Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 69
- 252
Cha mno ni nini hasa?
Nini matarajio yako nje ya ndoa yako uliyonayo sasa?
Ninini?, kwamba uliamini kwamba mwenzi wako ni malaika? Au unaamini kwamba ukimwacha huyo then utampata mtakatifu asiyekukosea, asiye saliti wala kukuudhi au uliaminishwa kwamba anayekuoa au umuoae atakuridhisha kwa kila sekta? Bahati mbaya mtu wa aina hiyo bado hajazaliwa na hatozaliwa!
Huyo uliyenaye pamoja na kasoro zake zote ndiye uloandikiwa, jukumu lako ili kutimiza Neno hilo ni kumvumilia tu ili kujisitiri wewe na mwenzio na familia yako kwa ujumla. Kama itathibitika ulikosea kuoa au kuolewa ndugu yangu hiyo ni kashfa, jitahidi kuificha kashfa hiyo. Kuna wanaoamini kwamba ukikutana na aliyeacha au kuachika basi mwangalie kwa macho matatu kwa sababu ni dariri kwamba ni dhaifu wa mahusiano, havumiliki au hajui kuvumilia na kuzikabili changamoto za mahusiano, Kwanini uruhusu jamii ikuangalie hivyo?
Nikikumbushe kidogo, ndoa huwa tamu saaana katika hatua tatu tu, moja ni kabla ya ndoa yenyewe, mwenzio utamuona ni katika watu bora duniani, pili ni wakati wa ndoa yako, ona watu wanavyoacha yao kuhangaika na wewe huku wakijinyima kukuchangieni, unajiona kama malkia au mfalme pale kila aliyekuja kwenye harusi yako anapopambana japo apate picha ya kumbukumbu nawewe.
Na ya tatu huwa ni fungate kama umebahatika kwenda, walioenda fungate wanaelewa ninachosema.
Zaidi ya hapo ladha tamu ya ndoa huanza kupoa taratiiibu, sasa hapa ndipo inapohitajika mwanaume kuonesha uanaume wako katika ndoa.
Ipo hivi, majukumu yako mwanaume katika ndoa ni ya asili na hayatokoma mpaka unafunga kauli. Hapa nazungumzia majukumu ya kutunza familia yako kwa kadri ya uwezo wako bila kuhoji au kutegemea mchango wa mwanamke kwako, mwanamke yeye kwa nafasi yake tu ameshahukumiwa kwa kuwajibika kwako lakini wewe mume ni sharti uoneshe kwa vitendo ili kujenga na kuboresha upendo hata kwa watoto ambao kiasili humwamini mama kwa sababu ndiye wanakuwa naye muda mrefu zaidi yako.
Ni wajibu wako kumuhudumia mkeo na kumpa pesa ambazo pia usijaribu kuhoji anavyozitumia, hata kama na yeye anakipato binafsi, bado nguo zake na viatu vyake ni jukumu lako.
Majukumu ndio kipimo cha uanamume wako nyumbani na watoto watakutambua na kukuheshimu kama ni mwajibikaji wakiuona mkono wako katika makuzi yao, vinginevyo utamlaumu mke kwamba anawaharibu na kuwafundisha vibaya watoto.
Hakuna ndoa isiyo na misukosuko wala usijidanganye kwa kujifananisha na fulani anavyoishi na mwenzie, yao ya ndani huyajui!!
Muhimu na wewe ficha ya kwako ili nao wawaone mfano kwao!
Kuna siku wazee wetu wakikumbuka misukosuko na mitihani waliyoipitia ndo utaona anawaalika ndugu, jamaa na marafiki kusherehekea Jubilee ya miaka kadhaa ya ndoa yao, yaani wanashangaa kuona wamemudu kufika uzeeni licha ya changamoto walizopitia ambazo yamkini ni hizihizi ambazo Leo wewe unaona zinakushinda katika ndoa yako, simama imara watu wajifunze kwako.
Wewe umebahatika malezi ya wazazi wote, ebu fikiria unavyowapa wakati mgumu watoto kwa malezi ya upande mmoja kwa kiburi chako tu cha eti " watoto wangu nawamudu", huwamudu watoto wako kwa sababu huwezi kuwapa malezi ya pande mbili! Jitahidi vumilia taabu kero za mwenzio kwa faida ya watoto wako, hata kwa kinafiki tu maisha yaendelee.
Ebu jaribu fikiri, ni dhambi kubwa saaaaana na ya ajabu ambayo kwako itakuwa ya kwanza kufanyiwa na unaguarantee hutofanyiwa nje ya mahusiano yako haya ya sasa, jibu ni hakuna.
VUA na achana kabisa na joho na kutaka kuhukumu kila jambo, mengine yameze kama yalivyo, mengine yapuuze kama hujaona au kusikia na kisha umlaani shetani na muombe mungu akupe uwezo wa ziada kuyashinda.
Kwenye ndoa kuna chokochoko, kuna maudhi, kuna husda, vijicho, wivu, kuna nongwa, kuna fitna, chuki, kero na yafafayo mengi tu, na bahati nzuri unao uwezo wa kuyashinda yote haya, na ukiona haya yote hayatokei kwenye ndoa yako nakuhakikishia hiyo ni NDOTO sio NDOA halisi, amka haraka usije ukakojoa kitandani mtu mzima!
Silaha zako ni tatu tu, VUMILIA, SAMEHE na SAHAU.