Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ndoa: Nimevipata vyote isipokuwa hiki tu

Ushauri mzuri sana umepata. ...wanawake wanataka strong man sio mtu wa kubembeleza sana..sometimes unakuwa mbogo.

Hako katabia ka upole ndio kanam boa kama ulikuwa hujui.

Fuatilia utagundua hamna furaha kwa sababu hamna adventures. ...hata mziki mzuri ukirudiwa rudiwa una boa.

Sasa kuwa bad boy kidogo uone mambo yatabadilika
 
Pia usiwe unaoongea fact sana wanawake wanapenda porojo porojo sana...kama ulikuwa hujui sasa jitahidi kujua porojo za mjini...wanaita ubuyu
 
Mkuu ushauri uliopata humu ni wa kutosha kabisa. Chagua linalokufaa na yasiyokufaa yaache. Mm la kwangu ni moja tu, je ulimshirikisha MUNGU kabla ya kuoa au uzuri wake ndio ulikupumbaza hata ukasahau kumshirikisha MUNGU. Kuna madhara makubwa sana ya kuoa mke kwa sura yake pasina kumshirikisha MUNGU. Ikiwa hukufanya hivyo basi fanya yafuatayo;
1. Tubu kwaajili ya kutompa nafasi MUNGU katika kuchagua mchumba. Kisha muombe airidhie ndoa yako
2. Pambana na roho wa uovu katika roho na kweli.
Nakusihi usikate tamaa kwakuwa huo ni mtihani kwako na ukishinda Mwenyezi MUNGU atakuondoa hapo ulipo na kukupeleka katika daraja ya juu zaid. Kila la kheri ktk safari ya kupandishwa daraja.
 
Mengi yamesemwa.
Langu ni hili, nachokiona ktk maelezo yako ni vita ya kiroho inayoikabili ndoa yako ili kuisambalatisha na mlango wa mashambulizi ni mke wako.
Unachokipitia ni kitu kinachokabili ndoa nyingi za wapendwa.

Fanya haya yatakusaidia.
1: funga siku tatu kavu ili kuhitaji maelekezo ya mungu juu ya kutambua msingi wa tatizo na mbinu ya kuvunja misingi hiyo.
2: ondoa attention kwa mke wako na matatizo yake ,now mpe Roho mtakatifu nafasi ktk fellowship kamili, ikikubidi kuchukua likizo ya muda ili ku deal na changamoto hiyo.
Usikate tamaa mtumishi Bwana ana haja nawe tena kubwa tu kuliko kulilia furaha na amani unazoziubiri,
Amani na furaha ya kweli vimefungwa ktk kusudi alilokuitia Bwana ,hivyo usikatishwe tamaa na mtu aliye mpa shetani nafasi.


Anza na hayo usiache kutupa mrejesho.
Wapendwa wenzako tutakuombea Mungu akutoe hapo.

Amina......
 
Changamoto za ndoa ni balaa ndiyo maana watu wengi ni Malaya. Nafuu unamjua Mungu wewe
 
Nik
Wakati mwingine kujieleza mwenyewe upande mmoja bila upande mwingine kuwepo huwa kama kuna mambo yanafichwa na upande unaojeleza. Nimejitahidi sana niandike bila hasira yoyote.Nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa mtu mwenye hisia kali sana zàkutengeneza picha ya familia yangu kuanzia mke mpaka watoto.

Kikubwa kilichokuwa kikijirudia ni picha ya familia yenye furaha sana. Hali hii ilijengea moyo wa upole na upendo sana ambao nimekua nao mpaka sasa.Mwaka 2013 nilifanikiwa kuoa mwanamke wa kinyakyusa aliekulia Dar, mmi nikiwa Mnyamwezi wa Ziba, Nzega Tabora. Wakati namuoa mke wangu alikuwa na mtoto mmoja.

Kwa maelezo yake ni mtoto aliezaa alipokuwa ameolewa huko Dar, ila ndoa ilivunjika baada ya mume kuoà ke mwingne na kumnyanyasa sana mke wangu huyu.Tulifahamiana Dar katia mishemishe ya maisha akiwa mwajiriwa wa shirika fulani. Kwakweli kwa uzuri wa binti huyu na vileàlivyoonekana mpole sikujishauri sana kuingia naye kwenye mahusiano hatimaye tukafunga ndoa.

Maisha yakaendelea na hali ilianza kubadilika àlionekàna kama mtu mwenyejupe na jeusi. Namaanisha anaweza kuamka amenuna bila sababu. Lakini pamoja na haya yote upendo wake kwangu ulionekana waziwazi mpaka kwa wazazi wake. Mwazoni mwa mwaka 2014 aliifungua mtoto wakike.

Tuliendelea na maisha ya ndoakwa hali hiyo hiyo.Ulifika wakati nikajaribu kuzungumza naye juu ya hali hiyo nakutaka kujua kulikoni anakuwa hivyo alisema kwa mateso alopata kwa mume wa kwanza yalimfanya kuwà na moyo katili. Nilimuanzishia huduma ya maombezi na kumpeleka kwa wachungaji walimwombea na hatimaye mapepo yalitoka. Kwa kiasi fulani alibadilika na kuwa mtu mzuri.

Pamoja na hali hiyo ya mabadiliko hali ya kununa iliendelea kuwepo na mbaya zaidi ukiuliza tatizo ninini anakuàmbia kawaida tu. Au mimi nina makosa? Anakuambia hamna.Wadau, nimejitahidi sana kumsaidia kwa kila jambo abadilke lakini hakuna mafanikio mpaka mudà naandika amekuwa na tabia za ajabu sana.

1. Hawezi kutii sauti ya mume kwa jambo lolote jema au baya. Unaweza kutoka naye out ukajidai kumçare wala hawezikusuuport hata. Unawezakmshauri asifanye jambo fulani vile linahatarish maisha yake wala hatakuelewa.

2. Kununa ni jambola kawaida kwake, hata siku3 amenuna tu bila sababu.

3. Hana muda wa kuchochea amani na upendo wenye ndoa, muda wote ni kutafuta namna ya kuingusha ndoa tu.

Kwakweli najisikia vibaya sana katika maisha yangu. Nilitamani sana kutimiza zile hisia za familiayangu yenye furaha na amani lakini imekuwa kinyume.Najisikia sina nafasi yoyote kwenye fàmilia kwa vile hawezi kunisikiliza na kukubaliana hoja zangu. Yàani kila jema unàlomfanyia yeye àtatakaufanya kinyume tu ilimradi mkorofishane.

Umefika wakati sasa hata hamu ya tendo landoa imekwisha kabisa, siwezi kusisimka kufanya naye chochote japo ni mzuri sana tu. Mfano mpaka sasa nina miezi 9 tangu nishiriki naye. Mimi ni mtumishi mkubwa tu kanisani kwetu nameshimu sana Mungu. Kwa muda wote huu sifanyi ngono, unafikawakati mwili unawaka tamaa mno lakini Mungu hunijalia uimara tena.

Nimemuombea sana huyu mwanamke lakinihakuna matund yoyote sasa. Nahisi hii hali ya kukosa hamu ya kushiriki nayehuenda ikaniathiri zaidkwani hata kwa wanawake wengi saasa naiona hàli hii.Wadau nimevumilia sana, nimepata vyote vizuri kwenye ndoa yangu lakinihiki kimoja amani na furaha nimevikosa. Naona bora nisingevipata vyote hivi ila nikakipata hicho kimoja.

Bora ningeoa maskni ambaye ningefurahinaye. Siwezi kutoka nje ya ndoa wala kuwa namçhepuko kwa vile imani yangu kwa Mungu ni imara. Lakini pia nahisi nawachukia sana wanawake sasa.Naona kama wote wànaweza kunifanyia hivihivi.Inaniuma sana bora Mungu aitwae roho yangu nikapumzike.

Maana mateso haya nimakali mno. Naandika nikiwa nabubujikwa na machozi mengi sana, je Mungu alinijalia upole na upendo ili niteseke namna hii? Naumia sana. Sijajua msaada mzuri zaidini upi, nimeamua kueleza jaambo langu hili la sirini kwenu huenda akapatikana hata mmoja akanipa ushauri.Mara nyingi nimekuwanikipost humu mambo ya utani lakiini leo nakuja kwenuna uchungu sana neno lako kwangu ni faraja tosha maishani mwangu.

Asante kwa ushauri wako
Ngoja nikwambie kitu mtumishi...waisraeli walipita jangwani na kutembea kwa miaka 40,Ila waliofanikiwa kufika caanan kwa kizazi hicho ni wawili tu,sasa elewa kwamba jangwa lako wewe ni ndoa yako mwenyewe,Mungu anajua ni kwa mini alikuruhusu umuoe huyo,Jivunie Sana kumuoa kwa sababu kwa sababu hiyo tu,Tambua ya kuwa wewe Una Misuli ya Imani na kwa Sababu hiyo Mungu anakuamini kuwa hakika utaifikia nchi ya maziwa na asali....Then Omba bila Kuchoka,Mungu atajibu kwa wakati wake..time heals everything...BARIKIWA
 
Wanasema ukiona unafanya jambo lile lile na unapata matokeo yale yale
basi jaribu kufanya kinyume chake

Kuna aina ya watu 'ukiwadekeza tu umewaharibu'
watazidi kukuletea utoto hadi ushangae

dawa yake ni wewe ku sit back and do nothing..

akinuna usimuulize kitu...shika remote control and ignore her...
Sorry Boss though it seems like am now bothering u, i just want to get updated with the NICOL issue. What do stakeholders say
 
Mleta mada ndugu yangu pole sana..mimi ningependa kukupa moyo sana Mungu ni mwema sana na anakupenda..na pia kuna watu kibao wanakupenda usifikirie kutwaliwa Mungu ana makususudi na wewe mm napitia kipindi kigumu sana tena bora ww ni mtumishi wa mungu atakufanyia njia ...binafsi nilikuwa na kazi nzuri nikamshirikisha kwa kila pato basi ndio kwanza kaoa mke wa pili ni story ndefu lkn maisha yanaendelea tu..jipe moyo utashinda japo inachukua muda kuzoea na huenda ana mtu...nahic anajilazimisha kukupenda
 
@Majaribu2013 Pole sana hakika Mungu atakusaidia kutua huu mzigo.

Kama unamjua Mungu, nadhani huu ni wakati wako wa kukaa tu na kutulia na Mungu.

Neno la Mungu linasema ni kitu gani kitanitenga na upendo wa Mungu, je ni dhiki, je ni njaa, je ni uchi je ni chochote ambacho unakijua wewe....
Ni wakati wako wa kujipima uone je haya uliyonayo yanatokana na nini. Unaweza ukahisi ni tatizo la shemeji kumbe yuko hivyo ili imani yako ipimwe. Fikiria mara mbili kabla haujakata tamaa.

Kwa mtumishi kama wewe, ukiona umeomba kila kitu hakisogei, mshukuru tu Mungu kwasababu imempendeza iwe hivyo. Pia mshukuru Mungu kwa kujibu ila wakati waje haujafika.

Yesu akutie nguvu ila nakusihibusikate tamaa ndugu maana ni dhambi.
 
Sorry Boss though it seems like am now bothering u, i just want to get updated with the NICOL issue. What do stakeholders say
Mkuu pole sio kwamba nilidharau hapana
mimi nasubiri mkuu @PARADIGM aje atupe feedback
tulikubaliana ataenda kujua nini kifanyike atuletee infos hapa
 
"Wakati mwingine kujieleza mwenyewe upande mmoja bila upande mwingine kuwepo huwa kama kuna mambo yanafichwa na upande unaojeleza"

Kwenye hiyo mistari hapo juu mie ndio naona umenena sawa...upande mwingine hauko hapa kujieleza...kwa hiyo hatujui kama kuna yaliyojificha kwenye maelezo yako. Unasema Mungu amekujalia upendo na upole, hili hatuwezi kuthibitisha hapa...
Mimi siwezi kukushauri kwani sina hakika huo upande wa pili nao unajitetea vipi.
 
Muignore mzee, ishi kama humuoni hivi...... Fanya yako mkuu. Kama hataki kupika we pika mwenyewe kifupi ishi tu kama upo single hivi, akitishia kuondoka msisitizie kuwa nauli utampa,,, mwambie ulimuoa ili akupe furaha sio karaha sasa ameonekana kushindwa hivyo umeamua uishi uwezavyo upate furaha. Wanawake sometimes ni wapuuzi sana ukiendelea kuwadekeza
 

Nakushauri kwa sababu hali kama hii nimewahi kukutana nayo.

Kuna mtu tulianza mahusiano vizuri sana. She was really in love hadi namuonea huruma. I loved her so much kwa sababu she was decent, very honest yani na ni msichana anayejiheshimu. We were so happy.

Ghafla akawa ni wa kununa, hana ushirikiano wa kimapenzi, ni mlazimisha mambo na wa kulaumu hata kwa kitu alichofanya mwenyewe analaumu ni kwanini sikumzuia (Hapo ukimwambia usifanye anakuambia unaleta mfumo dume kwenye mahusiano) . Nilikonda kwa sababu I really loved her and hata nikimpigia simu hatuelewani(It was so frustrating). Hataki tuonane. Nikajifunza kitu kimoja; nikawa naignore. Nikajifunza kuishi bila yeye na kumuaccomodate akirudi. It worked kwa sababu tunachuniana baada ya muda anakuja anaomba msamaha and we go on happy kisha inajirudia tena. That was our life. Nikajitahidi kumpan kila alichotaka kusuluhisha anaonesha ushirikiano kidogo kisha we are back to square one.

Nikaja kuwaza nikagundua SHE WAS NOT GETTING WHAT SHE WANTS! yani mapenzi hayakuwa vile anavyotegemea yangekuwa, na ndio alikuwa anarealize mapenzi hayako vile alivyokuwa anafikiria. Akakiri pia I was the best she could ever find lakini sasa its not what she wants!

Tafuta kumjua zaidi mkeo, tafuta anataka maisha yaweje. Just be crazy and date her all over again. Pay attention sana na ikibidi uandike ujue ANATAKA NINI OUT OF LIFE (NOT just out of u!) . Msaidie kupata maisha ayatakayo. Ndoto zake ni nini? Help her live her dreams. UJue fika kama ndoto zake hazifikii hata wewe maisha yako yanaathirika (Unfortunately that is one of the drawbacks of married life). Akiishi maisha yake happily you will have your marriage back and not before. Kama alitaka asome awe mtu fulani help her get there. Mfuatilie tu kwa sababu if we dont get what we have always dreamed about life is just working, eating and sleeping (Meaningless since we are not machines).

I always tell people, ndio unataka mke akupikie, atunze nyumba yako na watoto, akuhudumie na akupe company (Honestly this is what a man wants!). BUT If that's not all she has always dreamed about then NDOA YENU NI SHIDA!!
If you don't help her, is it worthy it to stay with a miserable wife??????

Ukiona mtu anasubbotage mahusiano makusudi hasa when you think you are happy. The hard truth is; They are not getting what they want!!!
Daah i like this coment
 
Mwache kwanza kwa mwaka 1,Dunia na maisha yakimpiga atarudii..halafu uliposema ungeoa masikini jee huyoo ni tajiri??hayo ndo yanayoyumbisha ndoa yenuuu!!
 
Maisha ni zaidi ya uyajuavyo ,pole sana mtumishi kuoa mjane au aliyeumizwa huko akaachika wakati wewe hujapotia hayo mambo ni ngumu mno ila ni changamoto tu hizo.

Ndio maana huwa mnaulizwa kwenye shida na raha ndio...

Mnafikiri ni mashairi yale sasa hiyo sio kwamba anakufanyia makusudi ila alishadhurika kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom