Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Mtu hunena yaujazao moyo wake, na kwa ulimi hutukana na kusifu, na hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea na pia mtu hujaribiwa kulingana na imani yake, sasa hadi unawaza kufa utapewa hitaji lako kwa kuwa umekata tamaa mpaka una hamu ya kufa subiri urajibiwa soon. Ila moja tu ndoa hata kama ya kikristo sio kifungo cha maisha unajua kuna watu badala ya kufunga ndoa wanafunga pingu za maisha sasa angalia jela yako ni ipi ubadilike.
 
We ulioa sura. Mmekutana 2013 na ndoa mwaka huo huo ? Pole lkn.

Mkiwekwa kwenye uchumba miaka mitatu mnalalamika kuwa wanaume wanachukua degree kwenu...cjui hata tuwafanyie nini nyie viumbe.
 
Kaka kwa uzoefu wangu naomba nijibu yafuatayo; wewe unaumri gani na yeye anaumri gani? Je familia anayotoka ikoje kimaisha na uwezo kiuchumi upoje? Yeye ni wangapi kuzaliwa ktk watoto wangpi?
 
Ukinijibu kiufasaha hayo nilio kuuliza nadhani kiini cha tatizo lako kinaweza kua hapo.
 
Ndugu yangu unayoyangumza darasani ni 100% lakini field ni tofauti mno na uhalisia. Si kila chui hurarua, si kila nyoka huuma kwa kung'ata, si kila mwizi huiba kwa bunduki. Sikia kwa wengine tu hii theory yako mpaka ungeisahau.

kama unajua kiasi hiki basi huna haja ya kutafuta ushauri mtandaoni.
 
Mkiwekwa kwenye uchumba miaka mitatu mnalalamika kuwa wanaume wanachukua degree kwenu...cjui hata tuwafanyie nini nyie viumbe.

Dont bee too fast or too slow... huyu kawa super fast inakula kwake, miaka mitatu uchumba nako kuzeeshana tu thats slow .. Not too slow but slow��������
 
Mkuu Pole,

Ningekuwa na simu ya dr.slaa angekushauri jambo lenye hekima na uzoefu. sidhani kila samaki aliyedondoka kwenye tenga ni muovu.

Nangu Mahwelu
 
Roho zifuatazo zinashughulika na kuvuruga ndoa:
1.Jina mahaba ( spiritual wife/ husband)

2. Jezebel
Jaribu ku google hizi roho na utapata maelekezo jinsi ya kupambana nazo; ushindi ni lazima maana yuko ambaye alishatushindia pale msalabani.
 
Mke wangu alikuwa kama wako, ila tulisha achana long time, siku ya ndoa tulikuwa tunagombana pale high table huwezi amini, yani ilikuwa shida, alikua mlevi sana, nikimshauri aache tunagombana ilifikia mahali nikawa sina hata marafiki kwa kifupi niliishiwa confidence. Huyu mwanamke alifikia hatua ya kuchana cheti cha ndoa mbele ya mama yangu mzazi.

Ilikuwa hivi, alirudi nyumbani akiwa amelewa, wakati huo mama yangu alikuwa amekuja kututembelea niliwahi kumshauri kuwa walau kwa kipindi ambacho mama yupo afanya unafiki walau kidogo, hakunielewa, basi siku hiyo kaja na mipombe yake nikamchapa kibao kimoja tu cha haja akaenda chini, alipoinuka akaingia chumbani akatoka na cheti akakichana mbele ya mama.

Nashukuru Mungu baadaye alinipa mwanamke simple na ambaye amekuwa na mchango mkubwa sana katika ustawi wa familia yangu.

Cha ajabu alipogundua nimependwa tena akaanza ku mind, kila mara kumsumbua mke wangu, shenzi kabisa yule demu, naye ni Mnyakyusa (sorry to mention this)
 
Nastahili pumziko la milele! Ee Mungu nisaidie!

