Ndoa yangu changa inataka kuniua

Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
anajenga kwa siri, shtuka kabla hujazikwa ukiwa hai.
 
Nimeogopa sana uliposema ameiba sadaka ambayo tayari mmeiombea,huyo mwanamke hamuhofii Mungu hivyo wewe ndo hawezi kushtuka hata mshipa wa ziwa.

Hiyo ni tabia mbaya sana,jaribu kukaa kumueleza wazi wazi usiishie kuficha vitu,yani ongea nae ukimpa warning mkuu,ataleta laana kwenye uzao wako.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Kama ulidate na kuoa type ya hawa ninaokaa nao ghetto yani wanaloweka mashuka mpaka yanaoza wanayatupa, wanaosha vyombo wakitaka kupika kisha baada ya hapo wanakaa siku nne hawajaosha mpaka wakipika tena. Nakuhakikishia utaishia kumfurahia mkienda Kidimbwi tu. Sijui kushauri ndoa
Kuna wengine anakuja getto unampikia akila vyombo anaacha havitoe wala kuviosha,anajirusha tu kwenye sofa kuendelea kuangalia muvi,takataka za namna hii mimi nazipotozeaga hapohapo.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
Mnunulie mihogo amekumbuka mihogo ya chuo
 
Huenda ana deni kubwa anadaiwa embu peleleza ama laah kuna mtu anamshika akili, yaweza kuwa Ke mwenzie ama Mwanaume.
 
Mkuu hapo hapana mke umeoa jambazi!
Inaonesha pia ni kama na wewe huonyeshi mbele yake kuchukizwa na matendo yake ilihali moyoni unaumia kiasi cha kufikiria kumuua!
Sasa fanya ongea ae kinaga ubgaga, mweleze wazi kuwa umechoshwa a tabia zake na umpe msimamo wako!
Akideviate mpige chini, endelea na maisha yako wewe sio wa kwanza kuoa na kuacha mke!
Hebu jiulize mpaka hapo mke wa type hiyo ana faida gani kwako?
Siku ukipata safari ya mbali unawezakuta alishauza hadi nyumba!
Huyo ni nyani ukiendelea kucheka nae utavuna mabua!
 
CHA AJABU WAKATI UNAFUNGA NAE NDOA HAPO KANISANI ROHO YA UFUNUO HAIKUFUNUA KUWA UNAOA MWIZI!NA PADRI NA MCHUNGAJI WAKABARIKI NDOA YA MWIZI BILA ROHO KUFICHUA!!!!MAANA YAKE NI KUWA ROHO WA MUNGU HAYUPO KWENYE KANISA ULIOFUNGIA NDOA!!!
 
Mkuu, umeoa mke au umeoa mwizi?

Huyo ni mdokozi kwa asili lakini pia tabia yako ya Ubahili wa kutompa hela inakuponza.

Atauza vyote. Vitu vya ndani vitaisha, itafuata gari kisha nyumba 😂😂😂. Baada ya hapo nguo zako alafu utabakia wewe na mtoto. Nani atangulie kuuzwa?

Bila kufumba macho ni wewe. Utauzwa abaki yeye na mtoto.

Kimbia Mkuu. Mtu asiye na soni hata ya kupunguza hela ya sadaka ni mtoto wa Lucifer tu.

Kimbia. Viatu vikikatika wewe kimbia, bora miiba kuliko kuuzwa. Kimbia Mkuu.

Chaguo lako ni kukimbia ama kuamua kumpa hela zote unazopata. Chagua kwa busara.
😀😀😀
 
Kuna wengine anakuja getto unampikia akila vyombo anaacha havitoe wala kuviosha,anajirusha tu kwenye sofa kuendelea kuangalia muvi,takataka za namna hii mimi nazipotozeaga hapohapo.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Wa hivyo unatakiwa uwaweke kando utawahitaji ukizidiwa maana hawatumii akili. Jana nilitoka na girl mmoja mpaka nikaona experience ya girl anayejielewa akakupenda na wazushi. Yani tofauti na dhamiri tunaziona ila sisi tunajitia ugumu wa kuchagua
 
Hii ndiyo raha ya JF.

Anauzwa alafu bei ya kutupa. Auzwe na viatu? Mpaka afike hapo hana tena viatu.

Yamebakia malapa ya uani. Ndiyo mkuu akimbie nazo.

apana mkuu jaman
Najua lazma atamuomba na kafigo kamoja akauze ndo umuache na hizo ndala et
 
Kuacha uwiz huyo kunaitaji kaz kubwa mno na sijui kama utaweza maana inaonekana kiasili kabsa n mwiz yan ndo asili yake kitu ipo damuni na hata ukifatilia kwao utaikuta hyo tabia
 
Visichana vya chuo hupenda wanaume wenye magari, pia ukumbuke kuvipatia pesa mara kwa mara utadumu nae.

Kwa taarifa yako hicho kisichana kilifukuzwa chuo kwa kosa la wizi. Ulizia vizuri.
 
Back
Top Bottom