Ndoa mbaya sana ikiwa...

Hapana sio kweli. Ndoa inahitaji mwanamke imara na mwanaume anayejitambua nafasi yake kama baba. Na kingine ambacho wengi tumesahau ni kwamba ndoa inahitaji kujishusha. Ikitokea wote wawili mkaweza kujishusha basi hiyo ndoa itakuwa na amani na upendo. Ikishindikana kwa wote wawili basi mmoja ajishushe. Tofauti na hapo hakuna ndoa kwani mafahali wawili hawakai zizi moja dada Hornet..
Naam kabisa mkuu
 
Wakuu ndoa mbaya sana ikiwa...

A) Umemtokea demu tu ambaye hukuwa na malengo naye bali kutoa genye alafu mwisho wa siku unampa mimba unaona uoe. Jamani utapata tabu sanaa labda salama yake urudi kwa Mungu wako.

Ndoa mbaya sana ikiwa..

B) Umeamua baada ya kuoa ndo utulie lakini bado unapiga michepuko Mingi ukitegemea ukioa mke wako mmoja utatulia. Aiseee utakuja kuona ndoa chungu na utachepuka zaidi kwa sababu kama hukutosheka ni michepuko mitano utatosheka vipi na mke huyo mmoja?

Aisee ndoa mbaya sana ikiwa

C) Unaanza kuishi kindoa na mwanamke hata kabla ya ndoa kwa kisingizio cha kumpima tabia eti. Halafu unampima na kumchunguza mtu ambae anajua hasa kwamba hapa nachunguzwa, atafanya mistake kweli na kuonyesha makucha? Hapo full heshima yaani,weka ndani sasa unaota mvi wakati umezaliwa wakati wa kifo cha nyerere.

Jamani ndoaa mbaya saaana ikiwa..

D) Mapenzi yako kwake unayetaka kumuoa yamejengwa na uzuri wa maumbile peke yake alafu tabia zero. Aiseee utajuta sana maana uzuri utaisha na atabaki na tabia ile ile(mbaya) ambayo mwanzo hukuona ina msingi kwa sababu ya uzuri wake,sasa hapo itakuwa mke uzuri ule wa mwanzo umepungua na wewe wazuri unazidi kuwaona,hapo itakuwa KUISHA+TABIA MBOVU=majuto.na utajuta mpaka uvimbiwe.

Ndoa mbaya sana ikiwaa....

E) Unajua kwamba unayetaka kumuoa ana tabia mbovu alafu ukaweka kisingizio cha eti utambadilisha,my friend utakuja kulia sana unajua kwa nini?

Hivi kama alishindwa kubadilika kabla ya ndoa na kama unavyojua wanawake wanafanya kila njia waolewe,sasa mwanamke na kigezo kwamba akibadilika ataolewa lakini bado hajabadilika,vipi akiipata hiyo ndoa tayari utamshawishi na nini mpaka abadilike tabia? Yaani hapo ndo utakapokuwa unafungia vifungo vya shati kwenye gari mana nyumba haikaliki.

Ndoa ni mbaayaa saana ikiwaa...

F) Hautotumia umakini kuchagua mke mtarajiwa,yaani ukiwa wewe ni mtu wa kuchunguza hospitali gani nzuri ukatibiwe ambayo inatoa huduma nzuri na ukawa unaulizia kwa watu wenye uelewa juu ya hospitali nzuri AU ukitaka kwenda kusoma chuo fulani unakuwa unafanya tafiti ya kutosha na ufundishaji wao ukoje hicho chuoo..alafu kwenye mke hutaki kufanya tafiti wakati ndo ambae utaishi nae milele basi juaa bado unamchukulia mke simple simple na unaichukulis ndoa simple sana na ukiingia lazma ujute tuu,unachaguaje kienyeji namna hiyo?

Zingatieni sana mnaotaka kuoa,ndoa sio lele mama kwamba uingie wakati bado akili bado ya kipuuzi,bado unatumia njia za kipuuzi kupata mke utakoma broo na mtazidi kulia kuhusu ndoa kama hamtochukua hatua.
Mke Mzuri Utoka Kwa Mungu, Muombe sana Mungu akupe Mke Mzuri Maana Kumchunguza Mwanadamu ni Kazi tena Kazi KweliKweli !!
 
Na juhudi zako pia.

We muombe mungu pesa wee alafu ukeshe chumbani na maombi yako usiende kutafuta mtaani kama utatoboa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Kweli Juhudi yako pia inahitajika. Zingatia pia, Pesa na Mapenzi ni Vitu viliwi tofauti, pesa inatafutwa Ila uwezi kutafuta mapenzi.
urongo mtupu..ndoa ni makubaliano yenu wawili bwana we!..ndoa yako haiwezi fanana na ndoa ya mwenzako😊
Kwan ndoa ni nn? Ndoa ni ileile maisha ndiyo na tabia ya wanandoa ndiyo yanatofautiana. Tunapozungumzia ndoa tunazungumzia mahusiano halali ya kimapenzi ya watu wawili yani Mke na Mume. Kwaiyo msingi wa ndoa yoyote ile ni mapenzi.
 
Huo ni mfano hakuna tofauti ya pesa na mapenzi katika ndoa.

Nimegusia kuhusu juhudi ya kutafuta mke mwema ni kama juhudi ya kutafuta pesa.

Na wala sijazungumzia juhudi ya kutafuta mapenzi ili upendwe mkuu.huwezi kutafuta mapenzi.

Ila kumtafuta mtu mwema inataka juhudi kama juhudi ya kutafuta pesa,huwezi kutembea barabarani ukasema unatafuta pesa zinazodondoka bila shaka utapata vitu ambavyo havina thamani kama vile mavi,makaratasi na peni zilizokwisha tu.

Ila ukitumia juhudi haswa kwa usahihi ukatafuta pesa basi utapata pesa japo kwa uchache wake.

Ndo hvyo hvyo usipoyumia njia nzuri na umakini kutafuta mwenza mwema basi utaokota makapuku tu mkuu hutompata mwenye thamani kama pesa.

Hapo suala la mapenzi linakuja baadae
Ni Kweli Juhudi yako pia inahitajika. Zingatia pia, Pesa na Mapenzi ni Vitu viliwi tofauti, pesa inatafutwa Ila uwezi kutafuta mapenzi.

Kwan ndoa ni nn? Ndoa ni ileile maisha ndiyo na tabia ya wanandoa ndiyo yanatofautiana. Tunapozungumzia ndoa tunazungumzia mahusiano halali ya kimapenzi ya watu wawili yani Mke na Mume. Kwaiyo msingi wa ndoa yoyote ile ni mapenzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom