Ndege ya rais Tanzania ni mali ya CCM?

nsami

Senior Member
Jun 11, 2010
175
8
Wakuu salaam!
Naomba msaada wandugu, nimeona picha ya ndege ya rais kwenye gazeti la the citizen la leo ambayo mhe. Mramba wakati akiwa waziri wa fedha alisema watz hata kama watakula nyasi lakini lazima inunuliwe. nimeshituka kuona pamoja na alama nyingine za taifa kama jina la nchi, nembo ya bibi na bwana alama ya bendera ya taifa pia imeandikwa 5H-CCM. Hii ina maana gani?
Msaada pleeeese!
 
Wewe ngoja aingie rais ambaye sio CCM nchi itawaka moto hii, magereza yatakuwa hayatoshi.
 
Uko makini sana mkuu kwa kuweza kuona hayo na kuyatafutia majibu.
Binafsi ngoja kwanza nifanye uchunguzi kidogo, nitarudi.
 
Hata EU waliona upungufu huo na kusema mipaka kunakoishia serikali na kule kunakoanzia himaya ya chama cha siasa kinachoitwa CCM ni nyembamba sana kama si kupata tu ujasiri wa kusema hamno.

Huu ni msingi mojawapo unaotufanya kutafuta Katiba Mpya nchini kurekebisha hilo dosari kubwa na lenye gharama kubwa nchini.
 
ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!

Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake,anayeshabikia ovyo matembezi ya Mhe Jakaya Kikwete Wizara moja baada nyingine bila kutupa VERIFIABLE FACTS and FIGURES juu ya ushabiki wake, akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??

Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.

Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????

Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.

Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.

Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.

Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????
 
Air craft registration number. THE PREFIX ......5H: DENOTES TANZANIA REGISTRATION AND SUFFIX ....... CCM IS THE AIRLINE CALL SIGN
 
Wakuu salaam!
Naomba msaada wandugu, nimeona picha ya ndege ya rais kwenye gazeti la the citizen la leo ambayo mhe. Mramba wakati akiwa waziri wa fedha alisema watz hata kama watakula nyasi lakini lazima inunuliwe. nimeshituka kuona pamoja na alama nyingine za taifa kama jina la nchi, nembo ya bibi na bwana alama ya bendera ya taifa pia imeandikwa 5H-CCM. Hii ina maana gani?
Msaada pleeeese!
Mkuu umechanganya mambo ndege ya 5h-CCM ni ile Faulker F-28 iliyonunuliwa mwaka 1978 (picha chini), miaka yote inaitwa CCM.
1788160.jpg

Ndege ambayo ilinunuliwa wakati wa Mkapa registration yake ni 5H - ONE (picha chini)
1874249.jpg
 
Attachments

  • 1788160.jpg
    1788160.jpg
    27.8 KB · Views: 117
Wakuu salaam!
Naomba msaada wandugu, nimeona picha ya ndege ya rais kwenye gazeti la the citizen la leo ambayo mhe. Mramba wakati akiwa waziri wa fedha alisema watz hata kama watakula nyasi lakini lazima inunuliwe. nimeshituka kuona pamoja na alama nyingine za taifa kama jina la nchi, nembo ya bibi na bwana alama ya bendera ya taifa pia imeandikwa 5H-CCM. Hii ina maana gani?
Msaada pleeeese!

Mkuu.
Hiyo 5H- CCM ina maana ya Tano Hatua ..Chidege Chinapaa Mawinguni.

Any way, Hapa TZ..Serikali ndio CCM na CCM ndio serikali kama hilo hukufundishwa shuleni.
CCM pia ndio Nchi yetu. Mkuu umesahau chama kushika hatamu?
 
Ondo shaka hiyo ni registration tu tena tangu inunuliwe na nyerere 1978!!

Ila ni kweli kuwa inatumiwa sana na viongozi wa ccm na kwamba haijawekwa wazi taarifa za mapato na matumizi ya shirika hili..
 
Wakuu salaam!
Naomba msaada wandugu, nimeona picha ya ndege ya rais kwenye gazeti la the citizen la leo ambayo mhe. Mramba wakati akiwa waziri wa fedha alisema watz hata kama watakula nyasi lakini lazima inunuliwe. nimeshituka kuona pamoja na alama nyingine za taifa kama jina la nchi, nembo ya bibi na bwana alama ya bendera ya taifa pia imeandikwa 5H-CCM. Hii ina maana gani?
Msaada pleeeese!

correction! ni waziri masilingi alipokuwa anahojiwa kama sio tbc itakuwa itv kipindi kilikuwa saa 3 usiku.
 
