Ndoa na mahusiano ya kimapenzi siyo mambo ya lazima kutekelezwa

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Karibuni nyote wanachama wa jukwaa hili.

Kuna mambo makuu mawili ambayo ningependa kuzungumza pamoja nanyi wanachama wa jukwaa hili yahusuyo Ndoa & Mahusiano ya kimapenzi.

Jambo la msingi hasa ambalo ningependa kuligusia ni kuhusu ukosefu wa fikra mpya na zilizo bora ndani ya jamii kupelekea kutasfiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi katika njia isiyo sahihi.

Ukosefu wa fikra bora umepelekea kuathiri jamii kwa kiwango kikubwa mpaka kushindwa kutambua yapi hasa ni mahitaji ya lazima ya mtu hapa duniani na yapi hasa sio mahitaji ya msingi ya mtu hapa duniani?

Jamii kwa kiwango kikubwa imeathirika haijalishi ni jamii ya watu wa somi au laa, kwa asilimia kubwa jamii imeshindwa kutofautisha kama ndoa na mahusiano ya kimapenzi ni mahitaji ya msingi ya watu hapa duniani?

Imefika hatua jamii imeweka ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama ni mahitaji ya msingi ya watu hapa duniani jambo ambalo si tafsiri sahihi.

Jamii kwa kiwango kikubwa imekwisha amishana kuwa iwe kijana au mtu mzima ni lazima awe na mwenza wake [ mpenzi wake/ mahusiano ya kimapenzi ] au mke/mme [ ndoa ].

Kwa asilimia kubwa fikra za wanajamii zimeathirika na kushindwa kung'amua kuwa ndoa na mahusiano ya kimapenzi si mahitaji ya msingi kwa mtu hivyo si lazima mtu awe nayo. Kwa kuwa haya leti athari zozote zile asipo kuwa nayo tofauti na mahitaji hasa ya msingi mtu anayo stahili kupata kama vile makazi/malazi, mavazi na chakula.

Elimu yetu kwa kiwango kikubwa imeshindwa kukomboa fikra mbovu hizi za wana jamii na mawazo yao hasi kuhusu mahitaji ya msingi ya mtu mpaka kufika hatua ya kuweka ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama ni mahitaji ya msingi ambayo ni lazima ya tekelezwe.

Jamii kwa kiwango kikubwa imeshindwa kung'amua kuwa kuna aina mbalimbali za watu wenye tabia tofauti tofauti walio wazunguka katika maisha yao mfano:
i. Alpha
ii. Beta
iii. Sigma

Hapa jamii imeshindwa kung'amua kuwa utofauti huu wa aina za watu una zalisha makundi tofauti tofauti ya watu yenye fikra, tabia na malengo tofauti tofauti kitu ambacho jamii zingine katika hayo makundi matatu, ndoa na mahusiano ya kimapenzi si mambo ya maana kwao ni miongoni mwa mambo ya hovyo yasiyo na maana kwao.

Wanafizikia/Wana sayansi Isaac Newton, Nicola Tesla na mimi mleta mada ni miongoni mwa watu tunao wakilisha kundi la watu tunao tafsiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke sio mahitaji ya msingi kwetu na wala sio mambo ya lazima kutimiza maana ni miongoni mwa mambo ya hovyo yanayo ondoa umakini katika mambo ya msingi katika maisha yetu na yana changia kwa kiwango kikubwa upotevu wa muda katika vitu visivyo vya msingi na visivyo na maana.

Elimu kuhusu mahitaji ya msingi kwa mtu mashuleni inapaswa kutiliwa mkazo haswa ili kuondoa hizi kasumba mbaya ndani ya jamii za kulazimisha na kutafsiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama mahitaji ya msingi kwa mtu huu ni upotoshaji usio paswa kuvumilika.
81L8YUl4tWS.jpg
zamaninin-cok-otesinde-bir-mucit-olan-nikola-11825896_osd.jpg
nikola-tesla-life-story-scaled.jpg
 
Kwa asilimia kubwa fikra za wanajamii zimeathirika na kushindwa kung'amua kuwa ndoa na mahusiano ya kimapenzi si mahitaji ya msingi kwa mtu hivyo si lazima mtu awe nayo. Kwa kuwa haya leti athari zozote zile asipo kuwa nayo tofauti na mahitaji hasa ya msingi mtu anayo stahili kupata kama vile makazi/malazi, mavazi na chakula
Umri wako tafadhali
 
Umri wako tafadhali
Anaweza kuwa ana zaidi ya miaka 30.Kuna mambo yanawasukuma kuwa na mawazo hayo:
-Kukata tamaa maishani ya kupata mwenza.
-Kutokuwa na chanzo cha kudumu kimapato.
-Kuwa na muathiriko wa kisaikolojia hasa kutokana na aliyowahi kushuhudia,kupigwa matukio au hata kupiga mtu tukio halafu akaathirika mwenyewe.
-Matatizo ya kiafya kimwili kama vile kutokuwa au kupungua nguvu za kiume/kike.
-Kutengwa na jamii ambapo huchukia jamii yote na kujichukia mwenyewe
Siweki nukta kuna sababu nyingi zaidi
 
Yote hayo si sahihi, jaribu kusoma sifa za makundi mbalimbali ya watu wenda utaweza kung'amua baadhi ya mambo kuhusu mimi.
i, Sigma,
ii, Alpha na
iii, Beta .
 
Mm ninaweza kukubaliana na ww linapo kuja kwenye suala la mahusiano hasa haya ya kiholela ya bila ndoa, hayo mapenzi bila ndoa hata mungu aliye tuumba ameyapiga vita maana yameshababisha uzinzi wa kiholela na madhara ya huo uzinzi wa kiholela tunayaona mitaani.
Umesababisha single mother, umejaza watoto wasio kuwa na baba mitaani,umefukarisha watu sio vijana wala wazee.
Lakini ndoa ni kitu cha razima maana ni kitu kilicho amuliwa na mungu.
 
Karibuni nyote wanachama wa jukwaa hili.

Kuna mambo makuu mawili ambayo ningependa kuzungumza pamoja nanyi wanachama wa jukwaa hili yahusuyo Ndoa & Mahusiano ya kimapenzi.

Jambo la msingi hasa ambalo ningependa kuligusia ni kuhusu ukosefu wa fikra mpya na zilizo bora ndani ya jamii kupelekea kutasfiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi katika njia isiyo sahihi.

Ukosefu wa fikra bora umepelekea kuathiri jamii kwa kiwango kikubwa mpaka kushindwa kutambua yapi hasa ni mahitaji ya lazima ya mtu hapa duniani na yapi hasa sio mahitaji ya msingi ya mtu hapa duniani?

Jamii kwa kiwango kikubwa imeathirika haijalishi ni jamii ya watu wa somi au laa, kwa asilimia kubwa jamii imeshindwa kutofautisha kama ndoa na mahusiano ya kimapenzi ni mahitaji ya msingi ya watu hapa duniani?

Imefika hatua jamii imeweka ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama ni mahitaji ya msingi ya watu hapa duniani jambo ambalo si tafsiri sahihi.

Jamii kwa kiwango kikubwa imekwisha amishana kuwa iwe kijana au mtu mzima ni lazima awe na mwenza wake [ mpenzi wake/ mahusiano ya kimapenzi ] au mke/mme [ ndoa ].

Kwa asilimia kubwa fikra za wanajamii zimeathirika na kushindwa kung'amua kuwa ndoa na mahusiano ya kimapenzi si mahitaji ya msingi kwa mtu hivyo si lazima mtu awe nayo. Kwa kuwa haya leti athari zozote zile asipo kuwa nayo tofauti na mahitaji hasa ya msingi mtu anayo stahili kupata kama vile makazi/malazi, mavazi na chakula.

Elimu yetu kwa kiwango kikubwa imeshindwa kukomboa fikra mbovu hizi za wana jamii na mawazo yao hasi kuhusu mahitaji ya msingi ya mtu mpaka kufika hatua ya kuweka ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama ni mahitaji ya msingi ambayo ni lazima ya tekelezwe.

Jamii kwa kiwango kikubwa imeshindwa kung'amua kuwa kuna aina mbalimbali za watu wenye tabia tofauti tofauti walio wazunguka katika maisha yao mfano:
i. Alpha
ii. Beta
iii. Sigma

Hapa jamii imeshindwa kung'amua kuwa utofauti huu wa aina za watu una zalisha makundi tofauti tofauti ya watu yenye fikra, tabia na malengo tofauti tofauti kitu ambacho jamii zingine katika hayo makundi matatu, ndoa na mahusiano ya kimapenzi si mambo ya maana kwao ni miongoni mwa mambo ya hovyo yasiyo na maana kwao.

Wanafizikia/Wana sayansi Isaac Newton, Nicola Tesla na mimi mleta mada ni miongoni mwa watu tunao wakilisha kundi la watu tunao tafsiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke sio mahitaji ya msingi kwetu na wala sio mambo ya lazima kutimiza maana ni miongoni mwa mambo ya hovyo yanayo ondoa umakini katika mambo ya msingi katika maisha yetu na yana changia kwa kiwango kikubwa upotevu wa muda katika vitu visivyo vya msingi na visivyo na maana.

Elimu kuhusu mahitaji ya msingi kwa mtu mashuleni inapaswa kutiliwa mkazo haswa ili kuondoa hizi kasumba mbaya ndani ya jamii za kulazimisha na kutafsiri ndoa na mahusiano ya kimapenzi kama mahitaji ya msingi kwa mtu huu ni upotoshaji usio paswa kuvumilika.View attachment 2453199View attachment 2453200View attachment 2453201

Watakuja kukubishia lakini ndio ukweli wenyewe...... kila kitu ni chema kama kimekaa sehemu yake, kwa kazi yake na kimeibeba maana yake

Yapo mambo mengi ya msingi tumetumwa kuyafanya duniani kwa sifa na utukufu wa Mungu

Huwa najiuliza tunaodhani ndoa ni lazima ndoa zao zimebeba sifa gani

Na wale tunaodhani kuwa na watoto ni lazima tulishawahi kujiuliza tuliowazaa ni kina nani?

Tumwombe Mungu sana ASIWAJU tunaotamani ndoa na watoto tuwazae kina Esta, kina Isaka, kina Rebeka, kina Dorcas..... na Mungu atuepushe na kina Kaini, kina Onani, kina Reuben
 
Anaweza kuwa ana zaidi ya miaka 30.Kuna mambo yanawasukuma kuwa na mawazo hayo:
-Kukata tamaa maishani ya kupata mwenza.
-Kutokuwa na chanzo cha kudumu kimapato.
-Kuwa na muathiriko wa kisaikolojia hasa kutokana na aliyowahi kushuhudia,kupigwa matukio au hata kupiga mtu tukio halafu akaathirika mwenyewe.
-Matatizo ya kiafya kimwili kama vile kutokuwa au kupungua nguvu za kiume/kike.
-Kutengwa na jamii ambapo huchukia jamii yote na kujichukia mwenyewe
Siweki nukta kuna sababu nyingi zaidi
Mi nadhani wewe umemaliza Kila kitu.
 
Back
Top Bottom