Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.
Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili
ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu