Ndoa ya CCM-CUF Visiwani: Ishara ya CUF kuwa 'CCM-B' huku Bara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa ya CCM-CUF Visiwani: Ishara ya CUF kuwa 'CCM-B' huku Bara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 31, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tangu hatua za kwanza za kutaka maridhiano kati ya CCM na CUF kule Visiwani zilipoanza nimekuwa najiuliza: Jee maridhiano haya yakizaa srikali ya umoja wa kitaifa kule Visiwani uhusiano wa vyama hivyo viwili huku Tanzania Bara utakuwaje? Utaendelea kuwa na ushindani wa jino kwa jino kama ilivyokuwa hapo zamani au huku Bara CUF nayo itabidi ipunguze makali yake dhidi ya chama tawala na hivyo kujipa label ya u-CCM B?

  Mimi naona hili ni jambo la msingi kulitafakari kwani huo u-CCM B ninaousema unaanza kujitokeza hasa ukizichunguza kauli za Katibu Mkuu wa CCM – Yusuf Makamba hivi majuzi – akiisifia CUF na kukiponda Chadema.
  Wasiwasi wangu ni kwamba CCM wanaweza kuwatumia viongozi wa CUF katika kudhoofisha kampeni za Chadema hasa zile zitakazolenga kuwapo kwa ufisadi uliokithiri katika serikali ya CCM.

  Na hili siyo la kuhisi kwani tulishaona huko nyuma jinsi Prof Lipumba alivyokuwa akitoa kauli za kutetea masuala ya ufisadi kama vile kuungana na akina Mkuchika na Sofia Simba kuzipinga kauli la Mengi pale alipowataja mafisadi papa (ambao wengine tayari wako mahakamani wakijibu kesi za ufisadi), na hali kadhalika kuuunga mkono wazo kwamba serikali inunue mitambo ya Dowans iliyoingizwa nchini kutokana na kashfa ya Richmond.

  Swali langu ni jee – huku Bara CUF itakubali kupiga ‘zumari namba 2’ (second fiddler) kwa niaba ya CCM?
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kafu kwisha,kama kule jikoni kumekwisha itakuwa huku matawini? kafu iko zanzibar bro,huku ng`ambo ni bendera fuata upepo.:A S shade:
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Zak: Ni suala gumu kulitafakari na kupata jibu lililo sahihi -- ingawa kila dalili zaonyesha kuwa huku bara uhasama kati ya CCM na CUF utapungua sana na ninathubutu kusema kwamba CCM sasa itaiona CUF siyo tishio tena kama zamani. Hali hii inasikitisha sana kwa huku Bara ambako mara mbili 2000 na 2005 CUF ilikuwa nambari 2 kwa kuzoa kura za urais huku bara. Ushindani ulikuwa mkubwa hasa 2005 pale hadi CUF waliposusia kutangazwa na NEC matokeo ya kura ya urais (Chadema walihudhuria) Diamond Jubilee Hall. Sidhani iwapo hali ya ushindani wa namna hii baina ya vyama hivi viwili itatokea tena.

  Jinsi CCM ilivyoi-neutralise CUF kule Visiwani kutaathiri sana harakati za chama hicho huku Bara! Tena sana.
   
 4. eddiy

  eddiy Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Yamani hebu tujiulize CUF ina kiti gani cha Ubunge Bara.Wazanzibari wao wamekiunga mkono kwa hali na mali hata kupoteza maisha yao kwa CUF sasa tujiulize Bara tuna nini na wakaazi wa Bara wanafikiria nini JE? tunahitaji UKOMBOZI kama Wazanzibar au tuendelee hali halisi ? naamini CUF itaendelea kuwa tishio kwa CCM Bara.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,325
  Trophy Points: 280
  Zak huu ni ukweli mchungu kuukubali lakini ndio hali halisi. Ili kudhoofisha nguvu ya Dr. Slaa, CCM itaitumia CUF kuibomoa Chadema kwa kifanya CUF ni mshirika na the common enemy sasa atakuwa Chadema.

  Kwa kuanzia, CUF itagomea ushirikiano wa aina yoyote na Chadema. Hii ndio mbinu kuu iliotumiwa siku zote, wagawe uwatawale. CCM inahakikisha inazigawanya kura za upinzani na benefishary ni yeye, kama vilivyo vita vya panzi.

