Ndoa yangu ipo mashakani nisaidieni

Ndoa yangu ipo mashakani nisaidieni

Haaaa....mimi mwenyewe sasa hivi nimevunjwa nguvu na baadhi ya watu wanaoandika ili tu kufurahisha genge na kubeza ndoa...sasa majina yote mazuri yeye anachagua hili ...mimi ni mmoja wa wasioamini kuwa hakuna maana yeyote kwenye avatar...

Maandishi yake yanaonyesha yuko humble...avatar inamuonyesha ni arrogant...ushauri pekee ni abadili tabia
ahahaaaaa jamani
 
Mume wangu nampenda sana
Miezi kadhaa iliyopita kuna mtu alipost humu tatizo kama hilo kwa mkewe na baadae alisema kuwa ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na fungal infection kali kwenye sehemu za uzazi na alipotibiwa mambo yakarudi sawa.
Hebu funguka zaidi kama unapata na maumivu fulani wakati mna-duu
 
Polesana bidada, ila kwa ushauri ulopewa ukiufanyia kazi utakusaidia
 
Hebu jicheki kama unaamka umechoka sana asubuhi, period yako iko consistent? Mke wangu alikuwa na hizi shida tukahangaika sana na madawa ya homone matokeo yake akawa hana hamu kabisa kwahio mzigo ikawa ngumu kupewa, Kumbe majini hayo. Nenda maombi kwa mastahi.
 
Jitahidi kuepuka mawazo yasiyohusu mapenzi wakati wa mechi.Sorry sister hivi dozi ya mnyonyo ikoje,nataka mke wangu atumie hiyo,msaada please.
 
Naamka,tunajiandaa na mume wangu,then kazini,na kazini sio busy kihiiivo,then home,napika hiyo jioni/usiku then nahakikisha shughuli zote zimemalizika then kulala full stop

kabla ya hapo ulikuwa vipi?...huwa mnatongozana kabla ya tendo...au mnakurupushana kama punda....mwenzio anajua unapopendwa kuguswa?........kuandaana sio kitandani tuu....kutwa nzima....yy huko na ww huko,,, lakini ni msg za mahabat yenu.. tena motomoto......uone kama hujatoroka kazini ukamsubiri......la sivyo umegeuza mwelekeo......kwa vijamaa ya hapo ofcn kwako... ole wako....
 
Hormones zikiwa chini huwezi enjoy sex
wala kupata hamu hata kama kuna mtu yupo moyoni
ninachoshindwa kuelewa tu ni kwamba kama huyo mtu niliyenaye hapo nampenda saaanaaaa hormones zinakuwaje chini?
Usinicheke, wengine sayansi tuliikimbia kitambo sana
 
ninachoshindwa kuelewa tu ni kwamba kama huyo mtu niliyenaye hapo nampenda saaanaaaa hormones zinakuwaje chini?
Usinicheke, wengine sayansi tuliikimbia kitambo sana

Disturbance ya hormones inaweza sababishwa na vitu vingi tofauti
mfano mimba na uzazi
mawazo na depression
madawa ya uzazi n.k...

so hata kama unampenda inaweza tokea
 
Disturbance ya hormones inaweza sababishwa na vitu vingi tofauti
mfano mimba na uzazi
mawazo na depression
madawa ya uzazi n.k...

so hata kama unampenda inaweza tokea
Asante sana kwa ufafanuzi
 
Jitahidi kuwa na hisia na mumeo, panga ratiba yako vizuri usiwe unakaa sebuleni mpaka saa sita usiku unaangalia movie hii husababisha uchovu na ukifika kitandani unawaza usingizi. Tenga muda wa kuwa na mumeo mkiwa wawili tu na ongelea mapenzi yenu.
 
una emotional shift kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto. Jaribu kuelewa tatizo hili ambalo ni lakawaida kwa kina mama. mpe mtoto nafasi yake bila kuvunja nafasi ya baba!
 
Mwanamke mji..........atavunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe!
 
Kama unatumia dawa za uzazi wa mpango (majira) inaweza iwe ndio chanzo cha matatizo yako. Taarifa hii imepatikana kutoka kwa Watumiaji wengi wa dawa hizo, muone Daktari wako. Vinginevyo mawazo yako yanakuwa mbali sana na kitendo unachotakiwa kukifanya wakati huo (kujamiana), hivyo unapoteza hisia. Cha kumalizia unaweza kuwa mapenzi kwa mumeo yameisha imebaki mazoea ama unachoka sana kimwili na kiakili kutokana na kazi unazofanya kutwa nzima.
 
Back
Top Bottom