Ndoa ya wanawake Wengi Ruksa Uganda

Ndoa ya wanawake Wengi Ruksa Uganda

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,588
Reaction score
10,120
🇺🇬Wanaume nchini Uganda sasa wanaweza kuoa wake wengi kisheria, Mahakama ya Katiba imeamua.

✍Uamuzi huo umekuja baada ya Chama cha Wanawake Wanasheria (WPI) kupinga mila hiyo ya wanaume kuoa zaidi ya mwanamke mmoja. Kundi hilo la watetezi lilisema kuwa mitala inadhalilisha, inadhuru, na inabagua wanawake.

✍Hata hivyo, mahakama haikupata ushahidi wa kutosha kuunga mkono kesi hiyo.

🇺🇬Uamuzi huo umezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya wanawake wa Uganda sasa wakitoa wito wa haki ya kuwa na wanaume wengi kama ambavyo wanawake wanaolewa wengi na mwanaume mmoja.
 
Labda wanawake wa Uganda rahisi kuwamudu

Hawa wa huku kuwamiliki kisheria zaidi ya mmoja yahitaji chembe hai ya kimanara na ki mwaka mwaka
 
Back
Top Bottom