Ndoa mbaya sana ikiwa...

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Wakuu ndoa mbaya sana ikiwa...

A) Umemtokea demu tu ambaye hukuwa na malengo naye bali kutoa genye alafu mwisho wa siku unampa mimba unaona uoe. Jamani utapata tabu sanaa labda salama yake urudi kwa Mungu wako.

Ndoa mbaya sana ikiwa..

B) Umeamua baada ya kuoa ndo utulie lakini bado unapiga michepuko Mingi ukitegemea ukioa mke wako mmoja utatulia. Aiseee utakuja kuona ndoa chungu na utachepuka zaidi kwa sababu kama hukutosheka ni michepuko mitano utatosheka vipi na mke huyo mmoja?

Aisee ndoa mbaya sana ikiwa

C) Unaanza kuishi kindoa na mwanamke hata kabla ya ndoa kwa kisingizio cha kumpima tabia eti. Halafu unampima na kumchunguza mtu ambae anajua hasa kwamba hapa nachunguzwa, atafanya mistake kweli na kuonyesha makucha? Hapo full heshima yaani,weka ndani sasa unaota mvi wakati umezaliwa wakati wa kifo cha nyerere.

Jamani ndoaa mbaya saaana ikiwa..

D) Mapenzi yako kwake unayetaka kumuoa yamejengwa na uzuri wa maumbile peke yake alafu tabia zero. Aiseee utajuta sana maana uzuri utaisha na atabaki na tabia ile ile(mbaya) ambayo mwanzo hukuona ina msingi kwa sababu ya uzuri wake,sasa hapo itakuwa mke uzuri ule wa mwanzo umepungua na wewe wazuri unazidi kuwaona,hapo itakuwa KUISHA+TABIA MBOVU=majuto.na utajuta mpaka uvimbiwe.

Ndoa mbaya sana ikiwaa....

E) Unajua kwamba unayetaka kumuoa ana tabia mbovu alafu ukaweka kisingizio cha eti utambadilisha,my friend utakuja kulia sana unajua kwa nini?

Hivi kama alishindwa kubadilika kabla ya ndoa na kama unavyojua wanawake wanafanya kila njia waolewe,sasa mwanamke na kigezo kwamba akibadilika ataolewa lakini bado hajabadilika,vipi akiipata hiyo ndoa tayari utamshawishi na nini mpaka abadilike tabia? Yaani hapo ndo utakapokuwa unafungia vifungo vya shati kwenye gari mana nyumba haikaliki.

Ndoa ni mbaayaa saana ikiwaa...

F) Hautotumia umakini kuchagua mke mtarajiwa,yaani ukiwa wewe ni mtu wa kuchunguza hospitali gani nzuri ukatibiwe ambayo inatoa huduma nzuri na ukawa unaulizia kwa watu wenye uelewa juu ya hospitali nzuri AU ukitaka kwenda kusoma chuo fulani unakuwa unafanya tafiti ya kutosha na ufundishaji wao ukoje hicho chuoo..alafu kwenye mke hutaki kufanya tafiti wakati ndo ambae utaishi nae milele basi juaa bado unamchukulia mke simple simple na unaichukulis ndoa simple sana na ukiingia lazma ujute tuu,unachaguaje kienyeji namna hiyo?

Zingatieni sana mnaotaka kuoa,ndoa sio lele mama kwamba uingie wakati bado akili bado ya kipuuzi,bado unatumia njia za kipuuzi kupata mke utakoma broo na mtazidi kulia kuhusu ndoa kama hamtochukua hatua.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Mkuu umejuaje yote hayo ? Au una ndoa mbaya?? nakubali mengi uliyoandika though
Mkuu binadamu tupo tofauti sana,mm ni kijana mdogo ambae nina uwezo mkubwa wa kuyahandle mambo ya ndoa hata huwezi amini.

Ingawa nini sasa mkuu?
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Kwani ukiona miyeyusho si unatoka tu .... ila kiukweli ndoa ni mtihan

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi nafaidi ndoa na rafk zangu wengi wanakimbia ndoa kwa sababu mbali mbali ikiwemo niliyotaja hapo juu.

Ukiwa na maarifa mengi husiti kuchagua mke popote pale hata humu kuna watu wanafaa kuwa wake.(nitaandaa uzi special za wanawake wa humu ambao wanaweza kukaa kwenye ndoa zao)
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Ukitaka kuwa Fundi mzuri wa magari nunua bovu, mkuu utakuwa Na ndoa moja mbovu saaaanaa maana umechambua poa sanaaa
Ahahahha,hata ukiishi jirani na magari mabovu lazima utakuwa fundi mzuri tuu.

Nimeishi na washkaji wengi ambao walikurupuka kuoa alafu wakawa hawako siriaz katika ndoa zao na kuchagua mke,matokeo yake siri za ndoa wanazitoa mpaka kwetu kwa sababu ni watu wachepukaji hata kabla ya ndoa hivyo kwao ni rahisi kukupa stori za ndani na mkewe,tunajifunza mengi kupitia washkaji ntaani,alafu tunatafuta ufumbuzi.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Naam mkuu,uzi wangu hakuna ambapo nimekataa kwamba ndoa sio makubaliano,manake mpaka kufikia ndoa basi mumekubaliana.

Kinachojadiliwa ni kwa yule ambaye hakubaliani na tabia mbovu za mwenzie alafu mwanzo hakutizama.

Ila kama wote mmekubaliana kuishi kivyenu vyenu sio kesi,lakini mtu asilalamike mara ooh mke kanifanyia hivi na vileeee,sie hatumoooo
urongo mtupu..ndoa ni makubaliano yenu wawili bwana we!..ndoa yako haiwezi fanana na ndoa ya mwenzako
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,190
2,000
Sana yani.

Ndoa inaanzia kwenye akili alafu yanafata matamanio.lakini ukianza kuchagua mke kwa kutumia genyeyenge basi kuangukia pua lazima.
Kweli bwana ndoa inahtaji umakini tangia mwanzo wa mahusiano wengi hu ignore vitabia vya mwanzo wa mahusiano wakiamini huko ndoani atabadilika matokeo yake ni majanga. Au mtu anaoa/olewa yet still ana act ka bachelor, mtu haachi uhuni lazima ndoa iwe msalaba walah

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom