kwa kiingereza.

Na kama Mungu angetaka Adamu awe na mke zaidi ya mmoja basi Mungu angemfanyia mke zaidi ya mmoja. Kwahiyo mmoja tu na Mungu akaona inatosha. Mungu anajua zaidi kuliko mimi na wewe mwanamke mwenye mume zaidi ya mmoja au wewe mwanamume mwenye mke zaidi ya mmoja.
Kwa sababu ya tamaduni zetu tunazoishi na makabila yetu tumejikuta tumeleta mawazo mengi sana duniani kuhusu ndoa tofauti kabisa na Mungu alivyowaza juu yetu.

Tumekuja kuibomoa hii taasisi. Kuna baadhi ya mawazo yetu yanakubaliana na mipango ya Mungu na mawazo mengi tuliyojiletea yanapinga mipango ya Mungu juu yetu. Na hii ndio kweli kuhusu matala au mitaala. Kwahiyo suala la matala au mitaala ni moja ya mawazo yetu sisi wanadamu tuliyojiletea kwenye ndoa zetu kwa sababu ya tamaduni zetu jambo linalokinzana na neno la Mungu.

Kwahiyo itoshe kusema kwamba matala sio makubaliano yetu na Mungu juu ya ndoa. Kumbuka kila jambo ambalo haliendani na kile Mungu alifanya, alichosema Yeye basi ni dhambi. Mpango wa Mungu ni mume mmoja na mke mmoja. No more No less(Soma mwanzo 2)

Hebu tuangaliebaadhi ya mifano ya matala au mitaala ndani ya biblia.

>Mtu wa kwanza kupotoka na kuingia kwenye matala alikuwa ni Lameki, alikuwa na wake wawili, Ada na Sila(Mwanzo 4:19-24) na biblia inamsema kabisa kuwa alikuwa ni muuaji.

>Ibrahimu alikuwa na matala pia(Mwanzo 16:1-5). Mkewe Sarai hakuwa na uwezo wa kuzaa, akaamua kumpa kijakazi wake kwa mumewe. Hajiri alizaa motto kwa Ibrahimu. Biblia inasema Sarah akawa na wivu juu ya Hajiri. Ndoa hii ilikuwa ndoano haswaaa.

>Matala nyingine ilikuwa kwa Esau. Alikuwa ni mtoto wa Kwanza wa Isaka na Rebeka. Esau alioa wanawake wawili wahiti (Soma mwanzo 26:33-34). Wakasababisha mateso kwa Isaka na Rebeka. Kwahiyo matala madhara yake sio kwa mume na mke peke yake kwani tunaona hapa matatizo yalienda hadi kwa Isaka na Rebeka, Baba na Mama wa Esau, au Baba mkwe na mama mkwe wa wake wa Esau.

>Gidioni alikuwa shujaa na kiongozi hodari. Alikuwa na watoto wa kiume 70 kwa wanawake tofauti (Waamuzi 8:30-31). Unadhani angekuwa baba wa aina gani kwa watoto wa kiume tu 70, hapo hatujaambiwa idadi ya watoto wa kike? Je ndio ambavyo Mungu anataka sisi akina baba tuwe?

>Mfalme Sulemani alikwa na wanawake 700, na Masuria 300. Huyu alivunja rekodi!! Biblia inasema wake zake wakaugeuza moyo wake usimwelekee Mungu (1 Wafalme 11:3). Anguko lake kubwa lilisababishwa na matala, alikiuka kanuni ya Mungu, Neno linasema “Wala asijizidishie wake ili moyo wake usikengeuke…” Kumbukumbu la Torati 17:17

Hakuna sehemu kwenye biblia ambapo matala imefanya vyema, au wamemaliza vyema mbele za Mungu. Kila tulichoona hapo juu kilisababisha matatizo, na hiyo haijabadili kitu. Hata sasa hilo halijabadilika,matala hadi sasa imesababisha matatizo makubwa kwenye ndoa za leo. Naandika haya ikiwa tayari wapo wanaolia na waliojela kwa sababu ya matala. Kuna yatima wengi kwa sababu ya matala. Kuna biashara nyingi zimekufa kwa sababu ya matala. Familia nyingi zimesambaratika kwa sababu ya matala, na kwenye hili la matala kuna wengine ni siri lakini siri hii ni kwao na sio kwa Mungu.

Tutaendelea na sehemu ya pili............

Mungu akubariki

Davidi Chacha
August 24, 2017
 
JE MUNGU ALIRUHUSU MATALA(MITAALA)?

Sehemu ya Pili

Karibu mwana wa Mungu tuendelee na sehemu ya pili ya somo letu. Tulikuwa tumefikia kuangalia mifano ya matala ndani ya biblia na matatizo yaliyotokea kwa matala hiyo kwa sababu ni kinyume na neno la Mungu.

Hebu sasa tuangalie kanuni za kibiblia ambazo zinaenda kinyume kabisa na matala au mitaala ndani ya jamii zetu hasa waaminio. Neno La Mungu:-
“ Kwahiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe…..” Mwanzo 2:23-24.

Mungu hakusema mwanamume ataambatana na wake zake. Alisema mume ataambatana na mkewe yaani hapo ni mtu mmoja mume na mtu mmoja mke.

Mtume Paulo anafananisha mume na mke kama Kristo na kanisa “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa” Efeso 5:23 halafu ukisoma kwenye kitabu cha efeso 1:22-23 inasema kuwa kanisa ni mwili wa Kristo. Kwahiyo kuna mwili mmoja tu (Efeso 4:4). Kristo anayefananishwa hapa alikuwa na kanisa , ndiyo maana efeso 4:4 inasema “mwili mmoja, Roho mmoja”. Paulo alimfananisha Kristo na kanisa kwa sababu Yesu alikuwa na kanisa moja tu, kadhalika mume anapaswa kuwa na mke mmoja tu. Hakuna sehemu biblia inasema mume mmoja na wake wengi halafu hilo jambo likawa sawa kwa Mungu.(Rudi usome sehemu ya Kwanza utaona)

Mathayo 19:3-9 inazungumzia kuhusu talaka. Yesu anaonesha kuwa Mungu hakutaka wana ndoa kupeana talaka, vile vile katika masuala ya matala Mungu hakuruhusu tangu alipomuumba mwanadamu wa kwanza. Mungu hataki mume awe na wake wengi au kwa lugha hajaruhusu matala, kinachoendelea ni sisi wenye tumejiamulia!!!!! Yesu anasema “mume atamuacha baba yake na mama yake na ataambatana na mke wake nao watakuwa mwili mmoja”
Yesu alinena kuhusu mwanamume (mmoja) na mwanamke (mmoja) kuwa mwili mmoja. Alisema kuwa ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja tu na sio mume mmoja na wake 10 au mke mmoja na wanaume 20!!!Hili ni kinyume na Mungu wetu na afanyaye haya atenda dhambi na ni chukizo kwa Mungu Baba Yetu.

1 Timotheo 3: inasema juu ya kiongozi kuwa ni mume wa mke mmoja, kadhalika mwanamke kwa mume mmoja, ambapo tunaweza kujiuliza kwanini isiwe ni matala, yaani awe ni mume wa wake wengi? Kwanini neno la Mungu limezuia matala? Ni kwa sababu Mungu HATAKI NA HAJARUHUSU MATALA!! Wafanyayo hayo wanatenda dhambi mbele za macho ya Mungu na hawapaswi kuwa viongozi wa dini au kanisa wala hawapaswi kuitwa watu wamchao Mungu au watu waliookoka wala waumini wa kanisa wala wafuasi ya Yesu Kristo. Kondo huijua sauti ya Bwana wake na kuifuata, je tumeisikia sauti ya Bwana wetu na kuifuata??

Kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili nimeongelea baadhi ya matatizo yanayoweza kusababishwa na matala, na pia hata yaliyowakuta wale walioishi maisha ya namna hiyo. Ndoa zao hazikuwa na furaha na waliacha kusudi la Mungu kwa kuendekeza tamaa za miili yao isiyoridhika na mume na mke mmoja au mke na mume mmoja.

> Kwanza, Uomvi na wivu mkubwa. Tunayaona haya kwa wanaoishi kwa matala hivi sasa. Unajua Yusufu aliuzwa na ndugu zake kuwa mtumwa Misri kwa sababu ya wivu uliotokana na matala, Yakobo alikuwa na wake wengi ugomvi na wivu ukaibuka

> Hakuna mwanamume atakayekuwa sawa kwa wake wengi, italeta shida kwa mmoja na matokeo yake ni dhambi kubwa kwa Mungu.

> Unawezaje kuwalea watoto katika adabu na maonyo ya Bwana kama ilivyozungumziwa na Efeso 6:4 wakati una wake 30 na watoto 50? Tuliona hili kwa Gidioni. Hata kama utaweza lakini Mungu alizuia tangu mapema!

> Matala itamsababisha mume kukengeuka na Mungu wake, na kutokuwa karibu na Mungu. Kumbuka hili kwa Sulemani!

Kwa mtu anayeishi kwa matala huyu sio mkirsto yaani hajaokoka na Yesu sio Bwana na mwokozi wake. Yesu alileta Neema duniani ya mtu kutambua kosa na kutubu.

Swali litabaki, Davidi nifanyeje kwa sababu tayari niko ndani ya matala na ninamtaka Yesu? Mwanadamu anapaswa kutambua kuwa amepotea na ametenda dhambi, halafu amwamini Kristo mwana wa Mungu (Marko 16:16, Inasema Aaminiye na kubatizwa ataokoka: asiyeamini atahukumiwa). Kufuata imani ya Kristo lazima kutubu (Matendo 2:30, Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipwa cha Roho Mtakatifu)

Tunapaswa kuzikana dhambi zote katika maisha ya mtu anayeishi kwa matala. Na katika ndoa zake za mitaala anapaswa kuwaacha wanawake wengine wote wawe huru isipokuwa mke wake wa kwanza au lugha nyingine mke mkubwa. Baada ya kutubu na kuacha, mtu huyo lazima amkiri Yesu maana biblia inasema, Warumi 10:10 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” baada ya ukiri huu wa imani sasa mtu huyu naweza kubatizwa, na ubatizo huu ni kuzikwa kwa mambo yote ya nyuma na mtu huyu anakuwa kiumbe kipya (Warumi 6:3-4) kwa ondoleo la dhambi. Hii ndiyo njia ya mtu anayeishi kwa matala anapswa kufanya ili kuwa mkristo na kuwa mfuasi wa Kristo.
Kwahiyo turudi kwenye kichwa chetu cha somo "JE MUNGU ALIRUHUSU MATALA(MITAALA)?" Jibu lake hapa bila kumung'unya maneno maneno ni kwamba Mungu hakurusu matala na yanayoendelea tumejiamulia wenyewe baada ya kumuasi Mungu.

Mungu akubariki sana,

Davidi Chacha
25th August, 2017
 
Katika Biblia Jacob alifanikiwa kuzaa na wanawake 4, kupitia hao wanawake 4 akazaa nao watoto 13, na hapo ndipo yakapatikana mataifa 12 ya Israel, hili limekaaje? Sasa kama Jacob alikuwa na wanawake 4, kwanini na mimi nisiwe na wanawake 4?

Wajuzi wa biblia mje hapa, waislamu tafadhali sana msilete matusi wala chuki za kidini.
Hakuna kitu chochote unachoweza kusema kwa msingi wa biblia ambacho hakiwezi kupingwa kwa msingi wa biblia.

Ukielewa hili, utaelewa kwamba biblia ni kitabu cha hadithi zinazotaka kutumika sehemu zote, na hivyo, ujuzi wako wa kujua wapi utumie kifungu gani ni muhimu kuliko fikra kwamba biblia ina majibu ya kukupa weee muongozo kuhusu kipi ufanye.

Biblia ni kama kitabu chenye methali nyingi. Upande mmoja utaona methali ineandikwa "Haraka haraka haina baraka" kwingine utakuta methali imeandikwa "Ngoja ngoja huumiza matumbo".

Sasa hapo kama unataka kutumia kitabu hicho kama muongozo, na unataka kujua uende haraka au polepole, utatumia methali ipi?

Huwezi kusema utumie hii au ile, kwa sababu zinapingana.

Itabidibuwe na uelewa wa kina zaidi wa mazingira na sababu zilizofikia methali hizo kutajwa.

Tukirudi kwenye mfano wako. Inawezekana kabisa, biblia, katika enzi hizo za dunia iliyokuwa na watu wachache sana, iliruhusu wake wengi kwa sababu watu wengi walihitajika kujaza dunia. Na sasa dunia imejaa mabilioni ya watu, hakuna haja ya kuzaana sana, mlango huo unefungwa na kila mtu awe na mke mmoja. Kila mtu akitaka kuoa wake wengi kutakuwa na wachache wenye wake kibao na wengi ambao hawana hata wake. Hata kibaiolojia hii italeta tatizo la lack of genetic diversity.

Kwa hiyoninabidi kuielewa biblia kama kitabu ambacho kinatakiwa kusomwa sio kama chavsheria za kufuata, bali cha mythological mores blended over and in time, with an everchanging dynamic due to the needs if the time and people.

Sent from my Kimulimuli
 
Katika Biblia Jacob alifanikiwa kuzaa na wanawake 4, kupitia hao wanawake 4 akazaa nao watoto 13, na hapo ndipo yakapatikana mataifa 12 ya Israel, hili limekaaje? Sasa kama Jacob alikuwa na wanawake 4, kwanini na mimi nisiwe na wanawake 4?

Wajuzi wa biblia mje hapa, waislamu tafadhali sana msilete matusi wala chuki za kidini.
Jacob was never a Christian..
Listen what Jesus said...Marko 10:6
[6]Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Biblia Jacob alifanikiwa kuzaa na wanawake 4, kupitia hao wanawake 4 akazaa nao watoto 13, na hapo ndipo yakapatikana mataifa 12 ya Israel, hili limekaaje? Sasa kama Jacob alikuwa na wanawake 4, kwanini na mimi nisiwe na wanawake 4?

Wajuzi wa biblia mje hapa, waislamu tafadhali sana msilete matusi wala chuki za kidini.



Naona unatamani kuwa mmoja kati ya wale wenye mioyo migumu kama wa upande ule mwingine, na ndiyo maana iliruhusiwa kipindi cha agano la kali kwa kuwa watu walikuwa na mioyo migumu lakini mwanzo haikuwa hivyo.

Mathayo 19:8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

Hiyo kauli ya mwisho kwenye mstari inaonyesha kipindi cha Musa mambo yalibadilika kutokana na watu kuwa na mioyo migumu. Watu waliishi kidunia na kusahau kuishi kiroho. Je huko mwanzo ilikuwaje?

Mathayo 19: 4-5; Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, + na akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Sasa ulitakiwa uende ukasomwe kitabu cha mwanzo ni sababu zipi Mungu alimuumba Adam na hawa na ni maagizo gani aliwapa.

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Lakini Mungu pia akawapa maagizo kama ilivyoandika kwenye kitabu cha Mwanzo.

Mwanzo 1: 28; Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Sasa unatakiwa kujiuliza maswali

je ukiwa na mwanamke mmoja hamuwezi kuzaa na kutimiza maagizo ya Mungu?
Je kama kulikuwa na umuhimu wa kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja kwanini Mungu hakufanya hivyo?
Je kuwa na wake wengi ni kutimiza maagizo au ni tamaa tu?
Je Mungu anazungumziaje wenye tamaa na wasiotosheka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom