Si kwamba namtetea, ila Mwigulu Nchemba anafaa katika wizara hii ya fedha
Tukumbuke alishawahi kuwa katika wizara hii na katika awamu yao hiyo ndio wizara ya fedha ilikuja na mifumo madhubuti ambayo kwa kiasi kikubwa ina control matumizi ya fedha za umma
Kubwa ninalokumbuka na alilofanya vizuri kipindi hicho ni mfumo wa ulipaji mishahara kwa watumishi wa umma "Lawson" (Sina hakika na spelling)
Huu mfumo kwa kiasi kikubwa ndio unaosaidia watumishi kupata mshahara kwa wakati na kwa pamoja kuliko ilivyokuwa zamani
Pia kwa kiasi kikubwa huu mfumo umedhibiti maafisa watumishi kulipa mshahara "account" fake na kwa kiasi kikubwa hakuna namna mtumishi wa umma atakosa mshahara kama yupo kwenye mfumo endapo yupo kazini Kama ilivyokuwa zamani
Pamoja na "ulimbukeni" wake aliouonyesha kipindi cha Magufuri, ila bado ni mtu makini pale anapokuwa na watu sahihi
Binafsi naamini alikuwa hivyo alivyo kwasababu ya kutaka kuendelea kubaki madarakani maana ndio aina ya Boss aliyekuwa nae
Bila kujipendekeza na kujifanya hazimo kulikuwa hamna namna ya kuendelea kula
Tumpe muda tuone Kama "sifa" zitaendelea ndio tumseme
Mtu ambaye naona ni "incompetent" mwanzo mwisho ni Jaffo
Huyu bwana ni Mzee wa makelele sijawahi ona utendaji wake tangu aanze kujulikana. Naamini huyu wanamstili tu lakini hana anachofanya