Ndo nimemaliza C-section ya 6, nimechoka akili na mwili. Halafu kuna Wanasiasa kwa mwezi wanakula 11 M na bado wanajiongezea mshahara 40%

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,052
71,331
Kwa Msioelewa, C-section ni Upasuaji wa kumzalisha Mama (kutoa mtoto/watoto) Kwa Kizazi kwa njia ya upasuaji.

Toka Nilipolala usiku wa kuamkia Jana, mpaka Leo sijalala yaani 24 hours bila kulala.

Kuweni na Huruma Enyi Viongozi, Hivi mtu toka saa Mbili usiku uko Chumba Cha Upasuaji , ukitumia Akili yote, Taaluma yote, kuhakikisha kwamba Mama na Mtoto wanatoka salama.

Hata Chakula nilokula Jana saa 12 jion, tumboni hakipo.

Tunafanya kazi kwelikweli, tunajituma mnoo bila kulala ,bila kupoteza muda, Akili na Mwili vyote vinachoka.

Hivi kweli kazi tunayoifanya inaendana na Mshahara Huu unaokatwa na unakatika haswaa ?. Na utu tuposho tudogodogo hivi?

Eehh Mwenyezi Mungu uendelee Kuwatia Nguvu Madaktari, Wauguzi na Wafanya kazi wote wa Kada hiii, Mungu Baba, kazi hiii ilikua yako, ila kwakua uko juu mbinguni, uliamua kutuchagua tuitendee hapa Duniani, Endelea kutulinda, tuepushie Magonjwa, linda familia zetu, Muda huuu Wake na watoto Wetu tumewaacha Majumbani, Usalama wao uko mikononi mwao.

Lakini Baba Mungu, embu nena na watawala wako, uwape Moyo wa kujinyenyekeza, wakati wanapanga Kujiongeza mishahara minono ya mamilioni, Baba Mungu wakumbuke kua Kuna watu wanapambana usiku kucha kwaajili ya Watanzania.

Screenshot_20230917_060652~2.jpg
 
Pole sana mtumishi. Wanakuja business owners na kaka yao Mpwanyungu kukwambia nenda kajiajiri…

Wanakuja ndugu zao viongozi wasio wahadilifu kukwambia ukipata upenyo hamisha mikasi na gloves nyumbani.

Mie jobless sina usemi zaidi ya pole.
 
Hongera. Muhimu jua tu duniani hakuna haki Wala usawa. Hivi vyote utakutana navyo siku ya mwisho wa maisha yako hapa duniani.
Mkuu Ahsante, Kwa kweli tunafanya kwakua ni wito wa rohoni.

Wanasiasa hawajali ,, Sasa itokee bahati mbaya upate MD au PD au vyote Kwa pamoja , utaitwa ujieleze mpaka Kwa Waziri husika, yaan wee ndo utageuzwa mpira Kila Mmoja atahitaji akupige .. yote tu sababu wanasiasa Hawajali.
 
Ujue Tanzania watu ambao hawajasoma ndiyo hupewa kipaumbele kwenye mambo ya msingi na mawazo yao huchukuliwa km reference muhimu ktk kuleta maendeleo kwa nchi. Rejea vigezo vya kuwapata viongozi wa Tanzania kwa mjibu wa katiba, ni kichef chefu tupu na hawataki vibadilike hata kwa dawa kwa sababu Watanzania wengi hupenda kusikiliza mambo ya hovyohovyo kutoka kwa watu wajinga. Wewe uliyesoma ukiongea point utaskia wanasema huo siyo utamaduni wetu, mara mitaala yetu inazalisha vijana wa hovyo. Muda mwingine hao gumbaru utawaskia humo mjengoni wakijisfia kuwa hawajasoma lakini Wana pesa.
 
Kwa Msioelewa, C-section ni Upasuaji wa
Kumzalisha Mama ( kutoa mtoto/watoto) Kwa Kizazi kwa njia ya upasuaji.

Toka Nilipolala usiku wa kuamkia Jana, mpaka Leo sijalala yaani 24 hours bila kulala.

Kuweni na Huruma Enyi Viongozi, Hivi mtu toka saa Mbili usiku uko Chumba Cha Upasuaji , ukitumia Akili yote, Taaluma yote, kuhakikisha kwamba Mama na Mtoto wanatoka salama.

Hata Chakula nilokula Jana saa 12 jion, tumboni hakipo .

Tunafanya kazi kwelikweli, tunajituma mnoo bila kulala ,bila kupoteza muda, Akili na Mwili vyote vinachoka.

Hivi kweli kazi tunayoifanya inaendana na Mshahara Huu unaokatwa na unakatika haswaa ?. Na utu tuposho tudogodogo hivi?.

Eehh Mwenyezi Mungu uendelee Kuwatia Nguvu Madaktari, Wauguzi na Wafanya kazi wote wa Kada hiii, Mungu Baba, kazi hiii ilikua yako, ila kwakua uko juu mbinguni, uliamua kutuchagua tuitendee hapa Duniani, Endelea kutulinda, tuepushie Magonjwa , Linda familia zetu, Muda huuu Wake na watoto Wetu tumewaacha Majumbani, Usalama wao uko mikononi mwao.

Lakini Baba Mungu, embu nena na watawala wako, uwape Moyo wa kujinyenyekeza, wakati wanapanga Kujiongeza mishahara minono ya mamilioni, Baba Mungu wakumbuke kua Kuna watu wanapambana usiku kucha kwaajili ya Watanzania.

View attachment 2751793
Mi nitakuja kuwa rais, maslahi ya Medical Doctor yatakuwa hivi;
1. Bima ya afya-maisha,
2. Kusomeshewa watoto-international mpaka chuo kikuu,
3. Mshahara minimum mil 12,
4. Makazi-bure,
5. Usafiri-unakopeshwa gari bila riba na unapewa mafuta
6. ….
 
Hapa bongo office assistant wa TRA ambae ana cheti tu cha form 4 ya division 4 ya 32 na akasoma office assistant VETA miezi 3 ana mshahara mkubwa kuliko Graduate wa Chuo Kikuu mwenye Shahada ya Udaktari kutoka Muhas ama hata nje ya nchi alieajiriwa halmashauri ama tamisemi.

Kuna fani ukisoma hapa Bongo na ukaajiriwa nazo hapa Bongo uko disadvantaged by default.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom