ndoa inanishinda nipen mawazo yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ndoa inanishinda nipen mawazo yenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by miss nora, Apr 12, 2011.

 1. miss nora

  miss nora Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari wana jamii forms, napenda mawazo yenu na michango mnayotoa humu,,mimi ni mama wa mtoto mmoja nina miaka 23
  naomba msaada jamn,nina mume ambaye nipo nae kwa miaka sita na nimezaa nae mtoto mmoja, kiukweli huyu kaka ni malaya cna kutokana na tabia yake hapo nyuma kwani aliowa wake 2 kabla yangu na wakaachan akidai hawafai walikuwa na tabia mbaya

  ameshanisaliti mara nyingi sana mpk sasa na ushahidi nikapata lkn aliomba msamaha coz nlikuwa bdo nampenda tukaendelea na maisha,,

  hivi sasa kanikataza kushika simu yake yaani tunagombana kila siku, kuna siku nilikuta kamtumia binti fulani pesa kwa njia ya m-pesa nilipomuuliza ni nani tuligombana cna akadai ni mama wa mtoto wake,, lakini nilichunguza nikakuta ni uongo kwani namba ya mzazni mwenzake naijua na hawezi kumuita mpenzi kwani huyo mzazi mwenzake keshaolewa,,

  nilimpigia huyo binti nikamuuliza yeye ni nani lakini matokeo yake alinitukana akaniambia sijaona wanaume nini???akasema yy hakumtongoza mume wangu bli mume wangu ndiye aliyemtongoza kiukweli niliumia cna nikalia mpaka nikachoka,,nikataka nirudi kwetu lakini nikaenda kwa mama mmoja rafiki wa familia akanishauri nisiondoke nikae nivumilie,,
  kwa upande mwingine huyu mume wangu ananijali na familia kwa ujumla lakiniatatizo ni umalaya,,
  natamani hata nitoke jne coz na mm najijua ni mzuri bado nafikiria nahitaji mawazo yako.
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hapo ukitoka nje ya ndoa watakulaumu.................???? Sitetei uzinzi lakini kwa hali hiyoo mmmmhhh inakuwa ngumu mwaya.......

  Ila ushauri wangu ni kwamba VUMILIA mpaka mwisho wa dahali mwanamke hakati tamaa wala kuchoka....................POLE DEAR.............

  SIRUHUSU MASWALI KWA HILI
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndoa ya miaka 6 na wewe una 23 tu?Hamna muda maalumu wa kuoa au kuolewa ila ni kama huyo kaka alitumia u-innocent wako kusiko.Kama hiyo ni tabia yake kuacha itakua ngumu.Kama uko tayari kumvumilia jaribu..kama umechoka ongea nae..wahusishe hata wazee ikibidi ila mwisho wa siku asipoelekea omba talaka.Pole sana!
   
 4. T

  TwendeSasa Senior Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dada angu Mwömbe Mungu wako na atakusaidia, kuwa na upendo wa dhat na ucjarbu kufuatilia mambo yake kabisa..kaa naye kwa ajili ya matunzo y mtoto na wala ucpende kum8liza vitu au mambo ya tabia yake..Nbm4ni Mungu atakusaidia
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umesema mmeo ni malaya,tena alikupata akiwa ameacha wake wengine!
  Wewe alikupata katika mazingira gani?
  Katika mazingira hayo ulikubali kuolewa nae ukijua wewe ni tofauti na alio waacha?

  Joke:Hivi miss ni dada mwenye sifa zipi?
  Advice:
  Ongea na Mungu,kama ndio mume aliye kupangia na hukuiba mme wa mtu basi ata mrekebisha!!
  Kama uliiba mme wa mtu,tegemea adhabu kama/zaidi ya hiyo ukiendelea kukaa nae
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Pole sana dada upo kwenye ndoa kwa mda wa miaka 6 kwa maana hiyo uliolewa chini ya miaka kumi na nane yaani uliolewa ukiwa na 17yrs na uhakika wkt unaolewa ulikuwa hujitambui na ulikuwa huelewi ni nn maana ya maisha sasa unafunzwa na dunia. Imradi uliamua kuubeba mzigo wa hao wanawake 2 walio pita huna budi kuvumilia mpaka mwisho.
   
 7. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,442
  Trophy Points: 280
  Kama hii thread ingekuwa imeanzishwa na mwanaume...... wanachama wake kwa waume humu tungeshauri 'mbwage, kimbia kimeo ect'.

  Hii vumilia vumilia tunayoshauriana is so relative, mwanaume malaya unamvumiliaje?

  Za kuambiwa changanya na zako bidada, una umri mdogo sana kufa kwa maradhi ya kuletewa.
   
