Ndoa mbaya sana ikiwa...

Ndoa mbaya sana ikiwa...

Wakuu ndoa mbaya sana ikiwa...

A) Umemtokea demu tu ambaye hukuwa na malengo naye bali kutoa genye alafu mwisho wa siku unampa mimba unaona uoe. Jamani utapata tabu sanaa labda salama yake urudi kwa Mungu wako.

Ndoa mbaya sana ikiwa..

B) Umeamua baada ya kuoa ndo utulie lakini bado unapiga michepuko Mingi ukitegemea ukioa mke wako mmoja utatulia. Aiseee utakuja kuona ndoa chungu na utachepuka zaidi kwa sababu kama hukutosheka ni michepuko mitano utatosheka vipi na mke huyo mmoja?

Aisee ndoa mbaya sana ikiwa

C) Unaanza kuishi kindoa na mwanamke hata kabla ya ndoa kwa kisingizio cha kumpima tabia eti. Halafu unampima na kumchunguza mtu ambae anajua hasa kwamba hapa nachunguzwa, atafanya mistake kweli na kuonyesha makucha? Hapo full heshima yaani,weka ndani sasa unaota mvi wakati umezaliwa wakati wa kifo cha nyerere.

Jamani ndoaa mbaya saaana ikiwa..

D) Mapenzi yako kwake unayetaka kumuoa yamejengwa na uzuri wa maumbile peke yake alafu tabia zero. Aiseee utajuta sana maana uzuri utaisha na atabaki na tabia ile ile(mbaya) ambayo mwanzo hukuona ina msingi kwa sababu ya uzuri wake,sasa hapo itakuwa mke uzuri ule wa mwanzo umepungua na wewe wazuri unazidi kuwaona,hapo itakuwa KUISHA+TABIA MBOVU=majuto.na utajuta mpaka uvimbiwe.

Ndoa mbaya sana ikiwaa....

E) Unajua kwamba unayetaka kumuoa ana tabia mbovu alafu ukaweka kisingizio cha eti utambadilisha,my friend utakuja kulia sana unajua kwa nini?

Hivi kama alishindwa kubadilika kabla ya ndoa na kama unavyojua wanawake wanafanya kila njia waolewe,sasa mwanamke na kigezo kwamba akibadilika ataolewa lakini bado hajabadilika,vipi akiipata hiyo ndoa tayari utamshawishi na nini mpaka abadilike tabia? Yaani hapo ndo utakapokuwa unafungia vifungo vya shati kwenye gari mana nyumba haikaliki.

Ndoa ni mbaayaa saana ikiwaa...

F) Hautotumia umakini kuchagua mke mtarajiwa,yaani ukiwa wewe ni mtu wa kuchunguza hospitali gani nzuri ukatibiwe ambayo inatoa huduma nzuri na ukawa unaulizia kwa watu wenye uelewa juu ya hospitali nzuri AU ukitaka kwenda kusoma chuo fulani unakuwa unafanya tafiti ya kutosha na ufundishaji wao ukoje hicho chuoo..alafu kwenye mke hutaki kufanya tafiti wakati ndo ambae utaishi nae milele basi juaa bado unamchukulia mke simple simple na unaichukulis ndoa simple sana na ukiingia lazma ujute tuu,unachaguaje kienyeji namna hiyo?

Zingatieni sana mnaotaka kuoa,ndoa sio lele mama kwamba uingie wakati bado akili bado ya kipuuzi,bado unatumia njia za kipuuzi kupata mke utakoma broo na mtazidi kulia kuhusu ndoa kama hamtochukua hatua.
G) Ndoa mbaya sana ikiwa unachagua mke kwa kuangalia wo wo wo na ikiwa unachagua mume Kwa kuangalia muonekano kama urefu kifua nk..
 
Hhhhhh kweli mkuuu alafu mwisho wa siku wowowo unaliona kawaida kwa sababu unapenda sama wowowo basi utapepesa macho kuangalia wowowowo za mitaani na hapo ndo utamuona mkeo wa kawaida,na utaanza kuwaza kumwaga na uweke ndani wa zaidi yake.

Utajikuta hutuliii tuu,kila mwanamke wako weweee
G) Ndoa mbaya sana ikiwa unachagua mke kwa kuangalia wo wo wo na ikiwa unachagua mume Kwa kuangalia muonekano kama urefu kifua nk..
 
Leo tumegusia uoande wa wanaume wanayoyakosea.

Siku nyingine tutagusia upande wa wanawake wanayoyakosea.
Haina maana kwamba ndo tumemaliza hapana mamy.nso wanawake wana nafasi yao ila tu tumewalenga wanaume kwa sababu wao ndo wana nafasi kubwa kuchagua.
Kwa hiyo ndoa inamuhitaji mwanamke bora na mwanaume yoyote?
 
Haya
 
Kwa hiyo ndoa inamuhitaji mwanamke bora na mwanaume yoyote?
Hapana sio kweli. Ndoa inahitaji mwanamke imara na mwanaume anayejitambua nafasi yake kama baba. Na kingine ambacho wengi tumesahau ni kwamba ndoa inahitaji kujishusha. Ikitokea wote wawili mkaweza kujishusha basi hiyo ndoa itakuwa na amani na upendo. Ikishindikana kwa wote wawili basi mmoja ajishushe. Tofauti na hapo hakuna ndoa kwani mafahali wawili hawakai zizi moja dada Hornet..
 
Ni kweli kabisa
Ndoa ni watu wawili
Waamue kwa pamoja,
Wajitambue
Wasikilizane na waheshimiane
Hapo utaiona furaha ya ndoa,

Unaweza ukachagua vyovyote uprndavyo kwa matamanio ya macho na mkaingia mkaelewana mambo yatanyooka tu.
 
Kikubwa ni kwa wawili kutambua kuwa nyumba ni ofisi ya mama na wewe baba ni mwajiriwa katika ofisi hiyo. Usimuingilie katika mambo yanayohusu vitu kama mlo usafi na budget. Mpe matumizi yake na mpe uhuru wa kuamua afanye nini. Kama mke ana akili na busara utafurahia. Usisahau kabla ya ndoa ni muhimu kujua mwenzako akikasirika anakuaje na utamtuliza vipi. Japo kwa upande wangu sijawahi kumuona mke wangu amekasirika..
 
Hongera sana mkuu.
Mimi mara ya mwisho kumkuta amekasirika sikumbuki,zaidi namkera mimi tu na namuomba msamaha yanaisha.

Ukipata mwanamke poa burudani kabisa

Back
Top Bottom