Ndo nimeua ama?

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Habarini wataalamu jana nimefanya format mashine yangu ya home dell nimeweka window XP serv pack
3 baada ya kumaliza kuformat ikapoteza sauti,na pia picha zikawa na scratch sana na font zimekuwa kubwa sana.
Naomba msaada wa mwenye hizo software za sauti na VGA na zakurekebisha hizo font ziwe kawaida.
Nashukuru sana wandugu.
 
Mara nyingi dell huwa zina cd driver, Baada ya kufomat unatakiwa uweke hiyo cd ili appearance yake iwe kama zamani kisha unaweka cd ya sound max kwa ajili ya sauti usiwe na hofu computer yako bado iko sawa tu ni cd zinazohitajika
 
Ina INTEL INSIDE? Kama ndiyo basi unaweza kutumia wizard.
 
Sound driver idownload from dell support
fonts na display-nenda control panel halafu kwenye display badilisha resolution
VGA drivers-nenda ktk dell support udownload inayoendana na machine yako
 
Mh hii ni kawaida huwa inatokea ukiinstal window ya serv park 1 mpaka serv park 3. Hapo tatizo sio software bali ni driver za sauti na display. Kuna cd inacontain drivers zote za window(universal drivers) kama ungeipata hiyo ingekusaidia kurudisha sauti na pia resolution ya display ingerudi kuwa ya kawaida. Au kama unaona itashindikana kupata hiyo cd waweza google 'sound drivers' na 'display drivers' for dell alafu udownload hayo mafolder, alafu ukishapata 'sound drivers' na 'display driver' for dell kuna steps kadhaa za kufanya mpaka sauti na diplay irudi, ukiipata niPM endapo utahitaji msaada. Ila huu ni uzoef wangu tu, kuwa na subira tusubir maoni ya wengine
 
Back
Top Bottom