Ndio, wewe ni ombaomba

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,085
Reaction score
165,855
Baada ya mazoea ya wiki kadhaa tu nikamsikia akiniambia "Babe sina salio, naomba nitumie Tsh 25000 nijiunge na kifurushi cha mwezi". Nikamwambia poa.

Siku chache baadae nikamsikia, "Nimepanga kwenda saloon kwa chichi nikasuke, naomba Tshs 60,000 nikanunue nywele.

Nikamwambia cool "Anything for you my dear.

Baadae kidogo kama wiki hivi nikamsikia "Babe nataka weekend ijayo twende tukale pizza, lakini nakuomba nitumie Tshs 35,000 naenda na marafiki zangu Dinner.

Nikasema poa, Hata hivyo nimepanga kukutumia kamzigo ka zawadi nzuri, nitazituma hizo fedha na huo mzigo."

Nikamtumia, alivyopata tu akanitext na kuniuliza; "Mzigo gani huu umenitumia wa nguo zilizotumika, au sio wangu?"

MIMI: Ni mzigo wako, nimekutumia nguo na viatu vilivyotumika tulivikusanya kwa ajili ya kuwapa omba omba.

YEYE: Kwanini umenitumia mimi? Kwahiyo mimi ni omba omba

MIMI: Wewe ni ombaomba my dear. Omba omba pekee ndio hua wanaomba pesa wanapokutana na mtu kwa mara ya kwanza !!!

Hatufanyi ujinga, tuta-win vipi economic freedom katika uchumi huu mgumu kwa aina hii ya wanawake? hana ushauri, hakutii moyo kutafuta, anawaza kukugeuza kuwa sponsor wake tu...No way!

My brothers we never taught how to be diplomatic when it comes to our hard earning money
 
Siombagi pesa kutoka kwa mwanaume, kama nimemzoea nitamueleza issues ninazopitia katika maisha. Anaweza kunipa ushauri hilo si haba wengine wanatoa pesa hili pia si dogo.
 
Siombagi pesa kutoka kwa mwanaume, kama nimemzoea nitamueleza issues ninazopitia katika maisha. Anaweza kunipa ushauri hilo si haba wengine wanatoa pesa hili pia si dogo.

Wengine wanangoja birthday yako ndiyo anakununlia zawadi, wengine wanakuambia babe jiandae tunakwenda Easter Mombasa kwa wiki mbili, hili si dogo.

Wengine anatoka kazini tu umeletewa kikuku na mkufu.
 
Malizia story. Mahusiano yaliendelea.

I mean. Alijitambua na kuendelea na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…