Ndoa yangu ina dalili za usaliti

Ndoa yangu ina dalili za usaliti

kwanini hukumuachia sabuni na kutandika kitanda kabla hujaondoka?
 
Nakushangaa kama bado yupo ndani kwako saa hizi wee sumu huyo hakikisha amefika kijijiniiii haraka.
 
Tatizo ni wewe, unawezaje kuendelea na kazi zingine mme wako hajaoga, ndio maana mnasalitiwa.
 
Ni uzembe wa hali ya juu mke kuzidiwa ujanja na dada wa kazi za ndani- kalagabaho ohooooo.....
 
Wadau poleni na mihangaiko ya siku. Jamani kama kichwa cha habari kinavyojieleza naombeni ushauri plz

Juzi nilirudi home nikakuta mdada wa kazi chumbani kwangu akiwa na kanga moja wakati huo mr akiwa anaoga bafuni nilipo muhoji msichana alinijibu kuwa aliambiwa atandike kitanda na mr wangu,nilipo muuliza mr kwann yule binti yuko pale akanijibu alimletea sabuni, je hapa sijasaritiwa kweli?
Ukiona manyoya yamebaki , ujue kuku keshaliwa
 
msaliti yaweka kuwa wewe ni kwanza, kwa nini usiweke chumba chako katika hali ya utayari mda wote? 1. ulipoondoka asubuhi uliacha sabuni bafuni? 2. je ulitandika kitanda na kusafisha chumba chenu? 3. nani anayemhudumia zaidi mumeo? 4. je, umeweka mipaka kati ya HG na mumeo?
 
Wewe una bahati ya mtende,house girl anakusaidia kazi nyeti,vinginevyo mme wako angeenda kuopoa mabwabwa nje akuletee ngoma,mnunulie zawadi huyo house girl ni lock ya nyeti za mmeo.
Naona ameufanyia kazi huu ushauri
 
Dada ndoa yako si mpya bado pole wanaume ni wadhaifu sana ni rahsi kuchepuka embu jiangalie na wew kama kuna kitu unamnyima mmewako mpaka anaenda kukitafta kwa housegirl
 
Pole my dia
Piga moyo konde let it go ila ch kufanya huyo dada wa kazi rudisha kwao haraka hat kesho asubhi abebe virago vyake kwao mbigili haraka unless otherwise unafunga chatu ndani atakumeza mzim mzima!!usilie lie hapa sikuhz wanawake hatulii tunapambana na hawa viumbe so called wanaume wachepukaji
Usilete tena housegirl ,fanya kaz zako mwenyew,kama una mtoto mdogo pelka day care!!pikapakua,osha vyombo na kila kitu tupa sis watz tunajiendekeza eti msichana wa kazi uvivu tu umetujaa,mbona wazung hawana hzo mambo z mdada kukaa hapo home!!
FUKUZA KESHO ASUBH SHOSTITO
ushauri mzuri ila i dont think kama unamjua vizur huyu drama queen anaitwa monicca mama wa telemundo, sijui hii ni episode ya ngap ila namkumbusha amesahau alipoishia last time kuwa kaachana na mumewe sasa kumfumania huko tena vepee
 
Pole endelea na maisha usiwaze sana utaumia zaidi
 
ushauri mzuri ila i dont think kama unamjua vizur huyu drama queen anaitwa monicca mama wa telemundo, sijui hii ni episode ya ngap ila namkumbusha amesahau alipoishia last time kuwa kaachana na mumewe sasa kumfumania huko tena vepee
Heeh
 
Back
Top Bottom