ndoa inapovunjika aibu ni kwa nani?

kinyoba

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
1,267
718
wakuu nawasilisha hili maana ndoa za siku hizi imekua kama fashion, ndoa inadumu miezi michache tu wanandoa wanachana. Hasa kati ya mwanamke na mwanaume. Utasikia ameachika kwa mumewe au ameachana na mkewe!
 
Aibu ya nini tu labda??

aibu ipo, kuna wazazi wa pande zote mbili, kuna wanandoa kwa ujumla wao, na individual kwa maana ya mwanamke na mwanaume. Kwa mfano unauliza habari kuhusu mtu, moja ya sifa unayopata ni ameachika(mwanamke) au ameacha(mwanaume)
 
Ndoa kuvunjika ni jambo la kawaida sana. Kila mara mtu atembeaye nje ya ndoa ake maana yake ni kwamba ndoa yake imeshavunjika. Sasa aibu ya nini hapo wakati ni jambo la kawaida kabisa....
 
aibu kwa wazazi wao na jamii iliyowalea kwa kushindwa kuwaandaa kuishi maisha ya ndoa.
 
aibu ipo, kuna wazazi wa pande zote mbili, kuna wanandoa kwa ujumla wao, na individual kwa maana ya mwanamke na mwanaume. Kwa mfano unauliza habari kuhusu mtu, moja ya sifa unayopata ni ameachika(mwanamke) au ameacha(mwanaume)

Kwa nini wazazi waone aibu?
 
Inategemea na sababu ya ndoa kuvunjika.ila mara nyingi ni kwa wote.kama mna watoto ndo inakuwa mbaya zaidi kwa mtazamo wangu
 
binti ameachika halafu karudi kuishi na wazazi, unadhani wazazi watafurahi?

lazima watafurahi kama binti yao
alikuwa anaonewa...

lakini bado hujanijibu swali langu
kwanini wazazi waone aibu???
na hapo juu umeelezea hasira si
aibu...
 
Back
Top Bottom