Unajua katika ndoa maongezi na kushirikishana (kupanga pamoja) ni kitu kinachorahisisha kila mmoja kumwelewa mwenzie na msimamo wake. Nasema hivi kwa sababu baadhi ya wanaume hawaongei na wake zao (hasa plan for future) utakuta mume anajenga, ananunua vitu mbalimbali, anafanya biashara kubwa kubwa lakini haongei wala kupanga na mkewe... mke naye anakaa kimya na kwa sababu ana pesa zake anaanza kupanga na kufanya mipango yake bila kumshirikisha mumewe. Kaa chini uongee na mkeo.... ni suala la marekebisho tuuu ukiliacha suala hili litakuwa kubwa na utavuna nyuki.
Usilipotezee swali langu.
Mkuu, mwingine atamchukua yeye lakini si nyumba. Pale ikibidi greda litapita ndio maana nipo kimya kwanza.
duu pole sana,kuchepuka is nt a solution,kaa chini na mkeo mliongelee hilo swala,mwisho wa siku nyie ndio ntakaoiokoa ndoa yenu
ubomoe nyumba kwani ipo kwako? Utaanzisha ugomvi mkubwa.
Mkuu, mwingine atamchukua yeye lakini si nyumba. Pale ikibidi greda litapita ndio maana nipo kimya kwanza.
Ha ha hata kama usingekuwa yatima, ni maelewano tu. Ndugu wanaweza kuwa baraka pia. Lakini ID ndio inatisha kidogo - love more than 100?
Hahahaaa...huo ni utata...
Natamani nikiolewa nikubaliane na mume wangu kuwa yeye ndo atakuwa na wajibu wa kunitunza na kuendesha familia, kama nikichangia kwenye mradi basi nichangie kama mtu mwingine na mapato yagawanywe, no joint account, sitomfuatilia anaingiza kiasi gani...just ahudumie familia.
Mshahara wangu haumuhusu, hatakiwi hata kujua naufanyia nini...labda tu nijisikie kumsaidia majukumu yake...
Yeye kajenga kisiri nami naibomoa kisiri vile vile
Pole.
Mkeo ameshikiwa akili,inauma ila bado yanaongeleka na kama mkeo hakuwa na nia mbaya ni ushauri mbovu tu wa dada basi mtalivuka hili salama.
Mh! Hako ka bint ka massage parlour hako!!! Kaa nako mbali maana ni kama umeanza kukafikiria kuhuisha furaha iliyokufa ndani yako. Kama ni lazima upate huduma ya massage parlour basi isiwe moja tu kama mboni ya jicho,jaribu kuchanganya leo ikiwa hapa basi next time iwe pale au kule!
Zaidi ya kumtumia dada yake kama mshauri mkuu mpaka kufikia kujenga kwa siri,kuna mapungufu mengine hasa huduma za kinyumba?
Tafuta suluhu kaka,yeye ameshamwaga mboga sasa nawe ukimwaga ugali bint yenu ndio atakayelala na njaa!!!
Weee utavaa chupi kichwani uzurure mji mzimaa maana kwa dua atakazokuombea waalai utoboi maana haikuhusuu ndo maana hujaambiwa. Na wewe si ujenge yakoo na usimshrikishee!
Ubomoe kwa sheria ya mahakama ipi na kajenga kwenuu au juu ya kiwanja chako na hata kama ni kiwanja chako ulikuwa wapi? Wee nawe unamatatizoo tuu na uenda ulioa ili ulelewee sasa kukuta hakubembelezi mtu ndio roho yakuuma! kajenge na wewe yakwako ukishirikiana na nduguzo na kama unataka kuoa wake wengi ungefunga ndoa ya bomani tena uchague kifungu cha ndoa ya wake wengi. WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZAA MPK KUWALIZA MIOYO.
Sasa hayo yatakuwa maisha kila mtu anamficha mwenzie. Ni bora kila mtu akachukua hamsini zake na uhuru wake!