Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

Ndimara: Kikwete, mmechelewa kuliita Jeshi

Wanaoharibu mchakato ni UKAWA ambao wametoka nje ya Bunge

Miafrika bwana tabu tupu! Yaani badala ya kufikiria na kujadili namna serikali tatu zitavyopata vyanzo vyake vya mapato yanajikita kutishia watu eti jeshi litapindua serikali! Mbona marekani haijapinduliwa? Mbona india haijapinduliwa n.k! Huyu rais wetu naye sometimes nashindwa kuamini kama huwa anaongea ya kwake au naye amelishwa tu na matepeli wa kisiasa! Kumbuka jeshi ni taasisi na jeshi kufikia kuchukua nchi eti kwa sababu serikali imekosa hela ya kulipa mishahara basi taasisi nyingine zote zitakuwa zimeshazirai kiuchumi. Jeshi ndiyo priority namba moja kwa nchi yoyote ile hapa duniani! iwe ni nchi maskini au tajiri!
 
Nilimsikia vizuri wakati Kikwete akihutubia bunge la katiba.Kifungu alichokisemea mtoa hoja ameamua kwa makusudi kabisa kutaka kupotosha jamii.Kikwete hakusema kukiwa na serikali 3 jeshi litapindua nchi.
Kama ufahamu wangu unaniambia niko sahihi na uchambuzi wa hutoba ya Kikwete ni kwamba ,rais alitoa angalizo kuwa serikali ya shirikisho itakuwa haina vyanzo vya UHAKIKA vya kukusanya kodi zaidi ya kuzitegemea serikali za washirika.
Wakati yaho yakitokea SERIKALI AMBAYO HAIKUSANYI KODI YAANI SERIKALI YA SHIRIKISHO NDIYO ITAKAYOMILIKI JESHI LA ULINZI,POLISI,MAGEREZA,UHAMIAJI,USALAMA WA TAIFA.
Katika akili ya kawaida tu mtu jiulize,hivi vikosi vyote hivyo vikikosa mishahara kwa miezi sita kutokana na serikali za washirika kutokupeleka fedha kwa serikali ya shirikisho hali itakuwaje.
Msimbeze bure ,Kikwete yeye ndiye rais wa nchi, na kwa hiyo mpaka atamke maneno yale, ni dhahiri hakukurupuka.
Mimi kwa mtazamo wangu ilikuwa tukanushe maneno ya rais kuwa sio ya kweli,tungejikwika mzigo wa kuisaidia serikali juu upatikanaji wa vyazo vya uhaklika vya serikali ya shirikisho vitatoka wapi bila kuadhiri mwendendo mzima wa uendeshaji aw serikali
 
Back
Top Bottom