Ndiyo kateuliwa lakini hapendwi na wengi

Ndiyo kateuliwa lakini hapendwi na wengi

Vichekesho vingine vya CCM , Mwizi Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa fedha , CCM na mama yenu mna utani sana na hii na watanzania .
 

Attachments

  • Screenshot_20210217-123842.png
    Screenshot_20210217-123842.png
    37.6 KB · Views: 7
Huyo ni Waziri ambaye hafai kabisa sijui kwanini amemuweka tena kwanza yuko arrogant sana hana sifa ya uongozi siku hizi ni anaona hii nchi kama vile yeye ana hati miliki.
 
Si kwamba namtetea, ila Mwigulu Nchemba anafaa katika wizara hii ya fedha

Tukumbuke alishawahi kuwa katika wizara hii na katika awamu yao hiyo ndio wizara ya fedha ilikuja na mifumo madhubuti ambayo kwa kiasi kikubwa ina control matumizi ya fedha za umma

Kubwa ninalokumbuka na alilofanya vizuri kipindi hicho ni mfumo wa ulipaji mishahara kwa watumishi wa umma "Lawson" (Sina hakika na spelling)

Huu mfumo kwa kiasi kikubwa ndio unaosaidia watumishi kupata mshahara kwa wakati na kwa pamoja kuliko ilivyokuwa zamani

Pia kwa kiasi kikubwa huu mfumo umedhibiti maafisa watumishi kulipa mshahara "account" fake na kwa kiasi kikubwa hakuna namna mtumishi wa umma atakosa mshahara kama yupo kwenye mfumo endapo yupo kazini Kama ilivyokuwa zamani

Pamoja na "ulimbukeni" wake aliouonyesha kipindi cha Magufuri, ila bado ni mtu makini pale anapokuwa na watu sahihi

Binafsi naamini alikuwa hivyo alivyo kwasababu ya kutaka kuendelea kubaki madarakani maana ndio aina ya Boss aliyekuwa nae

Bila kujipendekeza na kujifanya hazimo kulikuwa hamna namna ya kuendelea kula

Tumpe muda tuone Kama "sifa" zitaendelea ndio tumseme

Mtu ambaye naona ni "incompetent" mwanzo mwisho ni Jaffo

Huyu bwana ni Mzee wa makelele sijawahi ona utendaji wake tangu aanze kujulikana. Naamini huyu wanamstili tu lakini hana anachofanya
 
Mwigulu Nchemba Doctor of Philosophy. Upo vizuri mwana. Nakukubali Sana. Naona JF imepooza Sana. Au watu wa Waganga njaa hawakupata nafasi huko?
 
Back
Top Bottom