ndoa inapovunjika aibu ni kwa nani?

Aibu ya nani kivipi, weka bayana swali lako, Wanandoa ni binadamu wawili waliokulia kwenye mazingira mawili tofauti, kila mtu na makuzi yake, wameshindwa kuishi pamoja kutokana na tofauti zao wazijuazo wenyewe, sasa hapo aibu inatoka wapi, kwani kuolewa au kuishi na mtu ni lazima hata kama tabia zake na mwenendo wake umenishinda? ning'ang'anie tu eti kwa kuogopa aibu itakuwa ya nani.
 
hakuna aibu.....

kuacha/kuachwa/kuachana ni jambo la kawaida......

but ukifikiria kiundani aibu ni ya yule anayeona ni jambo la ajabu mke na mume kuachana wakati hakuona ajabu wawili kuoana (maana hii inainvolve wawili kuvuliana nguo)
 
lazima watafurahi kama binti yao
alikuwa anaonewa...

lakini bado hujanijibu swali langu
kwanini wazazi waone aibu???
na hapo juu umeelezea hasira si
aibu...

hakuna maswala ya kuonewa, nyie si ndo mnasema ulitaka uolewe ili uondoe mkosi? Ukishaolewa unaanzisha visa kibao!!!
 
hakuna aibu
kila chenye mwanzo chini ya jua lazima kiwe na mwisho,na ndoa is not an exception
mwisho wa ndoa waweza kuwa kifo au kuachana
sasa aibu in'toka wapi hapo?
mbon kawaida tu .......
 
nakubaliana sana na wanaosema kuwa aibu ipo kwa yule anaesababisha ndoa kuvunjika.
 
Ndoa haivunjiki sema wanandoa wanatengana.
Ndoa ni tendo na ukisha tenda halifutiki kwa hiyo hamna aibu.
Labda kama unauliza kama wana ndoa wametengana aibu ni kwa nani?
 
hakuna maswala ya kuonewa, nyie si ndo mnasema ulitaka uolewe ili uondoe mkosi? Ukishaolewa unaanzisha visa kibao!!!

hahahahahah lol
haya bwana ngoja nikuachie hiyo

lakini nijibu swali langu
"kwa nini wazazi waone aibu"???
asante na usiku mwema
 
Aibu itatokana na sababu iliyopelekea ndoa kuvunjika na hasa itakuwa kwa yule aliyesababisha kuvunjika - issues hapa ni 1. uchawi aka limbwata; 2. uaminifu zero ikiwemo kumegwa au kumega nje ya ndoa.
 
Ndoa sio ndoano....ni makubaliano ya pande mbili ...mtu mume na mtu mke. Kama ilivyo kwa mambo mengine ndoa nayo ina makubaliano ambayo yanafaa kuheshimiwa ili ndoa iweze kudumu...ikiwa upande mmoja umeshindwa kuheshimu makubaliano mliojiwekea na jitihada za kumrudisha ikashindwa kuzaa matunda si aibu kujiengua!....wakati mwingine kuachana tafsiri yake si udhaifu km wengi tunavyoweza kudhani ila ni namna ya kuonesha kua umekomaa vya kutosha kufanya maamuzi magumu!
 
Ndoa sio ndoano....ni makubaliano ya pande mbili ...mtu mume na mtu mke. Kama ilivyo kwa mambo mengine ndoa nayo ina makubaliano ambayo yanafaa kuheshimiwa ili ndoa iweze kudumu...ikiwa upande mmoja umeshindwa kuheshimu makubaliano mliojiwekea na jitihada za kumrudisha ikashindwa kuzaa matunda si aibu kujiengua!....wakati mwingine kuachana tafsiri yake si udhaifu km wengi tunavyoweza kudhani ila ni namna ya kuonesha kua umekomaa vya kutosha kufanya maamuzi magumu![/QUO]

Kwa hiyo ulioa/kuolewa ukiwa hujakomaa then ukakomaa ukiwa ndoani au ndio hizo ndoa za kufuata mkumbo?Ndoa sio sehemu ya majaribio!
 
Ndoa sio ndoano....ni makubaliano ya pande mbili ...mtu mume na mtu mke. Kama ilivyo kwa mambo mengine ndoa nayo ina makubaliano ambayo yanafaa kuheshimiwa ili ndoa iweze kudumu...ikiwa upande mmoja umeshindwa kuheshimu makubaliano mliojiwekea na jitihada za kumrudisha ikashindwa kuzaa matunda si aibu kujiengua!....wakati mwingine kuachana tafsiri yake si udhaifu km wengi tunavyoweza kudhani ila ni namna ya kuonesha kua umekomaa vya kutosha kufanya maamuzi magumu!

mkuu nimekukubali, upo sawa. Hasa ukizingatia kua mke/mume huwezi kumjua vizuri hadi mfunge ndoa hatakama uchumba una miaka 10, ukishaoa ndo utajua SIDE B ya mwenzio.
 
hahahahahah lol
haya bwana ngoja nikuachie hiyo

lakini nijibu swali langu
"kwa nini wazazi waone aibu"???
asante na usiku mwema

lazima wazazi waone aibu hasa ukizingatia kuwa wenyewe wazazi wanakua hawaelewi kwa nini umeachika maana nia yako ilikua pete ya ndoa kanisani. Hata kama wakijua majirani si wanaona gafla upo single nyumbani kwenu na juzi walikuaga na bonge la send off, na uchumba ulidumu miaka mi5 ndoa miezi miwili!!! mwenyewe jirani hapa kaachika juzi lakini habari mtaa mzima kuwa kaachika na wanaishi mkoani. Mi naona mnajiletea mikosi na hamtoi mkosi, we afrodenz ukishaachika ujue itakua ngumu sana kupata mume tofauti na mumeo, dakika mbili tu anaoa tena.
 
Kinyoba sina hakika na imani yako ila Wakristu husema "nitakua mme/mke wako hadi kifo kitakapotutenganisha"...vije km mmoja atakua mzigo kwa mwenzake? Nionavyo kutokana na uaminifu na mahusiano mengi kua ya mashaka itafika mahali hii statement ya kujifunga hadi kifo ijibadili na kuwa " nitakua mume/mke wako halali na muaminifu kwenye ndoa hadi pale nitakapokua/utakapokua mzigo kwangu/kwako ila kwa kwa habari ya ugonjwa na matatizo mengine kiafya nitasimama pamoja nawe hadi kifo!....huo ni mtazamo wangu na haupaswi kuwa kanuni kwa wanaofikiri vinginevyo!
 
Back
Top Bottom