OLESAIDIMU
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 19,139
- 9,574
Wakuu Nyani Ngabu na Eiyer napiga kura za wazi kuunga mkono hoja!!!!!!
Last edited by a moderator:
'kwenye maisha hakuna jambo baya au zuri ila wewe mwenyewe ndie unaeamua kulipa tafsiri'.. well said eiyer
Napenda kufahamishwa ni mambo gani ya kuvumilia katika ndoa na yapi sio ya kuvumilia?(Yaani yapi yakitokea ndoa ife? na yapi ya kusamehe)
Unawezaje kumsamehe na kuendelea kuishi na mwanaume ambaye amezaa nje ya ndoa tayari akiwa katika ndoa?
Inamaanisha nini watu wanaposema vumilia katika ndoa kwa ajili ya watoto?, eti usiwe m-binafsi kujiangalia mwenyewe.
Na maneno kama simama upiganie ndoa yako. napiganaje?
Je ni mwanamke pekee ndo anahitajika kupigania ndoa yake?
Tatizo katika jamii ni namna hiyo mitala inavyoanza, mingi inaanza kwa udanganyifu, dharau na dhuruma kwa mke aliyatangulia.na hiyo inapelekea chuki na machungu kwa wanawake wenyewe na watoto wanaozaliwa katika mitala. kama wewe ni wamitala kwa nini ukiri tena wengine kanisani ndoa ya mke mmoja? kama unajiamini wewe wa mitala kwa nini udanganye kwanza usubiri mpaka hawara anawatoto 3 ndo umwambie mkeo kuna mwenzio, kama umeamua kuvunja mkataba mjulishe mwenzio kabla hujawa na huyo mwingine ili nae aamue kama atabaki kwenye mitala au ataondoka. Mitala ya siku hizi inaendeshwa kwa siri,na fujo nyingi. inafika mpaka mke mdogo anaamua kujitambulisha mwenyewe kwa familia ya mwanaume na mke mkubwa eti namimi ni mke wa furani nimefunga nae ndoa ya serikali.afu ujidai unamitala hata kuihandle huwezi kwa kizazi hiki hamna mitala ni vurugu tu na matatizo katika jamii.
Napenda kufahamishwa ni mambo gani ya kuvumilia katika ndoa na yapi sio ya kuvumilia?(Yaani yapi yakitokea ndoa ife? na yapi ya kusamehe)
Unawezaje kumsamehe na kuendelea kuishi na mwanaume ambaye amezaa nje ya ndoa tayari akiwa katika ndoa?
Inamaanisha nini watu wanaposema vumilia katika ndoa kwa ajili ya watoto?, eti usiwe m-binafsi kujiangalia mwenyewe.
Na maneno kama simama upiganie ndoa yako. napiganaje?
Je ni mwanamke pekee ndo anahitajika kupigania ndoa yake?
