Ndoa ya wake wengi

Ndoa ya wake wengi

Kwahiyo sisi tumeumbwa kuwa na wanaume wangapi? mbona mnajifikiria nyie peke yenu, huo ni ubinafsi. Achepuke tu ila siku nikijua ndo basi tena.

Nyie mmeumbwa kuwa na mmoja tu, Sasa si bora umruhusu aongeze mwingine tu, wewe unaongoja hadi ujue? Haya!, omba tu asikuletee ugonjwa, sisi wanaume hatutosheki na mmoja, labda uwe mgonjwa.
 
Sio kwamba ndio namruhusu, siwezi kumruhusi mtu wangu achepuke. Nikiona mtu simuelewi nitamueleza asiponielewa basi

''Basi'' kwa maana unamuachaaa au unaendelea nae hivyo hivyo akiwa na mchepuko?
 
Nyie mmeumbwa kuwa na mmoja tu, Sasa si bora umruhusu aongeze mwingine tu, wewe unaongoja hadi ujue? Haya!, omba tu asikuletee ugonjwa, sisi wanaume hatutosheki na mmoja, labda uwe mgonjwa.

wewe kama hutosheki na mmoja sio wote. Wapo wanaume wanatosheka na mmoja ingawa ni adimu ila wapo. Labda nikuulize, nisipotesheka na wewe mfano unaniruhusu nitafute mwigine au mimi ndo natakiwa nivumilie sio wewe
 
''Basi'' kwa maana unamuachaaa au unaendelea nae hivyo hivyo akiwa na mchepuko?

Akishakuwa namchepuko mimi wa nini huyo, ina maana ndio tabia yake hawezi kubadilika. Hata huyo mchepuko wake bado atakuwa anamcheat.
 
Mbona kuoa wake wengi hata kama wewe ni mkristo inawezekana kaka.
Cha kufanya kama unaweza kumconvice mtarajiwa wako pale katika cheti cha ndoa wanauliza type of marriage,so wewe mconvince ama mkomalie afu tieni Tick kwenye #polygamous ama kwenye #potentiallypoligamous .
Baadae utakua unaenjoy kila ukitaka kuongeza mke,koz mkataba wa ndoa utakua unaruhusu.

Chief kanisa gani hilo, ndoa ya kikristo huwezi kufunga nyingine mpaka ya kwanza iwe imeisha kwa sababu zozote na pia kuwe na talaka
 
Hi mtu unahitaji serikali ikuruhusu kuoa mke????? sidhani kama hili ni wazo bali ni hisia binafsi! Siamini pia kwamba hili ni moja ya matatizo wanayowaza wengi walioko kwenye ndoa!
 
Y on earth would you want a piece of paper to make it legal for you to exercise the male (in your perspective) polygamous nature?

We chukua wasichana waambie uko na wenzao kama watataka weka ndani ishi. That is a concrete decision! Serikali haitokuja kuwa toa hapo kama wamependa kuishi hivyo.

Do you remember in Kenya last year? there was a need for a piece of legal paper to show that a man doesn't require his wife's consent if he wants to add another wife
 
by nature mwanaume hatosheki na mwanamke mmoja huo ndio ukweli. Na wanawake wenyewe wanajua kua mziki wa kumridhisha mume sio mdogo na hiyo kazi hawaimudu ila wivu unawasumbua
 
wewe kama hutosheki na mmoja sio wote. Wapo wanaume wanatosheka na mmoja ingawa ni adimu ila wapo. Labda nikuulize, nisipotesheka na wewe mfano unaniruhusu nitafute mwigine au mimi ndo natakiwa nivumilie sio wewe

Kama mwanaume yupo kamili lazima utosheke tu, kama mgonjwa ni kweli unaweza usitosheke,. Lakini ''ke'' ana subira sana, na hana matamanio ya haraka kama ''me' ndivyo mlivyoumbwa otherwise uwe na pepo la ngono. Hivyo, chakufanya ni kujitahidi kumtibu mwenza wako ili arudi kwenye hali ya kawaida ili uridhike, kama itashindikana kabisa na wewe umeshindwa kuvumilia hali hiyo unaruhusiwa kwenda kuolewa kwingine ila sio uwe mchepuko.
 
Nyie mmeumbwa kuwa na mmoja tu, Sasa si bora umruhusu aongeze mwingine tu, wewe unaongoja hadi ujue? Haya!, omba tu asikuletee ugonjwa, sisi wanaume hatutosheki na mmoja, labda uwe mgonjwa.

Labda uwe mgonjwa! umenichekesha sana, mimi uchumi tu ndo hunisumbua bora nipate hata wa bei poa kwa mara moja irimradi nisiwe na mmoja roho inaridhika kwel, hivyo wakubali tu tuoe wengi ili tusichepuke
 
Akishakuwa namchepuko mimi wa nini huyo, ina maana ndio tabia yake hawezi kubadilika. Hata huyo mchepuko wake bado atakuwa anamcheat.

Sasa utawakimbia wanaume wangapi, wanaume wote walio kamili wako hivyo? si bora umruhusu aoe mwingine tu.?
 
sasa utawakimbia wanaume wangapi, wanaume wote walio kamili wako hivyo? si bora umruhusu aoe mwingine tu.?

Aoe ili iweje, kwani huyo anaetaka kumuoa ana nini ambacho mimi sina, na kama nina mapungufu anaiambie nijirekebishe
 
Kama mwanaume yupo kamili lazima utosheke tu, kama mgonjwa ni kweli unaweza usitosheke,. Lakini ''ke'' ana subira sana, na hana matamanio ya haraka kama ''me' ndivyo mlivyoumbwa otherwise uwe na pepo la ngono. Hivyo, chakufanya ni kujitahidi kumtibu mwenza wako ili arudi kwenye hali ya kawaida ili uridhike, kama itashindikana kabisa na wewe umeshindwa kuvumilia hali hiyo unaruhusiwa kwenda kuolewa kwingine ila sio uwe mchepuko.

Sio kweli kwamba wanaume wote wameumbwa hivyo maana kuna wengine hawako hivyo. Yaan hiyo ni tabia kama tabia zingine anazoendekeza mtu bila sababu za msingi. Eti kwakuwa ni mwanaume ni sawa ila kwa mwanamke ni pepo la ngono hahaaaa
 
hata hao waislam nao, utakuta mtu ana wake wawili au watatu na bado ana michepuko.
 
Chief kanisa gani hilo, ndoa ya kikristo huwezi kufunga nyingine mpaka ya kwanza iwe imeisha kwa sababu zozote na pia kuwe na talaka

Hapo ninaongea kisheria zaidi.
Umeshawahibona cheti cha ndoa??
Kama umewahi angalia lazma wameandika type of Marriage.
Kama ni Monogamous watatia Tick,kama ni Polygamous wanatia tick,kama ni Potentialy Polygamous wanatia tick pia.
Angalia afu uje uniambie hapa.
Kisheria inawezekana bila tatizo,kidini ndio shida.
 
Aoe ili iweje, kwani huyo anaetaka kumuoa ana nini ambacho mimi sina, na kama nina mapungufu anaiambie nijirekebishe

Ha, ha, ha! sio hivyo, yaani hata uwe mzuri vipi, hilo suala lipo by nature, mumeo lazima tu atahitaji kuwa na mtu mwingine wa ziada ingawa anaweza asikwambie, ndivyo tulivyo wanaume. Hujawahi kukuta mwanaume ana mke mrembo lakini bado ana sumbuliwa na mtu mwingine tena sio mzuri kama mke wake?.
 
Mzinzi mini? Badili dini kama shida yako ni kua na mke zaidi ya mmoja. Sasa unataka kutu shawishi nasisi tusio kua na haja hiyo. Badili oa 40 huta ulizwa.
 
Back
Top Bottom