  Nawashauri Chadema, hata kama CUF itawagomea ushirikiano wa aina yoyote, Chadema isisimamishe mtu urais wa Zanzibar, ama kwenye CUF strong hold.

  Mpaka sasa, suala la mgombea mwenza wa Chadema, bado ni pasua kichwa.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,325
  Trophy Points: 280
  Zak huu ni ukweli mchungu kuukubali lakini ndio hali halisi. Ili kudhoofisha nguvu ya Dr. Slaa, CCM itaitumia CUF kuibomoa Chadema kwa kifanya CUF ni mshirika na the common enemy sasa atakuwa Chadema.

  Kwa kuanzia, CUF itagomea ushirikiano wa aina yoyote na Chadema. Hii ndio mbinu kuu iliotumiwa siku zote, wagawe uwatawale. CCM inahakikisha inazigawanya kura za upinzani na benefishary ni yeye, kama vilivyo vita vya panzi.

  Nawashauri Chadema, hata kama CUF itawagomea ushirikiano wa aina yoyote, Chadema isisimamishe mtu urais wa Zanzibar, ama kwenye CUF strong hold.

  Mpaka sasa, suala la mgombea mwenza wa Chadema, bado ni pasua kichwa.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  CCM wana hesabu sana, wamejua hawawezi kuiba kura election after election, wamekuja na insurance policy, wakishindwa uchaguzi na kuiba kura angalau wanakuwa katika serikali ya mseto.

  CUF walikuwa katika a tough situation, wakikataa mseto wanaweza kushindwa uchaguzi, au hata kushinda halafu kugeuziwa mchezo kama chaguzi zilizopita.

  Wakikubali mseto maana yake hata wakishinda hawawezi kupata uongozi wa peke yao.

  At the end of the day idea ya mseto ina make sense, kwa sababu ukiwa na situation ya 49% against 51% kuwa na a winner takes all ni kualika migogoro mitupu. Ila naona kama CUF wamekuwa shortchanged kwa sababu hii kitu ilitakiwa iwepo tangu day one ili kuwa fair.

  But hey, who said the world was a fair place.
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  hata mimi siamini kilichotokea kwa kafu kulainika hivi. Wanakafu ndio wajuao nini kinaendelea.:A S shade::A S shade:
   
 9. C

  Chuma JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine huwa nikisoma baadhi ya post huwa nacheka tu...Maana wakati ule CUF ilipokuwa kweli Jino kwa Jino...baadhi ya watu wakabrand chama cha Vurugu....!!!

  Sasa aproach imebadilika, kinaonekana CCM-B....i like it...!!!

  Pasco... suala la Muungano wa CUF na Chadema halipo. kama sehem CUF hawana mgombea watawaunga Mkono chadema, the same Chadema kama hawana Mgombea sehem watawaunga mkono CUF....!!!...

  ..CCM hawana muda kuwatumia CUF wala muda kuwatumia Chadema...kwao wao mpinzani ni mpinzani...!! hizi assumption za Wapambe ni zao wao wenyewe kujitengenezea Taswira ya paka wakati hayupo.

  By the way CUF ni wazoefu na wana uvumilivu ktk SIASA.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye red: Lakini CCM wakibanwa sana katika uchaguzi na hasa wakiona chama kimoja ni tishio kubwa kwake huamua kutumia vyama vingine vidogovidogo -- angalau katika kutoa vocal support. Hii imefanyika sana huko nyuma, kwani tumeona viongozi wa baadhi ya vyama hivyo wakitoa kauli za kuwaponada viongozi wa chama tishio kwa CCM. haiwezekani CCM haina mkono hapo.

  Kuhusu uzoefu wa uvumilivu wa CUF -- hujasema kama hii ni kitu negative au positive kwa CCM (au hata kwa CUF yenyewe). Lakini bila shaka ni positive kwa CCM kwani ukichukulia kule Visiwani, viongozi wa CCM wamekuwa wakila nchi kwa miaka 15 sasa, bila ya uhalali wowote (wakiwa wanapora ushindi) huku CUF wakifanya uvumilivu. Bahati hawakuamua kuingia msituni!
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  hili liko wazi kwani hata sasa cuf wamekua upande wa ccm zaidi ktk mambo mengi, nadhan financial support ndio driving factor ktk hilo!
   
Loading...