Pole mkuu, sina mengi yakusema, ila dawa moja wapo ya kujua maamuzi gani yatakua mazuri fanya utakavyoweza aweze jua umeomba ushauri humu Jf na asome haya uliyoandika yote, kama kweli anao upendo kwako yatambadilisha kabisa, na kama ni mapenzi yamemwisha utamjua na utaweza chukua hatua stahiki
 
Tatizo lilikuwa upande wako na bado liko upande wako...nina hakika haukumshirikisha MUNGU katika kutafuta huyo mke na badala yake ukaongozwa na tamaa ya mwili na shetan akachukua nafasi yake akakutafutia maumivu...wewe unajua kabisa maandiko yanasema nini kuhusu mwanamke aliyeachika,je ulijiridhisha kuwa aliachika kwa sababu hiyo akiyokuambia??yaan uliamua kesi kwa kusikiliza upande mmoja,..upande ambao kamwe huwez pata ukwel wa mambo,hakuna mwanamke anayetaka mahusiano mapya atakuambia ukwel kwa nini aliachika,atakueleza maneno kuwa yeye ndo aliyeonewa...wote wanaokuja hapa jukwaan wanatoa shutuma kuwa wanaonewa ila ukwel wa mambo ni kinyume chake,ni mabingwa wakuchezea hisia za wanaume wanaowapenda,wakija pigwa chini ndo wanapata akili kuwa wamepoteza bahati,..
Sasa chakufanya ni wewe kulia na MUNGU wako nakutubu kabisa kwa dhati kwa DHAMBI yakuoa mke wa mtu(huyo alikuwa mke wa mtu na bado ni mke wa mtu),kisha muombe MUNGU akupr furaha ya maisha,..atakujibu atavyoona yafaa,kwanza tubu
 
uyo mwanaume aliyezaanae lazma anatembea naye bado.
miez yote iyo hamjafanya tendo landoa na haulizi? amekuona boya na huwez fanya kitu.

ni kwel we unapigana vita vya kiroho lakin pia jiongeze kwa elim ya kidunia. mkeo angekua ameitaj hak yake ya ndoa ila yupo kimya kuna usaliti apo.

pole sana
 
Pole sana kaka, ila nakutia moto kuwa utashinda! Tambua kuwa vita vyetu si juu ya mwili..ni juu ya calme za nguvu za giza..mkeo kimsingi yupo posessed na mapepo..hivi usidhani anakuelewa maana anayemtawala kwa Sasa sio mungu anayekutawala...ni shetani ndio mtawala ktk moto Wake..hana control na maamuzi yake Tena..ni sawa na mtu mwendawazimu..anaokota makopo si kwa mapenzi yake..mapepo ndio yanamushurutisha na Kama neno linavyosema shetani anakuja kuharibu, kunyanganya na kuuwa..ila kristo kaka kujenga! Nakushauri kwa Sasa endelea kumwomba mungu akujanze nguvu ya kushinda majaribu ya michepuka..kujiua na kukata tammaa..na pia akujaze roho ya upendo kwa mkeo..umwone yule uliyempenda siku ya kwanza na pia umwone nae ni mwana wa mungu mwenye nia ya kuishi maisha ya amani..upendo..kumcha mungu nk.ukitambua hilo..hutachoka kumwombea..kumbuka mungu hachelewi wala awahi...na kila jaribu tulipitialo linaenda sawa na uwezo wako wa imani! Nakukumbusha kuwa si wewe tu unaepitia magumu..miaka miwili iliyopita mtumishi mkubwa na mashuhuri..Benny Hinni aliachana na mkewe kipenzi aliemuoa akiwa bikira ..suzan kwa zaidi ya mwaka..lakini wakati wa mungu kujibu maombi ulipofika..watumishi hawa walirudiana mbele ya macho ya wanadunia bila aibu..kumbuka kwa kuwa ni mtumishi wa mungu kashfa ilisambaa duniani..but God is always faithful..kwa watu Wake..akaiponya ndoa na Sasa wameridiana. Kwa hiyo si mkeo tu mwenye shida ya kuwapossessed na mapepo ..sasa endelea kuomba huku ukimkumbusha mungu ahadi zake..Kumbukumbu la torati 28..amekuahidi mambo mengi iwapo utaendelea kumtii! Na kumbuka kujiua ni dhambi..na kifo chako kitakuwa Kama mpagani...na utakuwa umempa ushindi shetani wa bure!!!
JIPE Moyo utashinda!
 
Tatizo ndoa za siku hizi watu mnaingia kichwa kichwa kwa kigezo tukishapendana inatosha, nani kakuambia. Alafu inaonekama kama hiyo ndoa wewe ndiyo uliilazimisha vile.
 
Wala usikate tamaa,issue yako ni ndogo sana kwa kuwa inahusu psychology,cha kufanya mpeleke mkeo caunseling
 
Mkuu umeowa mtu ambae hakuwa tayari kuolewa na kwake alikubali mahusiano ili apate relief (rebound relationship) moyoni ,then wewe ukakimbilia ndoa. But now ndo karudi kwenye hali ya kawaida na sahv atakuwa anajuta kuingia kwenye ndoa akiwa hayupo sawa kiakili ndio maana haoni hta raha wala amani na umuhimu wa ndoa yake.
 
Wakati mwingine kujieleza mwenyewe upande mmoja bila upande mwingine kuwepo huwa kama kuna mambo yanafichwa na upande unaojeleza. Nimejitahidi sana niandike bila hasira yoyote.Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa mtu mwenye hisia kali sana zàkutengeneza picha ya familia yangu kuanzia mke mpaka watoto.

Kikubwa kilichokuwa kikijirudia ni picha ya familia yenye furaha sana. Hali hii ilijengea moyo wa upole na upendo sana ambao nimekua nao mpaka sasa.Mwaka 2013 nilifanikiwa kuoa mwanamke wa kinyakyusa aliekulia Dar, mmi nikiwa Mnyamwezi wa Ziba, Nzega Tabora. Wakati namuoa mke wangu alikuwa na mtoto mmoja.

Kwa maelezo yake ni mtoto aliezaa alipokuwa ameolewa huko Dar, ila ndoa ilivunjika baada ya mume kuoà ke mwingne na kumnyanyasa sana mke wangu huyu.Tulifahamiana Dar katia mishemishe ya maisha akiwa mwajiriwa wa shirika fulani. Kwakweli kwa uzuri wa binti huyu na vileàlivyoonekana mpole sikujishauri sana kuingia naye kwenye mahusiano hatimaye tukafunga ndoa.

Maisha yakaendelea na hali ilianza kubadilika àlionekàna kama mtu mwenyejupe na jeusi. Namaanisha anaweza kuamka amenuna bila sababu. Lakini pamoja na haya yote upendo wake kwangu ulionekana waziwazi mpaka kwa wazazi wake. Mwazoni mwa mwaka 2014 aliifungua mtoto wakike.

Tuliendelea na maisha ya ndoakwa hali hiyo hiyo.Ulifika wakati nikajaribu kuzungumza naye juu ya hali hiyo nakutaka kujua kulikoni anakuwa hivyo alisema kwa mateso alopata kwa mume wa kwanza yalimfanya kuwà na moyo katili. Nilimuanzishia huduma ya maombezi na kumpeleka kwa wachungaji walimwombea na hatimaye mapepo yalitoka. Kwa kiasi fulani alibadilika na kuwa mtu mzuri.

Pamoja na hali hiyo ya mabadiliko hali ya kununa iliendelea kuwepo na mbaya zaidi ukiuliza tatizo ninini anakuàmbia kawaida tu. Au mimi nina makosa? Anakuambia hamna.Wadau, nimejitahidi sana kumsaidia kwa kila jambo abadilke lakini hakuna mafanikio mpaka mudà naandika amekuwa na tabia za ajabu sana.

1. Hawezi kutii sauti ya mume kwa jambo lolote jema au baya. Unaweza kutoka naye out ukajidai kumçare wala hawezikusuuport hata. Unawezakmshauri asifanye jambo fulani vile linahatarish maisha yake wala hatakuelewa.

2. Kununa ni jambola kawaida kwake, hata siku3 amenuna tu bila sababu.

3. Hana muda wa kuchochea amani na upendo wenye ndoa, muda wote ni kutafuta namna ya kuingusha ndoa tu.

Kwakweli najisikia vibaya sana katika maisha yangu. Nilitamani sana kutimiza zile hisia za familiayangu yenye furaha na amani lakini imekuwa kinyume.Najisikia sina nafasi yoyote kwenye fàmilia kwa vile hawezi kunisikiliza na kukubaliana hoja zangu. Yàani kila jema unàlomfanyia yeye àtatakaufanya kinyume tu ilimradi mkorofishane.

Umefika wakati sasa hata hamu ya tendo landoa imekwisha kabisa, siwezi kusisimka kufanya naye chochote japo ni mzuri sana tu. Mfano mpaka sasa nina miezi 9 tangu nishiriki naye. Mimi ni mtumishi mkubwa tu kanisani kwetu nameshimu sana Mungu. Kwa muda wote huu sifanyi ngono, unafikawakati mwili unawaka tamaa mno lakini Mungu hunijalia uimara tena.

Nimemuombea sana huyu mwanamke lakinihakuna matund yoyote sasa. Nahisi hii hali ya kukosa hamu ya kushiriki nayehuenda ikaniathiri zaidkwani hata kwa wanawake wengi saasa naiona hàli hii.Wadau nimevumilia sana, nimepata vyote vizuri kwenye ndoa yangu lakinihiki kimoja amani na furaha nimevikosa. Naona bora nisingevipata vyote hivi ila nikakipata hicho kimoja.

Bora ningeoa maskni ambaye ningefurahinaye. Siwezi kutoka nje ya ndoa wala kuwa namçhepuko kwa vile imani yangu kwa Mungu ni imara. Lakini pia nahisi nawachukia sana wanawake sasa.Naona kama wote wànaweza kunifanyia hivihivi.Inaniuma sana bora Mungu aitwae roho yangu nikapumzike.

Maana mateso haya nimakali mno. Naandika nikiwa nabubujikwa na machozi mengi sana, je Mungu alinijalia upole na upendo ili niteseke namna hii? Naumia sana. Sijajua msaada mzuri zaidini upi, nimeamua kueleza jaambo langu hili la sirini kwenu huenda akapatikana hata mmoja akanipa ushauri.Mara nyingi nimekuwanikipost humu mambo ya utani lakiini leo nakuja kwenuna uchungu sana neno lako kwangu ni faraja tosha maishani mwangu.

Asante kwa ushauri wako

Kama hachepuki hiyo haina shida. Kila mwanamke mzuri ana kasoro zake. Ukipenda boga penda na ua lake. Huyo mkeo hapendi wanaume kwa ujumla mvumilie tu.
 
Mwenyezi Mungu mwenye huruma na upendo akutie nguvu na pia kaisome zaburi 71 ikutie nguvu na moyo ndugu yangu, kwakua uko na imani kwa Kristo,basi we vumilia ti kwani hakuna lolote lisilo na mwisho kaka yangu, kwa muda uliovumilia usikate tamaa wala usife moyo si muda mrefu hayo yatakua kama ya kale,ndugu uonapo giza limekuwa kubwa sana ujue kunakaribia kukucha ndio ushauri wangu kwako, Mungu akutangulie.
 
Mwenyezi Mungu mwenye huruma na upendo akutie nguvu na pia kaisome zaburi 71 ikutie nguvu na moyo ndugu yangu, kwakua uko na imani kwa Kristo,basi we vumilia ti kwani hakuna lolote lisilo na mwisho kaka yangu, kwa muda uliovumilia usikate tamaa wala usife moyo si muda mrefu hayo yatakua kama ya kale,ndugu uonapo giza limekuwa kubwa sana ujue kunakaribia kukucha ndio ushauri wangu kwako, Mungu akutangulie.

Mkuu umemaliza kazi kabisa kama hataelewa na hekima hii basi yeye ndo atakuwa na tatizo. Imeandikwa tuishinao kwa akili sana. Mimi leo nimemsamehe wa kwangu alikwenda kuzulula watu wakavunja mlango na hata kutoa ripoti polisi hakujishughulisha kwenda.
 
Back
Top Bottom