Ndoa ngumu jamaani, ushauri tafadhari

Ndoa ngumu jamaani, ushauri tafadhari

unaeza mwaya kuishi na mwanaume aliyezaa nje ya ndoa, inauma sana lkn unasahau na maisha yanasonga, ilimradi km mwenyewe kaomba msamaha na kajirekebisha..

hata ukisema uondoke utaacha wangapi, unaweza kukuta huyo mwingine si malaya lkn ana tabia zingine mbaya zaidi au akawa malaya zaidi ya uliye nae sasa.

pili vumilia tu kwa ajil ya watt wako, ujue ukiondoka hapo ndio unampa mwenzio nafasi ya kuja hapo kuwa mama na mwishowe wanao walelewe na mama wa kambo..

ila ukiona machungu yamekuzidi sana waweza na wewe kurevenge na kuwa na kidumu chako kinakuliwaza huko nje ila ndoa huvunji na nyumbani huondoki.....siku hizi wanawake hatuondokagi bana hasa km mmejenga pamoja, mmezaa..tafuta furaha popote lkn baki hapo hapo

Hahahahaaaaaa mi chichemi! Usimfundishe! Ndoa itamfundisha!
 
Maisha ya ndoa ni kitendawili kigumu, wakati mwingine ni kujiongeza wewe mwenyewe na si kutegemea ushauri, nasema hivi kwa sababu kila mtu ana experience tofauti na kila mtu anadeal na changamoto zake kivyake, swali moja tu la kujiuliza " are u happy somehow? Ni ngumu kuenjoy kwa muda wote thats obvious when it comes to marriage life
 
sasa unaogopa nini ndg yangu, ndio ukweli ulivyo huo!!!!!! na hii ndio sababu kubwa ya wanawake kucheat kma ulikuwa hujui!
Kha!!! cha kufia presha na mawazo lukuki ndani kisa nini? ndio sasa wanaume wajue ubaya wa kuwasaliti wake zao, na mume wa hivo inafaa kumzalia katoto kamoja ambako si kake halafu akikua ndio unamwambia ili na yeye apate uchungu kama alioupata mke kwa yeye kuzaa nje ya ndoa....mxiuuuuu

Aisee hii kamusi ni OXFORD!
 
sasa unaogopa nini ndg yangu, ndio ukweli ulivyo huo!!!!!! na hii ndio sababu kubwa ya wanawake kucheat kma ulikuwa hujui!
Kha!!! cha kufia presha na mawazo lukuki ndani kisa nini? ndio sasa wanaume wajue ubaya wa kuwasaliti wake zao, na mume wa hivo inafaa kumzalia katoto kamoja ambako si kake halafu akikua ndio unamwambia ili na yeye apate uchungu kama alioupata mke kwa yeye kuzaa nje ya ndoa....mxiuuuuu

kwa mchango huu wanaume wenye wake mjichunge sana.
 
Sikuwahi kujua nilikuwa mkubwa mpk ndoa yangu ilipofika hapa!
Ghafla niliacha kuamini vyote nilivyowahi kuamini
Ghafla nilijikuta natakiwa kujishauri
Buuuuuut best part of it
Ghafla niliijua Nguvu ya Mungu katika maisha ya mwanadamu!
Aseee hebu nyanyuka hapo litazame hilo hivi
" tendo alilolifanya ulipokuta sms na simu ya honey nimekumiss ndio tendo hilo hilo alilofanya mpk akazaliwa huyo mtoto"
Sawa eeenh?
Hatushindwi maisha kwa maanguko ya watu wengine
Hatuachi kusonga mbele kwa ajili ya kushindwa watu wengine
Hatuukatai ukweli wa maisha eti kwa sababu fulani haoni thamani ya maisha hayo
Unabaki kuwa kiumbe mwenye akili,mamlaka na utashi sahihi kwa furaha sahihi kwa nafsi yako.
Ni hatua ngumu sana kuivuka ukiwa salama.MNO
Ila ukifanikiwa aseee maisha yanakuwa ni kitu Aziz sana kuliko ulivyowahi kufikiri!
Karibu kwa ushauri wa kigeloish zaidi
Anytime!
 
Mbona unauliza maswali magumu wakati haujayavulia nguo hayo maji? Navyojua wanawake mmepewa moyo wa uvumilivu na wenye kusamehe hivyo kama mmeo akichepuka msamehe kama anawatoto wengine nje mshawishi awakusanye uwalee kwa moyo wa upendo

Napenda kufahamishwa ni mambo gani ya kuvumilia katika ndoa na yapi sio ya kuvumilia?(Yaani yapi yakitokea ndoa ife? na yapi ya kusamehe)

Unawezaje kumsamehe na kuendelea kuishi na mwanaume ambaye amezaa nje ya ndoa tayari akiwa katika ndoa?

Inamaanisha nini watu wanaposema vumilia katika ndoa kwa ajili ya watoto?, eti usiwe m-binafsi kujiangalia mwenyewe.

Na maneno kama simama upiganie ndoa yako. napiganaje?

Je ni mwanamke pekee ndo anahitajika kupigania ndoa yake?
 
kwa kweli kwa wanaume wa sasa hii ndio inatakiwa!!!!!! kama wewe hupendi kuchitiwa kwa nn umcheat mwenzio, mkuki kwa nguruwe sio?
hakuna kitu mbaya na inayoumiza kwenye ndoa kama mtu kucheat, na bora basi acheat responsibly, yaani kujiachia hadi kutia mimba, halafu eti unategemea mama nanihiii atasamehe ivi ivi tu....hiyo ilikuwa ni enzi za mababu zetu bhana......revenge inakufanya uwe mind settled na kupunguza machungu kwa sana
.

Umewahi fikiri hasara ya kuwa na watoto ulio changanya baba tofauti...
 
Napenda kufahamishwa ni mambo gani ya kuvumilia katika ndoa na yapi sio ya kuvumilia?(Yaani yapi yakitokea ndoa ife? na yapi ya kusamehe)

Unawezaje kumsamehe na kuendelea kuishi na mwanaume ambaye amezaa nje ya ndoa tayari akiwa katika ndoa?

Inamaanisha nini watu wanaposema vumilia katika ndoa kwa ajili ya watoto?, eti usiwe m-binafsi kujiangalia mwenyewe.

Na maneno kama simama upiganie ndoa yako. napiganaje?

Je ni mwanamke pekee ndo anahitajika kupigania ndoa yake?

Mnaya sababisha wenyewe mnakuja kulia lia hapa! Mpaka akazae nje wewe ulikuwa wapi, ...... - *c
 
Napenda kufahamishwa ni mambo gani ya kuvumilia katika ndoa na yapi sio ya kuvumilia?(Yaani yapi yakitokea ndoa ife? na yapi ya kusamehe)
Mkuu ni vigumu kujibu swali hili kwa ujumla kwani kila mtu ana mtazamo tofauti kuhusu ndoa . Utofauti huo wa mitazamo unasababishwa na familia uliyotoka na watu wanaokuzunguka bila kusahau malezi tuliyopata toka tungali wadogo.

Unawezaje kumsamehe na kuendelea kuishi na mwanaume ambaye amezaa nje ya ndoa tayari akiwa katika ndoa?
Hili ni swali la msingi nafikiri itakua vema kama muhusika angeulizwa kulikoni mpaka akaenda huko na kujipatia uzao. Huenda kulingana na maelezo yake waweza kusamehe na maisha yakasonga au mwingine hii ndo inakua sababu ya kuvunja ndoa. Kwa hiyo tunatofautiana maamuzi ktk hili na maamuzi yote ni mazuri lkn uamuzi wa kuvunja ndoa lazima uutafakari kwa kina na uwe wa kutoka moyoni kwani kama uamuzi huo haukutoka moyoni utajikuta unawalaumu watu wengine na kuishi maisha ya lawama.
Inamaanisha nini watu wanaposema vumilia katika ndoa kwa ajili ya watoto?, eti usiwe m-binafsi kujiangalia mwenyewe.
Hili nalo linahitaji moyo. Kuna wamama walivumilia lkn wengine walikufa kwa maradhi na mambo mengi. Kama nilivyosema maamuzi yanayohusu maisha ya ndoa kila mmoja ana mtazamo wake . Hii ndio silaha kubwa wanayoitumia wanaume kuwaumiza wake zao kwa kuwaambia wavumilie kwa sababu ya watoto . Nafikiri watoto ni wenu wote hivyo kama mkiachana kistaarabu anapaswa kuwatunza watoto. Kuna wengi hawakuondoka kwa sababu ya mali lkn kwa bahati mbaya magonjwa hayakuwaacha walijikuta hata hao watoto walibaki yatima. Maamuzi mazuri ni yale anayoyafanya mtu toka nafsini mwake na si kufuata wengine wanasemaje. Yote hii ni ktk kuepuka maumivu ya ndani kwa ndani na kujilaumu kwamba kama si wale nisingeondoka au ningeondoka na kuanza maisha upya.

Na maneno kama simama upiganie ndoa yako. napiganaje?
Mkuu tunapigania ndoa zetu kwa sala na maombi na mara nyingi tunaombea afya na baraka ktk shughuli zetu za kila siku. Huwa hatufanyi maombi eti mume wangu asiwe na kimada mmmh hapana kwani kuwa na kimada si jambo la bahati mbaya ni mpango kamili uliosukwa kwa muda mrefu na muhusika .Kwa hiyo basi kuna mambo ya kuombea na mengine ni utashi wa mtu yanapaswa kukabiliwa kwa mazungumzo . Tunaenda mbali zaidi kama kuna kasoro unaziona kwa mwenzako basi unazihoji kwa upendo ili kujiondolea wasi wasi.

Je ni mwanamke pekee ndo anahitajika kupigania ndoa yake?
Hapana kama kupigania ndoa unamaanisha kuiombea basi mwenye macho kati yenu ndiye anayeweza kumsaidia mwingine kuipigania ndoa. Lkn kwa mtazamo wangu nafikiri kabla ya kufika huku kote ni bora mkakaa na mwenzako na kujiuliza mlitoka wapi , mko wapi na mnakwenda wapi. Maswali haya yatawasaidia kuanza upya kwani kuishi kwa kutegeana si jambo jema na inafanya ndoa kuwa chungu na ngumu kuiishi. Ndoa yangu ina 15+ na sina experience kama hii , labd nikuambie tumewezaje kufika hapa. Kwanza upendo wetu haujawahi kupungua na kila mmoja wetu anaona ana wajibu juu ya mwenzake, uaminifu na kuchukuliana. Hivyo kwa njia hii imepelekea kuwa na ndoa yenye amani na furaha . Ila kitu kikubwa tunachotumia ni kumtegemea Mungu yaani kila mmoja wetu amejikomiti kwa Muumba wake.

Kabla ya kufanya maamuzi magumu rudi moyoni mwako na tafakari kwa kina ili ufanye uamuzi ulio bora.
 
Mnaya sababisha wenyewe mnakuja kulia lia hapa! Mpaka akazae nje wewe ulikuwa wapi, ...... - *c
Hapana sijalia na siwezi lia kwa hili. Siishi kwa kumtumainia mwanadamu mwenzangu mpaka anilize kwa matendo yake. Mpaka muda kalia yeye kwa aliyoyafanya.
 
Hivi mkuu hapa umeniitia nini bana?

Kama unadhani mimi ni mtu wa mitaala umekosea kabisaaaa

I hate that thing for sure!


Umenifurahisha Eiyer....! Wewe wa ukweli.... Mwaaaaaa!
 
Ndoa sio ngumu,unachokijenga kichwani ndicho kinachokupa ugumu,!
 
Umenifurahisha Eiyer....! Wewe wa ukweli.... Mwaaaaaa!

images
 
Ukitaka kujua uzuri wa ndoa hasa wewe mwanamke jitoe ukishaingia, ndoa haipimwi kwa tangibles. Amka.
 
[QUOTE Nyani Ngabu;1. Kutembea nje ya ndoa au niseme usaliti, uwe wa kihisia au kimwili. Hili kwangu halina mjadala kabisa. If I find out you're two-timing on me, we are through. I call it one strike and you're out policy.

2. Physical violence. Ukinitwanga na frying pan kichwani au ukinitandika chupa ya Balimi usoni, kutakuwa hakuna tena ndoa hapo. Kwa sababu nita-swing for the fences, and if I connect, lights out. Lose-lose situation there.

3. Vices nyingine kama ulevi usio wa kupindukia, uvutaji sigara, matumizi mabaya ya pesa, uvivu wa kufanya kazi, kuvaa nguo kama hoochie mama, kutumia lugha chafu chafu, uchafu wa mwili na mazingira, ili mradi tu hazijavuka mipaka na kuwa kero ambazo siwezi kuzivumilia, nadhani ni vitu ambayo mimi na yeye tunaweza kukaa chini, tukavijadili, na kukubaliana namna ya kuvikabili na kuvirekebisha.

Lakini watu tumetofautiana. Wapo ambao hata wachitiwe namna gani bado watang'ang'ana kupigania ndoa zao. Wengine hata wawe wananyanyaswa kiasi gani, iwe kihisia au kwa kupigwa bado tu watang'ang'ana.

Well, siwezi kuwakosoa sana maana huo ni uamuzi wao. Lakini huwa siamini katika upuuzi wa kudhani kuwa kwa vile tu mtu uko kwenye ndoa na kwa vile labda mna watoto basi ndo uendelee kuvumilia kila aina ya upuuzi na ujinga.

Kufanya hivyo (kuvumilia kila aina ya upuuzi na ujinga) ni kuwa mpuuzi na mjinga. Hata kama kuna watoto, hiyo haina maana ndo ushikwe mateka katika ndoa yenye kila aina ya manyanyaso.

Inafika wakati mtu unaweka mguu wako chini, unachora mstari na kusema 'sasa basi, imetosha'. Unasepa unaenda kuendelea na maisha yako.


Mtoa mada Realme;

Mimi siafiki kikubwa na ushauri uliotolewa na Nyani Ngabu kwa vile nadhani uchambuzi wake sio mpana vya kutosha. Hapa nitaeleza kwanini nahisi ushauri huu hautatatua tatizo lako. Tuanze na wanaovunja ndoa zaidi duniani.

1. Nchi kumi zinazoongoza kwa kuvunjika ndoa duniani ni hizi hapa

Countries with Highest Divorce Rates - World Top Ten

Hamna nchi yoyote ya kiafrika. Kabla yeyote hajarukia kuwa Afrika haipo kwa vile ni masikini basi azonagatie kuwa Japan, Ujerumani, China, Marekani hawamo. Katika hizi kumi nyingi ni za ulaya kaskazini na haswa Scandinavia. Hapa la maana ni kwamba kuwa zile nchi zenye kuenzi tamaduni zao, basi hazimo katika kumi bora. Kinachofanana katika nchi hizi ni kule kuaminishwa sana na social media zao kama vile kuolewa ni utumwa. Hawa wanavunjiwa ndoa na social media. Sio culture. Hapa kwetu kudumisha ndoa yako kunaegemea sana umelelewa vipi (zamani ilikuwa kuwekwa ndani 1-2 months, ikazomewa ikapuuzwa, leo inaitwa kitchen party-1 day). Curricular zinafanana ila muda hautoshi (1 day) kwa wanafunzi wa enzi zetu.


2. Hebu tuangalie sababu kubwa zinazovunja ndoa nyingi SIKU HIZI(nachukua mfano toka Afrika Kusini)

Marriage Counselling- combatting SA’s high divorce rate «

Utaona kuwa sumu nambari moja ni Financial stress and Pressure, ikifuatiwa na SOCIAL MEDIA> Baada ya hapo ndipo unakuta Ku-cheat, Addiction na kama Lack of Communication.

Hapa kwenye Social media lazima uweke aina zote ya mawasiliano. Anzia marafiki, facebooks, emails, simu, JF, na vijiwe vya kijinsia ambavyo ni nadra kupeana ushauri wa kustahimili. Na hapo kwenye Financial stress na Pressure ni papana sana. Ila kila mwanaume mwenye mke na watoto anapajua. Tena kama kachukua hii mikopo (ya kuendeleza kina mama!!!!) halafu imefika siku ya marejesho na hana kitu, hiyo dhahama kwa wewe mume utajuta!!!! Wanachosema hapa ni kuwa pato la familia kuyumba na ushawishi toka nje ndivyo vyanzo vikuu vya matatizo.

Baada ya kuyaona hayo, sasa tuna focus tatizo lako.
- Hapa Tanzania ndoa nyingi zinavunjika mikoa ya pwani ambako watu wake wala siyo VIONGOZI WA KU-CHEAT WALA KUPIGA. Kwa maana hiyo ushauri wa hapa juu kuwa ukipigwa tuu au mume akiiba mdada mwingine wewe unasepa hauelezi ukweli wa matukio yalivyo nchi hii. Potelea mbali, kama wewe ni mwepesi wa kutelekeza ndoa yako sababu umepigwa basi ondoka bila kumwona wala kumuita yule anayeamua kuwa na subira kuwa ni MJINGA. Wewe sepa na WEREVU wako.

- Tutumie mifano hai, Mikoa yenye kuripotiwa vipigo vingi kwa wanandoa imeshamiri kanda ya Kati, kaskazini na Ziwa. Yaani Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na mikoa ya Ziwa haswa Mara. Lakini jee, utasema ni mikoa hii hii ndiyo yenye ndoa zinazovunjika kwa wingi Tanzania? Mbona ni kama kinyume? Na hapa ndipo utaona UKWELI WA HUU UTAFITI WA SOUTH AFRICA kwamba FINANCIAL STABility ndio inachangia SANA NDOA kuyumba. Huko Ulaya ndoa zinakufa sababu ya Social media kushabikia mno mambo ambayo yanahatarisha maisha ya wanandoa kama ushoga, usagaji na pornography bila kuweka vipindi sawia ili watu waenzi maisha ya kifamilia.

- Ndugu yangu lazima uwe Jasiri KUU-FACE UKWELI; Wanaume kuzaa nje ya ndoa zao hakutaisha na leo na wala hawataacha kwa vile wanasemwa hapa JF. Wakwako sio wa mwisho. Na wala hakuanzisha balaa hili. Rais mmoja wa Ufaransa (yeye alikuwa na watoto wawili kabisa). Orodha wa wazito tena wenye watoto ni ndefu mno. Hujaingia orodha ya watumishi wa Bwana wenye watoto na wake za watu. Tosheka kuwa sio wewe peke yako alikuwa majeruhi wa tatizo hili. Sidhani kusepa ni BIMA AU CHANJO ya tatizo lako. Dawa ni meza ya Mazungumzo na MUMEO. Chumbani.

- Ukweli mwingine unaokufuata ni kuwa WATOTO WAKO wa Kuzaa hawatahuzunika kama wewe. Jiandae, siku moja lazima utawasikia wanacheka wakisema wamempata DOGO. Kama Unaye haswa binti jiandae na kauli kuwa "yule dogo ni baba mtupu" Hii kauli utaambiwa tu na mwanamke mwenzio (binti yako)hata kama utaolewa baada ya kusepa.

MAWAZO YANGU
1. Huna haja ya kusepa. Linda ndoa yako. Kwani umefukuzwa? Upo uwezekano chanzo kilichompelekea huu mwanya labda umechangia. HUWEZI JUA. Wewe tafakuri, fungua mawasiliano na mwenzio, kisha taratiiiiiibu rekebisha BOMA lako.

2. Zidisha mawasiliano rafiki kati yako na mumeo juu ya mtoto huyu hii itasaidia kumwondolea uwezekana wa kulirudia hili pengine.

3. Usifuate KILA ushauri wa SOCIAL networks na media. Pia Huna haja ya kuapa kulipiza kisasi kwa mama mtu. Hakuna haja na wala haina tija.

4. Kila nyumba ina matatizo yake. Haya ya kwako ni matatizo. lakini nakushauri sana tunza ndoa yako. Ilimradi hujamdhulumu huyu bwana kama mkewe kwa hakika lazima Mwenyezi Mungu atakufanyia wepesi. Usikimbie nyumba yako, wanao,na kiapo chako, wende kuwa mdada huna mwenyewe kila mtu anajipanga kukuwahi mwisho na wewe kama mumeo uishie kuzaa watoto wa mababa wengine.

Wengine wataboresha mapungufu yangu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom