Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

ccm hawana hualali wa kutawala sasa hivi wanatumia nguvu za majeshi lakini waelewe kwamba,mwisho wao ni 2015 zaidi ya hapo ni kuliingiza taifa kwenye machafuko kama wataendelea kutumia nguvu ya majeshi
CCM kupitia wazazi wake TANU na ASP ndio walioleta uhuru wa nchi hii na ndio walioifanya Tanzania iwe na muonekano huu. Wengine ni wapiga mayowe tu
 
CCM kupitia wazazi wake TANU na ASP ndio walioleta uhuru wa nchi hii na ndio walioifanya Tanzania iwe na muonekano huu. Wengine ni wapiga mayowe tu
lakini wana TANU wenyewe sasa hivi hawapo waliopo ni wapiga mayowe tu,
 
Hakika nashindwa kuelewa. Ina maana Ndimara hajaelewa dhana ya jeshi kutwaa madaraka pindi wanapoona mambo hayaendi? Kwa nini anashindwa kujifunza yanayotokea QUOTE Misri. Hakika huyu mzee anakoelekea ni kubaya au anafanya kusudi kujitia Mpendwa
Mpendwa Lizaboni, hoja ya ndimara ni kwamba kuitwa jeshi kuzima matakwa ya watanzania ni kosa kubwa NA kuwa anaamini history so sababu ya uwepo wa makeshift ya watanzania. Pia yafaa ujue ya kwamba wanajeshi wetu walio wengi hawaishi kwenye ahera ya rushwa,ufisadi na
Utapanyaji wa Mali na TUNU za taifa hivyo ni waathirika kama wananchi wengine.
Kuwaita kuzuia matakwa ya wananchi si justified Bali waliokoe taifa kuzuia amani, utanangamano na uhuru wetu usituponyoke kama watakavyo watawala wasiojali.
 
Kuogopa kupinduliwa ndio wananchi wanataka. Yaani ile hofu ya kupinduliwa ndio itakuwa salama ya wananchi na itawaweka viongozi more responsible kuliko hivi sasa ambapo watawala na viongozi wanakuwa kama managing directors na owners wa nchi. We need 3 governments. Tuchukulie shirikisho la Afrika Mashariki ambapo mfano Tanzania kuridhia bado serikali ya Tanzania inabaki na autonomy yake na Kenya na yake ila kunakuwa na mambo wanayokubaliana katika shirikisho. Wasitudanganye. Hatudanganyiki. Gharama za uendeshaji kwani wanatoa mifukoni mwao? Mamaaaeh! Sisi wananchi wavuja jasho ndio tutagharimia wao inawahusu nini? Mbona wanapopandisha umeme, mafuta nk hawajadili kwa uchungu huo wa serikali tatu? Mamaaeeh! Inaghadhibisha sana na ni unafiki mtupu. Piga ua garagaza serikali tatu ndio utakuwa mpango mzima acha wabwate ikirudi kwa wananchi tupige kura kisha tumalizie la sivyo hizo mbili ndio wanataka mambo kama ya Misri, Libya, Syria yaje Tanzania, hawajui wimbi la mapinduzi ya kweli huanzaje? Kutokujali mambo ya nyakati na matakwa ya wananchi. Wengi wape. Tumechoka kuburuzwa. Sasa basi!
 
Nia ya ccm hajaiwai kuwa njema ktk mpango mzima wa mchakato wa katiba mpya. wanalowaza wao ni madaraka ambayo katiba iliyopo inayalinda. Hofu yao kubwa ni katiba mpya kuwapunguzia madaraka hayo na kuyarudisha kwa wananchi. Watatumia kila njia kuhakikisha katiba mpya yenye mawazo mapya ya kulijenge taifa ili upya hayapiti.

Hata hivyo kila jambo lina wakati wake...sidhani kama wataweza kurudisha nyuma nguvu ya umma kiasi hicho. Ninaloliona mbele ni machafuko yatakayoletwa na ccm. Haiwezekani wakati bunge la katiba likiendelea Kinana na Nape wanaeneza sumu nje ya bunge ilo na bado serikali hiyo inakubali waendelee tu wakati huo UKAWA wajipange kueleza ya kwao wazuiliwe. Tunakokwenda si pazuri...
 
wwe huna tofauti na mwanafunzi aliefeli form four kwa kupata zero naomba tu nikuombe hv una uhakika tukileta hansard ya bunge yenye hotuba ya rais kikwete tutaona aliposema mkileta serikali tatu jeshi litachukua nchi au umekurupuka kuchukua mwisho wa sentensi? wwe ni mbumbumbu sana tena zero brain kichaa wwe unajua kuropoka tu acha kuwadanganya wananchi wwe M :flypig::flypig::flypig:
 
Kikwete mmechelewa kuliita jeshi - NDIMARA

YA KIKWETE, KARUME NA LUKUVI
Ni ghiliba, woga au uchovu kisiasa?


Na Ndimara Tegambwage

NAANZA kushindwa kuandika mara kwa mara. Kama ulimi unavyokwama ndivyo mkono unavyotetemeka. Hasa juu ya hili la watawala kusingizia jeshi kuwa litapindua serikali pindi nchi ikiwa na utawala wa mfumo wa serikali tatu.

Jeshi? Kutwaa madaraka? Kwa kuwa wananchi wametaka mfumo wa serikali tatu? Kwani jeshi linalinda nani, kama siyo wananchi? Hapana! Haya ni matusi kwa wananchi na jeshi lao.

Hadi sasa kauli hizo zimetolewa na Rais Kikwete, Balozi Ali Karume na hivi majuzi Waziri William Lukuvi. Eti serikali tatu zitakula fedha nyingi kiasi cha kuishiwa na kushindwa kulipa mishahara ya wanajeshi; na hapo wanajeshi watapata sababu ya kupindua serikali.

Woga wa kupinduliwa unatoka wapi? Tusaidiane: Watawala wamepata wapi woga wa kupinduliwa? Tangu lini wamekumbwa na woga huu? Labda ni hisia tu. Hilo laweza kukubalika; lakini hisia zinatokana na nini? Kutokana na maoni ya wananchi kwamba wanataka utawala wa mfumo wa serikali tatu?

Watawala wana maana kwamba majeshi yana uchungu mkubwa na fedha za wananchi/umma pale tu yatakapokosa mishahara na siyo yanapoona watawala wakishiriki au kunyamazia au kupuuza wizi, uporaji na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu (BoT) na Hazina; na ufisadi wa kila aina?

Haya ni matusi kwa jeshi. Niliishaandika hivihivi. Ni matusi pia kwa wananchi.

Sikubaliani na wanaodai kwamba kauli hizo za watawala zinachochea jeshi. Sikubaliani. Hakuna uchochezi wowote. Kuna kejeli. Kuna kebehi. Kuna dharau – kwa jeshi; na hata wananchi ambao ndio walipakodi na waajiri wa majeshi yote.

Angalia jinsi watoa kauli wanavyohema, wanavyoweweseka, wanavyomiminikwa jasho na mishipa kuwanaga usoni na shingoni. Polepole na taratibu, wanachumbia jeshi na kuliingiza katikati ya mjadala wa wananchi wa kuamua jinsi wanavyotaka kujitawala.

Wanahema kana kwamba wameambiwa au wameona "kikosi kinaingia nchini ili kusimika mfumo wa serikali tatu!" Ajabu! Kama kikosi hicho kipo, andishi hili liwe, mara moja, ombi langu rasmi la kuingia jeshini ili nishiriki kuzuia kikosi hicho kuingia nchini.

Lakini kama mfumo wa serikali tatu ni utashi na uamuzi wa wananchi wenyewe - na bado kuna fursa ya kupima hilo kwa njia ya kura ya maoni - majeshi yanakwenda wapi, badala ya kukaa imara kulinda utashi, matakwa na uamuzi wa wananchi?

Uanasiasa wa aina hii – ya kuita jeshi kutwaa madaraka – kwa kutumia mtindo wowote ule wa kejeli au vitisho kwa wananchi; ni hatari kwa usalama wa wananchi na taifa kwa jumla. Ni kupanda mbegu ya woga miongoni mwa wananchi; ingawa pia ni kuamsha hisia za kisiasa ndani ya majeshi; na kudhalilisha jeshi kuwa ni mali ya watu au kikundi fulani katika jamii.

Aidha, uanasiasa wa ngeli hii – ya vitisho na vitimbi – unaonyesha watawala waweza kuita jeshi la nje kukabiliana na jeshi la ndani; iwapo jeshi la ndani litakataa kukubali matakwa ya wachache wanaotaka kulitumia na wanaotaka kuzima matakwa na sauti ya umma. Hili ndilo tatizo la kutawaliwa na wanaoishi kwa mazoea na wachovu wasio na jipya.

Hadi sasa mjadala wa Katiba Mpya katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, umesaidia wote wanaoufuatilia kujua fikra na upeo wa fikra wa watawala.

Hoja moja tu ya serikali mbili au tatu, imewafanya watawala wajiapize, watambe kuwa wao ni wengi katika Bunge la Katiba; watukane mwenyekiti wa Tume ya Katiba, washambulie na kubeza wajumbe wa Tume; na watishie wananchi kwamba “jeshi litapindua serikali.”

Hoja imewafanya warudi haraka kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; yule waliyepuuza, kuua na kuzika alichotamani na kupigania – Azimio la Arusha. Yule ambaye walipuuza miiko yake ya uongozi na maadili – vitu alivyosimamia. Angalia sasa wanaanza kumuimba, kumnukuu na kujiapiza kuwa hawakubali serikali tatu “...alizotuachia Baba wa taifa.”

Mbona watawala hawakumuimba Nyerere wakati wanavunja Azimio la Arusha? Mbona hawakumnukuu Nyerere wakati wanavunja miiko na maadili? Mbona hawakumsifu Nyerere walipokuwa wanauza mali ya umma – viwanda, majumba makubwa na nyumba za serikali? Mbona hawakuogopa jeshi kupindua serikali katikati ya ufujaji wa kiwango hicho?

Hoja ni kuwa na serikali tatu chini ya jina lolote lile – Muungano au Shirikisho; lakini watawala wamechonga ndimi na kupeperusha midomo yao wakidai ndani na nje ya Bunge, kwamba serikali tatu “zitaua Muungano,” na kwamba jeshi litawapindua.

Kinachoonekana machoni mwa watawala na katika kauli zao; ni kwamba hawaamini wanachosema. Wangekuwa wanaamini wasemacho, Zanzibar isingempokonya rais wa Muungano madaraka makubwa anayopewa na Katiba huku yeye na wenzake wakichekelea tu.

Kama kweli watawala wanaogopa serikali yao kupinduliwa na jeshi la wananchi kutokana na kuwa na mfumo wa serikali tatu; wanashindwaje kuelewa kuwa waliishapinduliwa zamani kwa rais kupokonywa mamlaka kadhaa kupitia Katiba ya nchi jirani – Zanzibar?

Walichelewaje kuita jeshi kulinda mamlaka ambayo rais alipewa na wananchi chini ya Katiba? Hakika utawala wa mazonge!

(imechotwa katika mtandao wa: ndimara.tegambwage.facebook.com ya 17 Aprili 2014)

Mtazamo mzuri
 
Dah, sasa ngoma inogile ...nimeipenda hoja ya Jeshi kufanya mapinduzi! ...siyo mtazamo mzuri sana LAKINI nahisi kuanzia hapo patakuwa na kuheshimiana tofauti na sasa dhihaka zimekuwa nyingi sana! Naamini kama Jeshi lingekuwa madarakani ungekuta lukuvi kapelekwa TBC, ITV, DTV, Chan 10 chini ya mtutu wa bunduki KUKANUSHA uchochezi wake wa Jamii...
 
Hivi jeshi linaweza kukubali tembo waendelee kuuliwa na mchanga wa dhahabu kutoroshwa? Hivi jeshi halijui kuwa kuna vigogo wamejilimbikizia mali nje ya nchi na watawala wako kimya? Hivi jeshi halisikii hoja za wajumbe wa bunge la katiba mpya walivyo na uchochezi usio na misingi? Kwamba jeshi halioni maamuzi ya kipuuzi ktk serikali hii (wapi pesa za epa na richmond). Kwamba jeshi halioni upendedeleo wa vyeo serikalini? ....Kwamba halioni...halioni...
 
wwe huna tofauti na mwanafunzi aliefeli form four kwa kupata zero naomba tu nikuombe hv una uhakika tukileta hansard ya bunge yenye hotuba ya rais kikwete tutaona aliposema mkileta serikali tatu jeshi litachukua nchi au umekurupuka kuchukua mwisho wa sentensi? wwe ni mbumbumbu sana tena zero brain kichaa wwe unajua kuropoka tu acha kuwadanganya wananchi wwe M :flypig::flypig::flypig:
Punguza hasira mkuu, mwaga facts atakuelewa tu... humu kuna watu wako kwenye kazi maalum, wengine wanategemewa na watu wao kama spin doctor ... NGUVU ya HOJA tu ndiyo muhimu hapa...
 
Hawajui kwamba bila hata jeshi wataondoka tu madarakani! Aliyemloga Kikwete alikufa siku nyingi sana ndio maana hajitambui...
 
Mkuu hapa umenena, ingawa watahofiwa kuchekwa kwa kuingia gharama lakini...wengine watatakiwa kuwajibika!!!
Ila hatujachelewa..AMANI NI MUHIMU SANA KATIKA NCHI HII..Rais wetu avunje tu hilo Bunge..
Mkuu kuhofia kuchekwa kuna thamani kiasi gani mbele ya Amani ya Watanzania? Kwanini asiichukulie kama experiment iliyofeli? then next time tukaiangalia kwa makini ingredients moja moja kabla kuirudia tena?... Again, kuna manufaa makubwa zaidi ya kuvunja BMK na kusitisha mijadala yote ya katiba ili maisha yaendelee... Gharama za kurejesha amani yetu baada ya kupandikiza mbegu nyingi zenye chuki za Kidini, Ubaguzi wa Rangi, Ukanda, Ukabila, Itikadi za Vyama ni KUBWA mmno na itachukua zaidi ya karne nyingi zijazo...Come-on ...we are better than that...Hakuna haja ya kuwafanania majirani zetu walikopitia...
 
CCM kupitia wazazi wake TANU na ASP ndio walioleta uhuru wa nchi hii na ndio walioifanya Tanzania iwe na muonekano huu. Wengine ni wapiga mayowe tu

Usiishi kwa historia za akina homohabilis,heshimu mawazo ya watanzania.Kama issue ni TANU na ASP kuna haja gani ya kutunga katiba mpya?
 
Amaaaaah! Kumbe jeshi ndilo linalotaka serikali mbili na limemtuma JK alisemee? Mbona jeshi halikanushi wala kuunga mkono kauli za boss wao?
 
wwe huna tofauti na mwanafunzi aliefeli form four kwa kupata zero naomba tu nikuombe hv una uhakika tukileta hansard ya bunge yenye hotuba ya rais kikwete tutaona aliposema mkileta serikali tatu jeshi litachukua nchi au umekurupuka kuchukua mwisho wa sentensi? wwe ni mbumbumbu sana tena zero brain kichaa wwe unajua kuropoka tu acha kuwadanganya wananchi wwe M :flypig::flypig::flypig:

Wewe ndo unajaribu kutudanganya,hatudanganyiki tumechokaaaa.Hivi nyie,tume zote zinazokusanya maoni zinakuja na serikali 3,kwa nini mnapuuza matakwa ya wananchi? "TIME WILL TELL"
 
Hakika nashindwa kuelewa. Ina maana Ndimara hajaelewa dhana ya jeshi kutwaa madaraka pindi wanapoona mambo hayaendi? Kwa nini anashindwa kujifunza yanayotokea kule Misri. Hakika huyu mzee anakoelekea ni kubaya au anafanya kusudi kujitia upofu

kwan sa hv mambo yanaenda? yap hayo? hivi jeshi linashindwa kuingilia wakati nchi iko midomoni mwa mafisadi ccm??
 
Ndimara umenena vyema mkuu, sasa wanatafuta crime kwenye hilo bandiko i guess........... intarahamwe mambo hayaendi sawa wanatafuta wa kufa nae sasa
 
Back
Top Bottom