Ndoa hizi.....we acha tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa hizi.....we acha tu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Jan 2, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mke na Mume Wafumaniana Usiku wa Krissmass
  [​IMG]
  Saturday, December 26, 2009 11:48 AM
  NDOA moja ambayo bado ilikuwa ni miongoni mwa ndoa changa hapa jijini Dar es Salaam, imejikuta ikiingia doa baada ya wanandoa hao kila mmoja kumfumania mwenzake katika moja ya sehemu za starehe maeneo ya Kibamba jijini Dar es Salaam.Tukio hilo la kuvutia na la kusisimua lililowaacha watu wengi hoi lilitokea katika baa iliyotambulika kwa jina la Mwanzo Pub, majira ya saa moja za usiku huko maeneo ya Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Wanandoa hao ambao walishikwa na bumbuwazi na kila mmoja akishindwa kumuadhibu mwenzake kwa wakati huo, walijikuta sikukuu hiyo ya kuzaliwa kwa mwokozi Bwana Yesu Kristu ikiingia dosari baada ya kufumaniana.

  Katika tukio hilo, mume aliyegoma kutaja jina lake, aliingia mapema katika baa hiyo akiwa na nyumba ndogo wake na alishangaa kumuona mkewe naye akiingia kwenye baa hiyo na mpenzi wake.

  Mwanaume huyo alimuangalia mke wake akingia na mpenzi wake huyo na aliendelea kujibanza kwenye kona moja nzuri akiangalia mienendo ya mkewe bila ya mkewe kutambua kuwa mumewe yupo kwenye baa hiyo hiyo.

  Mwanaume huyo mwishowe uvumilivu ulimshinda alivyoona mali zake zikitawaliwa na mwanaume mwingine. Aliamua kwenda moja kwa moja kwenye meza aliyokaa mke wake huyo.

  Awali mkewe alipomuona mumewe alijaribu kukimbia lakini mumewe aliwahi kumdaka na kuanza kumuuliza huyo mwanaume aliyekaa nae ni nani huku mkewe akikosa majibu.

  Katika purukushani hiyo, mwanaume huyo alitaka kumpiga mke wake lakini hali ilibadilika ghafla wakati hawara yake naye alipokwenda kwenye meza hiyo na kumuuliza huyo mwanamke aliyekuwa akimgombeza ni nani yake.

  Alimjibu “ Niache na wewe hayakuhusu nenda ukakae kule huyu ni mke wangu”

  Ndipo dada yule nae alishangaa na kumuuliza kuwa mke wako? Na yeye alianza varangati kwa mume huyo mkware kwa kuanza kumkunja na kumwambia ”kumbe una mke halafu mimi ulikuwa unaniongopea siku zote, we mwanaume kumbe Malaya ulikuwa unaniahidi ndoa kila kukicha kumbe muongo".

  Katika hali ya kushangaza mke aliyefumaniwa nae alianza kumkunja ghafla mwanamke huyo na kuanza kumpa kichapo na kumwambia “ kumbe wewe ndie uliyekuwa unaiibia mume wangu ndio maana mume wangu alibadilika kitabia.

  Hali iliyofanya kuwe na zogo na makelele katika baa hiyo kiasi cha kufanya walinda ulinzi katika baa hiyo “mabaunsa kuwashika wanandoa hao na kuwaweka pembeni huku kila mmoja akiwa hana la kufanya kwa mwenzake.

  Hawara aliyekuwa na mume wa mwanamke huyo alianza kumshambulia tena mwanaume huyo kuwa umenijengea nyumba na kuniahidi ndoa kumbe ni muongo kuanzia leo sitaki uje nyumbani kwangu endelea na mke wako, huku baba huyo akiwa hana la kusema.

  Katika juhudi za Nifahamishe kutaka kujua undani wa ndoa hiyo ilibaini kuwa wanandoa hao toka waoane, katika moja ya makanisa Katoliki nchini walikuwa na muda wa miaka miwili, na mke aliyefumaniwa aliiambia Nifahamishe.com kuwa wanaishi maeneo ya Kinondoni Mkwajuni.

  Alisema kuwa mume wake Desemba 24 usiku alipata simu ya dharura na alimuaga akisema kuwa anahitajika mkoani Dodoma kikazi na angerudi Desemba 26 nyumbani.
   
 2. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kujua kama mumeo au mkeo anajirusha mtaani basi omba tu mbadilisheni simu zenu za mkononi kwa wiki moja tu na muwe na tabia ya kufanya hivyo wiki moja kwa kila mwezi uone atakavyong'aka. Au mwambie mchuchu wako akupe password zake za email accounts zake zote ili wote muwe na uhuru wa kusoma kila kinachoingia na kutoka hapo kijasho chembamba kitawatoka wote kwa kudai mambo mengine inabidi yabaki private. Hizi ndoa za siku hizi! We acha tu ni WIZI MTUPU!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  An interesting series of lack of trustworthness, matrimonial integrity, and family boundaries!...

  Nawashangaa wenye imani kwamba kwenye ndoa ni mahala pazuuri, na ni raha tupu!
  Lakini, siri kubwa katika ndoa ni moja tu-UAMINIFU!
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hapo patamu na ningoma droo na ndio ndoa za siku hizi hizo watuwanaingia bila kujiaandaa
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  dah, jamaa alijenga na nyumba kabisa, alikuwa anapewa nini huko?
   
 6. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa uzoefu wangu, hiki si kisa cha kweli, ni cha kutunga. lakini maudui yake ni halisi, tuwe waaminifu kwa ndoa zetu. wanawake wana nafasi kubwa sana ya kutatua tatizo la uaminifu wakiacha tamaa ya vitu na kujifunga unyenyekevu na heshima kwa waume zao


  HERI YA MWAKA MPYA
   
 7. bht

  bht JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mapochopocho haaaaa!! lol!!!
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndoa zilikuwa enzi hizo! hakuna ku beep una hakika utamkuta mwenzio hajatumika (not used) na wanakuwepo wapambe kuhakikisha hilo na kama halipo hakuna ndoa hapo!! Tangu utandawazi umeingia kwenye ndoa kwamba bikira sio issue haya ndiyo matokeo yake.

  Umemkuta mwanamke used, utajuaje kama ki mahusiano wamemaliza agenda zao? Unaingia kichwa kichwa matokeo yake wenzio wanaliendeleza wewe hujui. Ndipo hapo waswahili mtaani ukipita wananyoosheana vidole "babu jinga inama ufikiri mali yako inaliwa". Inauma, tuwe waaminifu jamani.
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  anakijua yeye, wewe huko unakokimbilia kila siku unapewa nini?????
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe kuwa huyo anakijua mwenyewe. hata mie kuna wakati nafikiria kumjengea nyumba dada mmoja kwa mapenzi makuwa ya heshima na uaminifu anayonipa. ni moyo tu ndio unaotaka!!!!!!!!!! wala si kutokana na ushawishi wake!!
   
 11. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hao mnaowaona ndio wanyenyekevu basi ndo balaa usisikie yani. Wanatafuta tuu hapo wakisha pata utakama kumjua jua.
   
 12. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siwezi kubisha kwa tahadhari kama hii, na kwa kweli silubaliani kabisa na mtu kujengea mashangingi nyumba, hasa yale ambayo unaona kabisa kuwa si lolote wala chochote bali machunaji tu.

  lakini jamani nyumba kitu gani mbele ya utu? mtu akupende, akufariji, akujali wakati mwingi hata akuzalie mtto, halafu eti nyumba iwe kuuuuuuuubwa mpaka ishangaze watu?

  tujali utu jamani, mapenzi tuayapenda lakini utu twauona ghali!
   
 13. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujapenda wewe!!!!,ukifanyiwa mambo na ukapenda na uwezo wa kujenga unao,unajenga tu!!!,wangapi wamejengea wenzi wao?,wako wengi saaana!!!
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhhh.......
   
 15. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufanyiwa mambo kama yapi Sugar?
   
 16. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusema kweli, mimi naendelea kujenga moja huko kisukulu kwa ajili ya mpenzi wangu
   
 17. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mfano kubebwa kupelekwa washroom kuoga!!!
   
 18. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe na wewe hujui kazi!!!!!!!hayo ya kubebwa mbona ni vijimambo tu!!!!!!!!

  kuna mambo wewe, mie najenga nyumb unadhani kwa ajili ya kubebwa? yako mambo penny we acha tu, kunako yenyewe hata mzee hugeuka kijana!!!!!!
   
 19. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2014
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi shemegi ulipoteleaga wapi?
   
 20. REALITY

  REALITY JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2014
  Joined: Jul 2, 2014
  Messages: 2,536
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  UMBEYA nothing here ni pumba
   
Loading...