Ondo shaka hiyo ni registration tu tena tangu inunuliwe na nyerere 1978!!

Ila ni kweli kuwa inatumiwa sana na viongozi wa ccm na kwamba haijawekwa wazi taarifa za mapato na matumizi ya shirika hili..
Mkuu,

Wewe at least umeanza kutoa mwanga wa jibu la muuliza swali!

Kwa kawaida na kwa mujibu wa sheria na miongozo ya ICAO, registration ya ndege kwa nchi husika ni kama zile za Magari tu..Kwa Tanzania, zote zinaanza na 5H(Ikimaanisha nchi ta Tanzania).Kenya ni 5Y, Uganda 5X, na S.Africa wanaanza na ZS.

Kuna series ya kawaida inayoendelea ya utoaji wa namba hizo, lakini kama mwenye ndege anataka herudi fulani za kuzichagua mwenyewe, basi analazimika kulipia kiasi fulani cha fedha kuprocess ombi hilo...Kuna wenye ndege kibao wanaolipia na kuweka majina yao au ya familia zao.

Ndege ya serikali(5H-CCM) ilinunuliwa mwaka 1978, mara baada ya kuzaliwa chama cha mapinduzi, hivyo kwa akili ya kawaida tu , na kwa uzalendo wa miaka hiyo waliamua kuipa hiyo registration kama sehemu ya excitement ya tendo hilo la kizalendo kwa enzi hizo, lakini haimaanishi kamwe kuwa ni mali ya chama cha mapinduzi.

Ndege hii ni mali ya Tanzania Government Flights Limited(TGFL), au Wakala wa Ndege za SERIKAli...
Wengi wamekuwa wakistuka wakiona registration hiyo, lakini ni usajili tu, na si vinginevyo.
 
Asante kwa kumueleza ndugu yetu, na to add to that hatuna ndege ya "rais", zote ni ndege za TGF na zinaweza kutumika kwa shughuli mbali mbali anyone can lease them if they can afford it. 5H-CCM (Fokker f28)imekuwepo miaka 33! nyingine ni 5H-TGF (Fokker F50) na 5H-ONE (Gulfstream G550)
 
Kwa kuongezea kuna rubani alikuwa akiirusha aliwahi niambia kuwa inaitwa "Chali Chali Mike"
 
Mkuu,

Wewe at least umeanza kutoa mwanga wa jibu la muuliza swali!

Kwa kawaida na kwa mujibu wa sheria na miongozo ya ICAO, registration ya ndege kwa nchi husika ni kama zile za Magari tu..Kwa Tanzania, zote zinaanza na 5H(Ikimaanisha nchi ta Tanzania).Kenya ni 5Y, Uganda 5X, na S.Africa wanaanza na ZS.

Kuna series ya kawaida inayoendelea ya utoaji wa namba hizo, lakini kama mwenye ndege anataka herudi fulani za kuzichagua mwenyewe, basi analazimika kulipia kiasi fulani cha fedha kuprocess ombi hilo...Kuna wenye ndege kibao wanaolipia na kuweka majina yao au ya familia zao.

Ndege ya serikali(5H-CCM) ilinunuliwa mwaka 1978, mara baada ya kuzaliwa chama cha mapinduzi, hivyo kwa akili ya kawaida tu , na kwa uzalendo wa miaka hiyo waliamua kuipa hiyo registration kama sehemu ya excitement ya tendo hilo la kizalendo kwa enzi hizo, lakini haimaanishi kamwe kuwa ni mali ya chama cha mapinduzi.

Ndege hii ni mali ya Tanzania Government Flights Limited(TGFL), au Wakala wa Ndege za SERIKAli...
Wengi wamekuwa wakistuka wakiona registration hiyo, lakini ni usajili tu, na si vinginevyo.

Lakini hata viwanja vya mpira vilijengwa chini ya ccm na mpaka leo ni mali ya ccm. Hata hii ndege watasema mali yao waliisahau vilipokuja vyama vingi.
 
Sasa umeanza kuja vizuri. sio ndege tu. bali vyama vyote vilivyokewepo kabla ya 1991, vilitakiwa kuhakikiwa na mali zote za umma kuwekwa sawa. Jina CCM halikutakiwa kutumika, kama vile ANC, UPC Nk sasa, tatizo CCM haikuvunjwa wakati ule. Kumbuka Chama na serikali ilikuwa kitu kimoja. CCM ikachukua mali zote za umma, na kuzimiliki.

Office
Viwanja
Ndege
Magari
Kura
Raisi
nk

Haya mambo mazito, ngoja nifikiri zaidi, nitarudi:redfaces:
 
Back
Top Bottom