 8. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  pole na matatizo vumilia dada huwa tunabeba magunia yote ya michele, pumba, maharage etc kwa ajili ya watoto wetu hamna kingine.Muombe Mungu ambadilishe.:bored:
   
 9. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mmmh Pole mpz inaelekea uliolewa bado ukiwa mdogo sana na misuko suko ya ndoa /mahusiano kwako ilikuwa bado. Kama jamaa alishaoa na kuacha mara mbili ww unanini cha ziada asikuache?rember if he cheated on her he will cheat on you.
  :Umaskini ni tatizo kubwa ktk maisha yenu na inatufanya kutae sehem tu kwa manyanyasho na misuko suko mingi,nadhani jamaa anauwezo kifedha ndio mana unashindwa uamue nini,anything thats hutrs u its not urs,jipange sawasawa fanya kazi,biahsara kwa bidii kuna mtoto na familia kwa ujumla inakutegema,huna haja ya kupigiwa watu na kuuliza kama wana uhusiano na mumeo au la utaishia kupata pressure buree na cancer ya mdomo maana wengine hawajafunza hata chembe,jaribu pia kuongea na mumeo mueleze jinsi unavyompenda,ni ngum kujifnya humuoni lkn sometimes it beta to let it go,kuwa busy na kazi na Mungu pia,jihusishe na jamii na kushirikiana na wenzio,achana na kutoka nje uo ni ushamba na ulimbukeni unaofanywa na wasiojua wajibu wao ktk jamii
   
 10. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kamwaga mboga na ww mwaga ugali na ww tafuta ch nje ....mi niko available kuwa w nje.aki2ma pesa kw m-pesa kw kimada chake na ww unamlipa kw kuni2mia pesa kw m-pesa.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Umemsoma hapo juu anasema kuwa bado anampenda sana.

  Kutenganisha ndoa za watu jamani ni dhambi hata Mungu hapendi.
   
 12. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Du unasemw anakujali @hapo umeniache hoi ,yaelekea uapnde wa pili(wewe)Ikawa ni tatizo zaid katka mkasa hu ,kama kweli uanayoyaeleza ni ukweli huko kujali anaopokujali una maana ganni! au ulifuat mali !
   
 13. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Leo una point...ni kweli jamaa alichukulia kuwa mdogo (23-6=17), ili aweze kuwa na heshima tu ya ndoa lakini aendeleze tabia zake, kwa sababu alijua huwezi kumwambia kitu.
  Ushauri ni hakikisha sasa unachukua hatua, lazima ajue kwamba ENOUGH is ENOUGH, simamia ndoa yako, washirikishe wazazi na washenga..(ikiwa mlifunga ndoa halali)
   
 14. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,442
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ya kulazimisha mapenzi gani hayo. Raha ya mapenzi kupendwa na kuenziwa na anayejiheshimu.

  Ukigundua mkeo malaya utaendelea kumpenda tu kunusuru ndoa isivunjike? Mpende mwenzio kama unavyojipenda wewe so mpe ushauri unaostahili kwani mwisho wa siku mtu halazimishwi kutekeleza kila analoshauriwa.
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  huyu Mungu 2namchosha sasa, akae tu aombe Mungu akiletewa maradhi ndani yeye aombee tu tu...wewe eti akae nae tu kwa ajili ya ma2nzo ya mtoto asiulize mambo yake? kama ndio hivyo hakuna ndoa hapo...mdada huyo mwanaume ni wa kumfungia kibwebwe aisee, tena funga kabla jua halijazama mkalishe chini uongee nae na masharti kibao huku ukiandaa plan b in case akienda kinyume na makubalaino,hii kukaa kwa ajili ya watoto itatumaliza wengi wenye mawazo hayo, ukae na mtu tu kwa ajili ya mtoto uletewe na magonjwa ndani?
   
 16. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  wale wanaosema avumilie: Hivi mpaka apelekewe kile kirusi chenye herufi tatu ndio mtamshauri atimue?

  Ushauri wangu:
  -achana na hiyo ndoa haraka iwezekanavyo, as per ur story, hiyo njemba tayari ina historia mbovu so hauwezi kumbadilisha wewe. Ulikosea in the first approach lakini hauwezi kurejesha kalenda nyuma.
  -Hiyo njemba kuna weakness amegundua kwako na anaiabyuzi hiyo weakness. think abt it!
  -Achana na sjui anajali jamaa zako sijui anakupeleka shopping blah blah blah, as long as hajali hisia zako, He is useless. kilichowakutanisha ni hisia na sio kutembelea shangazi na mjomba.
  -am sure hapo ulipo umeanza kunyonyoka manywele kwa stress, sasa whats the point?

  NB: kujali hisia za mwenza ni muhimu hata kama unacheat.

  -----------------------THE END-------------------
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie mwenzio pia nimeshachoka kuckia hizi vumilia vumilia, tunauana hivi hivi kwa ajili ya huyu "vumilia"...nadhani wanaosema hiyo vumilia hawajui ni kiac gani mwanaume wa hivi anavyokosesha amani ndani ya nyumba, leo utamshika na hili kesho na lile hakuna amani ni mawazo na presha za kuletea magonjwa....wanawake hebu tuamke jamani..
   
 18. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kasema anampenda na anajali familia we unataka kuwatenganisha nimeshindwa kuelewa mtu anayekujali anakuwaje tena malaya.

   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Dah tangu nikufahamu sijawahi kukuona umeandika bonge la point kama hili. Leo umeamkaje lakini?? Unakunywa kinywaji gani?? Nidai chupa zaidi ya kumi . Serious....................
   
 20. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sijakuelewa hapa umeshauri atapelekewa virusi,hapo kwenye red mbona umeharibu au ukifanya bila kukamatwa hamna virusi.   
Loading...