Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

ndimala we ni kibaka huna hadhi ya kusimama na watu kama jk

changia hoja acha kashfa. Kwani jk ni mungu au malaika? Kwanza unamjua vizuri ndimara au umetoka chooni bila kunawa umeingia jf. Ndimara ni kichwa kuliko unavyodhani au umelewa pijau la pasaka ?m.....o !
 
Wanaoharibu mchakato ni UKAWA ambao wametoka nje ya Bunge

Lizaboni;
Kwa nini ccm mnajitia kichaa? Kila mmoja anajitahidi kujitetea utafikiri mpo mahakamani? Nani kakuambia jitetee? Usijali, ipo siku mtaulizwa au mtaamriwa kujibu mashitaka tu.
Mleta hoja kawaambia kina Kikwete, wamechelewa kuliita jeshi liasi. Jeshi haliasi kwa njia yao hiyo. Amewafungua mimacho yao tu. Na ndivyo ilivyo. Usitutoe nje ya huu mjadala kwani hiyo ndiyo jadi yenu. Mmeambiwa mkajadili Rasimu ya Warioba iliyoboreshwa nasi wananchi, mnaenda kuinanga ati si lolote si chochote. Mnaleta yenu kutoka Lumumba! Kweli kazi ipo
 
Umenena vyema Ndimara.
Umetimiza wajibu wako hata ukipuuzwa ukweli utadhihirika.
 
Hakika nashindwa kuelewa. Ina maana Ndimara hajaelewa dhana ya jeshi kutwaa madaraka pindi wanapoona mambo hayaendi? Kwa nini anashindwa kujifunza yanayotokea kule Misri. Hakika huyu mzee anakoelekea ni kubaya au anafanya kusudi kujitia upofu

na jeshi likichukua madaraka na kumtia kizuizini kikwete mwenyewe? au hajalifikiria hilo?
 
Ndimala we ni kibaka huna hadhi ya kusimama na watu kama JK

JK ndo nani? Hivi wakiambiwa marais wanyoshe mikono na JK nae atanyosha mkono wake?
JK anaogopa hadi majangiri wakubwa eti kisa walimfanyia kampeni ya kuiba urais wa Dk. Slaa?
Kwa hawa polisi jamii wake wanaojiita JWTZ wapiga mizinga msibani wacheza kwaya kwenye sikukuu ndo ameona dili kutishia uma? JK asizani kwamba wananchi hawajui uchafu wake. Ipo siku atasaga meno huyu rais muuza sembe100%%%%%%%%%
 
We ni mzee wa kuburuzwa na umeshalishwa sumu na ccm, pole sana!!
 
Haya maelezo Ndimala ameyatoa wapi? Kwamba ikiwa serikali tatu jeshi litachukua nchi?
Ni vizuri kuisikiliza vyema ile hotuba ili kuzuia upotoshaji. Alichokisema (na ambacho Walioba alikisemapia) ni kwamba Serikali ya Muungano (shirikisho) itasimamia majeshi, polisi usalama wa taifa na wizara zile za muungano. Budget ya shirikisho itatokana na michango kutoka nchi washirika.

Ndiyo maana JK akasema -ikiwa washirika wakikataa kutoa mchango ndiyo itakuwa mwisho wa shirikisho (mf.URUSI/RUSSIA) na pia kutokana na hilo hayo majeshi yanaweza ku take advantage.
 
Jeshi lenyewe lipi hilo lisilokuwa na nidhamu? Kila kukicha linapiga wananchi bila sababu zozote za msingi, au bado ile dhana potofu ya kuwaita Nigerians waje wawafundishe tena bado ipo. Ni aibu kubwa kuwa na rais ambaye alikuwa mwanajeshi na kuwa na jeshi lisilokuwa na nidhamu.
 
BONGE la andiko. Na kwa taarifa, wanajeshi wastaafu wameitwa kwa ajili ya usaili. Hivi vyote ni mipango ya kutaka kutisha watu.

Hhaha, wantaka kuwapa kadi upya za chama au?
mimi najua soon tutakuwa na jeshi lisilo kuwa na MACC na hakika lazima kinuke.
 
Hii JWTZ kwa kauli ya Lukuvi mimi nilitarajia kesho yake tuamuke tukiwa chini ya marshal law! Kumbe hawa JWTZ hawana tofauti na akina Abdulhaman Shimbo (Ref Kauli ya Shimbo wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010)
 
[h=2]Kikwete mmechelewa kuliita jeshi - NDIMARA[/h]
YA KIKWETE, KARUME NA LUKUVI
Ni ghiliba, woga au uchovu kisiasa?


Na Ndimara Tegambwage

NAANZA kushindwa kuandika mara kwa mara. Kama ulimi unavyokwama ndivyo mkono unavyotetemeka. Hasa juu ya hili la watawala kusingizia jeshi kuwa litapindua serikali pindi nchi ikiwa na utawala wa mfumo wa serikali tatu.

Jeshi? Kutwaa madaraka? Kwa kuwa wananchi wametaka mfumo wa serikali tatu? Kwani jeshi linalinda nani, kama siyo wananchi? Hapana! Haya ni matusi kwa wananchi na jeshi lao.

Hadi sasa kauli hizo zimetolewa na Rais Kikwete, Balozi Ali Karume na hivi majuzi Waziri William Lukuvi. Eti serikali tatu zitakula fedha nyingi kiasi cha kuishiwa na kushindwa kulipa mishahara ya wanajeshi; na hapo wanajeshi watapata sababu ya kupindua serikali.

Woga wa kupinduliwa unatoka wapi? Tusaidiane: Watawala wamepata wapi woga wa kupinduliwa? Tangu lini wamekumbwa na woga huu? Labda ni hisia tu. Hilo laweza kukubalika; lakini hisia zinatokana na nini? Kutokana na maoni ya wananchi kwamba wanataka utawala wa mfumo wa serikali tatu?

Watawala wana maana kwamba majeshi yana uchungu mkubwa na fedha za wananchi/umma pale tu yatakapokosa mishahara na siyo yanapoona watawala wakishiriki au kunyamazia au kupuuza wizi, uporaji na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu (BoT) na Hazina; na ufisadi wa kila aina?

Haya ni matusi kwa jeshi. Niliishaandika hivihivi. Ni matusi pia kwa wananchi.

Sikubaliani na wanaodai kwamba kauli hizo za watawala zinachochea jeshi. Sikubaliani. Hakuna uchochezi wowote. Kuna kejeli. Kuna kebehi. Kuna dharau – kwa jeshi; na hata wananchi ambao ndio walipakodi na waajiri wa majeshi yote.

Angalia jinsi watoa kauli wanavyohema, wanavyoweweseka, wanavyomiminikwa jasho na mishipa kuwanaga usoni na shingoni. Polepole na taratibu, wanachumbia jeshi na kuliingiza katikati ya mjadala wa wananchi wa kuamua jinsi wanavyotaka kujitawala.

Wanahema kana kwamba wameambiwa au wameona "kikosi kinaingia nchini ili kusimika mfumo wa serikali tatu!" Ajabu! Kama kikosi hicho kipo, andishi hili liwe, mara moja, ombi langu rasmi la kuingia jeshini ili nishiriki kuzuia kikosi hicho kuingia nchini.

Lakini kama mfumo wa serikali tatu ni utashi na uamuzi wa wananchi wenyewe - na bado kuna fursa ya kupima hilo kwa njia ya kura ya maoni - majeshi yanakwenda wapi, badala ya kukaa imara kulinda utashi, matakwa na uamuzi wa wananchi?

Uanasiasa wa aina hii – ya kuita jeshi kutwaa madaraka – kwa kutumia mtindo wowote ule wa kejeli au vitisho kwa wananchi; ni hatari kwa usalama wa wananchi na taifa kwa jumla. Ni kupanda mbegu ya woga miongoni mwa wananchi; ingawa pia ni kuamsha hisia za kisiasa ndani ya majeshi; na kudhalilisha jeshi kuwa ni mali ya watu au kikundi fulani katika jamii.

Aidha, uanasiasa wa ngeli hii – ya vitisho na vitimbi – unaonyesha watawala waweza kuita jeshi la nje kukabiliana na jeshi la ndani; iwapo jeshi la ndani litakataa kukubali matakwa ya wachache wanaotaka kulitumia na wanaotaka kuzima matakwa na sauti ya umma. Hili ndilo tatizo la kutawaliwa na wanaoishi kwa mazoea na wachovu wasio na jipya.

Hadi sasa mjadala wa Katiba Mpya katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, umesaidia wote wanaoufuatilia kujua fikra na upeo wa fikra wa watawala.

Hoja moja tu ya serikali mbili au tatu, imewafanya watawala wajiapize, watambe kuwa wao ni wengi katika Bunge la Katiba; watukane mwenyekiti wa Tume ya Katiba, washambulie na kubeza wajumbe wa Tume; na watishie wananchi kwamba “jeshi litapindua serikali.”

Hoja imewafanya warudi haraka kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; yule waliyepuuza, kuua na kuzika alichotamani na kupigania – Azimio la Arusha. Yule ambaye walipuuza miiko yake ya uongozi na maadili – vitu alivyosimamia. Angalia sasa wanaanza kumuimba, kumnukuu na kujiapiza kuwa hawakubali serikali tatu “...alizotuachia Baba wa taifa.”

Mbona watawala hawakumuimba Nyerere wakati wanavunja Azimio la Arusha? Mbona hawakumnukuu Nyerere wakati wanavunja miiko na maadili? Mbona hawakumsifu Nyerere walipokuwa wanauza mali ya umma – viwanda, majumba makubwa na nyumba za serikali? Mbona hawakuogopa jeshi kupindua serikali katikati ya ufujaji wa kiwango hicho?

Hoja ni kuwa na serikali tatu chini ya jina lolote lile – Muungano au Shirikisho; lakini watawala wamechonga ndimi na kupeperusha midomo yao wakidai ndani na nje ya Bunge, kwamba serikali tatu “zitaua Muungano,” na kwamba jeshi litawapindua.

Kinachoonekana machoni mwa watawala na katika kauli zao; ni kwamba hawaamini wanachosema. Wangekuwa wanaamini wasemacho, Zanzibar isingempokonya rais wa Muungano madaraka makubwa anayopewa na Katiba huku yeye na wenzake wakichekelea tu.

Kama kweli watawala wanaogopa serikali yao kupinduliwa na jeshi la wananchi kutokana na kuwa na mfumo wa serikali tatu; wanashindwaje kuelewa kuwa waliishapinduliwa zamani kwa rais kupokonywa mamlaka kadhaa kupitia Katiba ya nchi jirani – Zanzibar?

Walichelewaje kuita jeshi kulinda mamlaka ambayo rais alipewa na wananchi chini ya Katiba? Hakika utawala wa mazonge!

(imechotwa katika mtandao wa: ndimara.tegambwage.facebook.com ya 17 Aprili 2014)​

Well said Mzee Ndimara jamaa wanatumia vitisho badala ya hoja kutetea serikali 2
 
Back
Top Bottom