Mtoa mada kuwa mvumilivu na usome hiki kisa kilichotokea mbele ya macho yangu
Jamaa yangu wa karibu sana alikuwa na mke ambae waliishi kwa upendo mkubwa sana kwa muda wa miaka 4 ,maisha yaliendelea kama kawaida lakini jamaa yangu huyu kuna kitu hakukijua kwa mkewe ambacho ni usaliti ambao mkewe alikuwa anaufanya kwa siri sana
Kama ilivyo ada jamaa yangu alikuja kumfumania siku moja tena ndani ya nyumba yake mwenyewe
Jamaa yangu alipanga kumuacha mkewe lakini kabla ya kufanya hivyo aliamua kwenda kumtaarifu baba yake.Baada ya kumpa baba yake hizi taarifa baba yake alimuambia kuwa kama ana uhakika mwanamke ambae atakuja kumuoa hata msaliti kama huyu,jamaa yangu alisema ana uhakika.Baba yake alimuuliza huo uhakika kama alikua nao wakati anamuoa huyu wa sasa na akasema ni kweli alikuwa na uhakika,baba yake akamuambia ni kitu gani kimetokea hadi akasalitiwa jamaa yangu hakuwa na jibu
Baba yake akamuambia kuwa kuna wakati unaweza kukosewa na ukasamehe tu bila ya kujiuliza sana kwani maisha ndivyo yalivyo na inawezekana jamaa yangu akawa huyu tunaezungumza nae sio baba yake halisi kwani huenda mama yake alifanya mambo ya hovyo nyakati hizo,Jamaa yangu kusikia hivyo aling'aka na kusema kuwa mama yake hawezi kufanya hivyo,baba yake akamuuliza kuwa kama akithibitisha hilo atafanya nini jamaa yangu akasema kuwa kama mama yake nae alikuwa au anafanya uhuni basi hatamuacha mkewe kwasababu anamuamini sana mama yake
Basi baba yake alimuambia jumapili dadazake na jamaa yangu watakuwepo nyumbani kwani watakuja kusalimia kutoka huko walikoolewa na mama yake atakuwepo na akamuagiza aje tu asubuhi na akija wakiwa sebuleni yeye na baba yake ajidai kuwa ameanguka na kuzimia ili awe anasikiliza kitakachokuwa kinaendelea
Kama kawaida jumapili ilifika na jamaa yangu alikwenda na aliniomba niende nae na alinijulisha kila kitu,tulifika na tuliwakuta wote kama baba yake na jamaa alivyosema na baada ya kusalimiana nao walikwenda jikoni kuandaa chai na sisi yaani mimi,jamaa yangu na baba yake jamaa yangu walituacha sebuleni
Baada ya nuda baba yake jamaa yangu alimuambia jamaa yangu kuwa huu ni wakati muafaka wa tukio kwani kuna mtu ameshamuandaa wakuja kufanya jambo,basi jamaa yangu alilala chini na baba yake jamaa yangu aliwaita dada zake na mama yake jamaa yangu kwa hamaki kuwa jamaa yangu amepatwa na tatizo,kama kawaida ya wanawake walikuja kwa hamaki na kuanza kuhaha bila majibu.Kiukweli nilijikaza sana nisicheke kwani ilikuwa kama tunacheza muvi
Baba yake na jamaa yangu alisema ngoja amfuate mzee mmoja ambae huwa anamfanyia mambo yake ambae huwa anaishi jirani sana na nyumbani pale,basi baba yake na jamaa yangu alikwenda na bila kupoteza muda yule mzee alikuja na kuanza kumtibu jamaa yangu kwa geresha tu kwani ishu alikuwa anaijua na baada ya nuda alisema kuwa mizimu ja kwao na baba yake ilikuwa imekasirika kidogo lakini ameipoza na dawa pekee ni mtu ambae ni msafi [ambae hajafanya ngono nje ya ndoa kwa muda wa wiki moja uliopita] akamguse jamaa yangu kichwani na fahamu zitamrejea,kumbuka hiulo linafanyika mimi nipo pamoja na jamaa yangu aliyejidai kuzimia pamoja na dada zake wawili ambao wameolewa na mama yake jamaa yangu
Basi yule mzee "mtaalam' alianza kumuita dada yake jamaa yangu akamguse jamaa yangu akagoma,akamuita wa pili akagoma kisha akamuita mama yake jamaa yangu nae akagoma kisha akaitwa baba yake na jamaa yangu na akaenda kumshika kichwani na jamaa yangu akainuka
Yule mzee akamuagiza mambo ya kufanya ili asirudiwe na ile kadhia mambo ambayo kiuhalisia yalikuwa ni geresha tu na yule mtaalam aliondoka na dada na mama ya jamaa yangu walirudi kwenye mambo yao ya kuandaa chai
Unajua nini kilitokea ni kuwa jamaa yangu hata chai ilimshinda na tuliondoka,jamaa yangu alisema kumbe haya mambo yanafanyika na hata mama yangu na utu uzima wake anafanya? Aliamua kutokumuacha mkewe na sasa wana watoto wawili na ndoa yao haikuwahi kupata mgogoro tena
Ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kwenye maisha hakuna jambo baya au zuri ila wewe mwenyewe ndie unaeamua kulipa tafsiri
Hilo lako unaweza kuliona kuwa ni baya au la kawaida tu na ukaendelea na maisha yako na huyo bwana au ukaamua kuachana nae
Lakini kuachana nae sio gerentii ya kuja kumpata ambae ametulia,kama unaachana nae achana nae kwasababu nyingine na sio uaminifu kwani huenda ukaja kumkosa muaminifu na ukajilaumu sana kumuacha huyo ambae tayari mmeshaishi kwa muda na mnafahamiana kwa mambo mengi!
Rudia kusoma naona umemiss sehemu ya maelezommh!ina maana huyo baba alikuwa anajua kwamba mkewe anachepuka? au mama naye alikuwa sehemu ya deal (alijua kinachoendelea) ili kuokoa ndoa ya kijana
Hivi mwanamke unachapiwaje?Back to the topic, kuchapiwa kunauma sana hata kwa wanawake. Dada hayo mambo ni magumu, sijui hata nikwambieje maana mi ningeshamuhamisha ndani kwa muda kama sio mimi kuhama, ili tujitafakari kwanza. Ila, kila mtu ana jinsi yake ya ku-react akikutwa na hayo mambo.
Usikae na kujifungia ndani ukiwaza na kulia. kama ni muajiriwa, fanya kazi sana ili kupunguza mawazo, work extra hours. Nenda gym baada ya kazi, kula vizuri kwa ajili ya afya ya mwili na ya akili.
Rudia kusoma naona umemiss sehemu ya maelezo
Du! Mtambuzi, unakumbuka mpaka ya nyuma,. Kweli wanaume watu wa ajabu sana.Nimekumbuka haya maoni yako katika huu uzi hapa chini, kumbe it was like time bomb, sasa limekulipukia, wanaume ni watu wa ajabu sana eh...!
https://www.jamiiforums.com/mahusia...e-kwa-asili-wanaume-ni-watu-wa-mitala%85.html
Kumbuka hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja muda wote.Wanatamani kama watoto wachanga1. Kutembea nje ya ndoa au niseme usaliti, uwe wa kihisia au kimwili. Hili kwangu halina mjadala kabisa. If I find out you're two-timing on me, we are through. I call it one strike and you're out policy.
2. Physical violence. Ukinitwanga na frying pan kichwani au ukinitandika chupa ya Balimi usoni, kutakuwa hakuna tena ndoa hapo. Kwa sababu nita-swing for the fences, and if I connect, lights out. Lose-lose situation there.
3. Vices nyingine kama ulevi usio wa kupindukia, uvutaji sigara, matumizi mabaya ya pesa, uvivu wa kufanya kazi, kuvaa nguo kama hoochie mama, kutumia lugha chafu chafu, uchafu wa mwili na mazingira, ili mradi tu hazijavuka mipaka na kuwa kero ambazo siwezi kuzivumilia, nadhani ni vitu ambayo mimi na yeye tunaweza kukaa chini, tukavijadili, na kukubaliana namna ya kuvikabili na kuvirekebisha.
Lakini watu tumetofautiana. Wapo ambao hata wachitiwe namna gani bado watang'ang'ana kupigania ndoa zao. Wengine hata wawe wananyanyaswa kiasi gani, iwe kihisia au kwa kupigwa bado tu watang'ang'ana.
Well, siwezi kuwakosoa sana maana huo ni uamuzi wao. Lakini huwa siamini katika upuuzi wa kudhani kuwa kwa vile tu mtu uko kwenye ndoa na kwa vile labda mna watoto basi ndo uendelee kuvumilia kila aina ya upuuzi na ujinga.
Kufanya hivyo (kuvumilia kila aina ya upuuzi na ujinga) ni kuwa mpuuzi na mjinga. Hata kama kuna watoto, hiyo haina maana ndo ushikwe mateka katika ndoa yenye kila aina ya manyanyaso.
Inafika wakati mtu unaweka mguu wako chini, unachora mstari na kusema 'sasa badi, imetosha'. Unasepa unaenda kuendelea na maisha yako.
Na bado anaendelea na LULUKapteni John Komba aliwahi kusema akihojiwa na Salama kuwa anampenda sana mkewe kwa sababu alipoteleza(kuzaa nje ya ndoa) mkewe huyo alimsamehe na kuendelea kumlelea huyo mtoto wa nje.Life Goes on...
Na akiwa mwanamke ndio kazaa nje ya ndoa, mwanaume avumilie tu na ikibidi achukue amlee na hapo mkewe atampenda sana??!!Kila mtu na moyo wake au hisia zake,na wanaume wengi wanafanya siri jambo hili la kuzaa nje ya ndoa na kama kakwambia basi hakuwa na nia ya kukupoteza tofauti ungesikia kwa watu wengine ,we vumilia tena chukua kabisa ulee maisha yaende ,I swear to u mumeo atakupenda zaidi ya hapo .
unaeza mwaya kuishi na mwanaume aliyezaa nje ya ndoa, inauma sana lkn unasahau na maisha yanasonga, ilimradi km mwenyewe kaomba msamaha na kajirekebisha..
hata ukisema uondoke utaacha wangapi, unaweza kukuta huyo mwingine si malaya lkn ana tabia zingine mbaya zaidi au akawa malaya zaidi ya uliye nae sasa.
pili vumilia tu kwa ajil ya watt wako, ujue ukiondoka hapo ndio unampa mwenzio nafasi ya kuja hapo kuwa mama na mwishowe wanao walelewe na mama wa kambo..
ila ukiona machungu yamekuzidi sana waweza na wewe kurevenge na kuwa na kidumu chako kinakuliwaza huko nje ila ndoa huvunji na nyumbani huondoki.....siku hizi wanawake hatuondokagi bana hasa km mmejenga pamoja, mmezaa..tafuta furaha popote lkn baki hapo hapo
Mtoa mada kuwa mvumilivu na usome hiki kisa kilichotokea mbele ya macho yangu
Jamaa yangu wa karibu sana alikuwa na mke ambae waliishi kwa upendo mkubwa sana kwa muda wa miaka 4 ,maisha yaliendelea kama kawaida lakini jamaa yangu huyu kuna kitu hakukijua kwa mkewe ambacho ni usaliti ambao mkewe alikuwa anaufanya kwa siri sana
Kama ilivyo ada jamaa yangu alikuja kumfumania siku moja tena ndani ya nyumba yake mwenyewe
Jamaa yangu alipanga kumuacha mkewe lakini kabla ya kufanya hivyo aliamua kwenda kumtaarifu baba yake.Baada ya kumpa baba yake hizi taarifa baba yake alimuambia kuwa kama ana uhakika mwanamke ambae atakuja kumuoa hata msaliti kama huyu,jamaa yangu alisema ana uhakika.Baba yake alimuuliza huo uhakika kama alikua nao wakati anamuoa huyu wa sasa na akasema ni kweli alikuwa na uhakika,baba yake akamuambia ni kitu gani kimetokea hadi akasalitiwa jamaa yangu hakuwa na jibu
Baba yake akamuambia kuwa kuna wakati unaweza kukosewa na ukasamehe tu bila ya kujiuliza sana kwani maisha ndivyo yalivyo na inawezekana jamaa yangu akawa huyu tunaezungumza nae sio baba yake halisi kwani huenda mama yake alifanya mambo ya hovyo nyakati hizo,Jamaa yangu kusikia hivyo aling'aka na kusema kuwa mama yake hawezi kufanya hivyo,baba yake akamuuliza kuwa kama akithibitisha hilo atafanya nini jamaa yangu akasema kuwa kama mama yake nae alikuwa au anafanya uhuni basi hatamuacha mkewe kwasababu anamuamini sana mama yake
Basi baba yake alimuambia jumapili dadazake na jamaa yangu watakuwepo nyumbani kwani watakuja kusalimia kutoka huko walikoolewa na mama yake atakuwepo na akamuagiza aje tu asubuhi na akija wakiwa sebuleni yeye na baba yake ajidai kuwa ameanguka na kuzimia ili awe anasikiliza kitakachokuwa kinaendelea
Kama kawaida jumapili ilifika na jamaa yangu alikwenda na aliniomba niende nae na alinijulisha kila kitu,tulifika na tuliwakuta wote kama baba yake na jamaa alivyosema na baada ya kusalimiana nao walikwenda jikoni kuandaa chai na sisi yaani mimi,jamaa yangu na baba yake jamaa yangu walituacha sebuleni
Baada ya nuda baba yake jamaa yangu alimuambia jamaa yangu kuwa huu ni wakati muafaka wa tukio kwani kuna mtu ameshamuandaa wakuja kufanya jambo,basi jamaa yangu alilala chini na baba yake jamaa yangu aliwaita dada zake na mama yake jamaa yangu kwa hamaki kuwa jamaa yangu amepatwa na tatizo,kama kawaida ya wanawake walikuja kwa hamaki na kuanza kuhaha bila majibu.Kiukweli nilijikaza sana nisicheke kwani ilikuwa kama tunacheza muvi
Baba yake na jamaa yangu alisema ngoja amfuate mzee mmoja ambae huwa anamfanyia mambo yake ambae huwa anaishi jirani sana na nyumbani pale,basi baba yake na jamaa yangu alikwenda na bila kupoteza muda yule mzee alikuja na kuanza kumtibu jamaa yangu kwa geresha tu kwani ishu alikuwa anaijua na baada ya nuda alisema kuwa mizimu ja kwao na baba yake ilikuwa imekasirika kidogo lakini ameipoza na dawa pekee ni mtu ambae ni msafi [ambae hajafanya ngono nje ya ndoa kwa muda wa wiki moja uliopita] akamguse jamaa yangu kichwani na fahamu zitamrejea,kumbuka hiulo linafanyika mimi nipo pamoja na jamaa yangu aliyejidai kuzimia pamoja na dada zake wawili ambao wameolewa na mama yake jamaa yangu
Basi yule mzee "mtaalam' alianza kumuita dada yake jamaa yangu akamguse jamaa yangu akagoma,akamuita wa pili akagoma kisha akamuita mama yake jamaa yangu nae akagoma kisha akaitwa baba yake na jamaa yangu na akaenda kumshika kichwani na jamaa yangu akainuka
Yule mzee akamuagiza mambo ya kufanya ili asirudiwe na ile kadhia mambo ambayo kiuhalisia yalikuwa ni geresha tu na yule mtaalam aliondoka na dada na mama ya jamaa yangu walirudi kwenye mambo yao ya kuandaa chai
Unajua nini kilitokea ni kuwa jamaa yangu hata chai ilimshinda na tuliondoka,jamaa yangu alisema kumbe haya mambo yanafanyika na hata mama yangu na utu uzima wake anafanya? Aliamua kutokumuacha mkewe na sasa wana watoto wawili na ndoa yao haikuwahi kupata mgogoro tena
Ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kwenye maisha hakuna jambo baya au zuri ila wewe mwenyewe ndie unaeamua kulipa tafsiri
Hilo lako unaweza kuliona kuwa ni baya au la kawaida tu na ukaendelea na maisha yako na huyo bwana au ukaamua kuachana nae
Lakini kuachana nae sio gerentii ya kuja kumpata ambae ametulia,kama unaachana nae achana nae kwasababu nyingine na sio uaminifu kwani huenda ukaja kumkosa muaminifu na ukajilaumu sana kumuacha huyo ambae tayari mmeshaishi kwa muda na mnafahamiana kwa mambo mengi!
...Ukishamvulia mwanaume mwingine, ukaamua kuwa mtupu mbele zake, ukaamua kupanua...akafanya yake, hakika nitakuacha, hamna mjadala katika hilo...
Nimesoma hadi nkaogopa ikiwa ulichoandika ndio uhalisia