Ndege ya Precision Air yapasuka matairi yote manne huko Arusha!

Ndege ya Precision Air yapasuka matairi yote manne huko Arusha!

jamani eeeh tusitie chumvi,hakuna kiraka katika tairi.....kitaaalam inaonekana brake haziku fungua mpaka mwisho ndo maaana hii ikatokea....ni technical problem ya kawaida .........

Ni technical problem ya kawaida?!? Sasa hii ndio chumvi, tena kali. Umewahi kupanda ndege? Uliza wanaopanda ndege kila siku ni mara ngapi ndege walizopanda zilipasuka matairi wakati wa kutua, kitu ambacho "ni technical problem ya kawaida".

By the way, suala la viraka kwenye tairi limeripotiwa na shuhuda wa hii incident. Sasa sijui tukuamini wewe au yeye?
 
kambi za urais zinatafutana roho,sijui kambi ya nani hii ilitaka kumuondoa mamvi?am only thinking aloud.
 
Kama kweli hizi tairi wanachakachua nma kuweka viraka aisee wasimamishwe haraka na mamlaka husika ifanye kazi ipaswavyo kuokoa maisha ya watz lakini pia kujenga imani kwa usafiri wa anga ni aibu kwa tendo kama hili.poleni mlifikwa na mkasa huo
 
Hata kama angeondoka sioni hasara yoyote kama alishindwa cheo kidogo kikubwa atawezaje? Namshauri 2015 agombee uenyekiti wa kijiji
 
Raisi wako au wa kikundi fulani ndani ya ccm? Mimi kwa makundi haya na hali ilivyo ndani ya ccm nasubiri kuona kitakachotokea 2015, macho yangu mie.
 
Rais wa Akudo (wazee wa masauti) au Extra Bongo? Nasikia alisomea sanaa!
 
Huo urais 2015 labda akaupatie MIREMBE...

By the way naskia Mzee afya ni gogoro ataweza mikikimikiki ya kupangua tuhuma za ufisadi zinazomkaba?
 
Hiyo ni ajali ya kawaida tu ila kwa ninavyowajua watz kwakuwa el alikuwepo suala litaelezewa kama hujuma za kisiasa.
 
Rais wa chama cha kutoa misaada 2015-2025 cha Rotary Club tawi la Tanzania.
 
Nani anampa kura lowasa?? Akiwa raisi naenda kukaa ughaibuni mpaka muda wake uishe
 
Abiria kadhaa akiwemo aliyekua
Waziri Mkuu na Mbunge wa
Monduli Edward Lowassa leo
December 13 wamenusurika baada
ya ndege waliyokuwa wakisafiria
kupasuka matairi yote manne ya
nyuma wakati ilipokuwa ikitua
katika uwanja wa ndege wa Arusha
Ijumaa December 13 2013.
Ndege hii mali ya shirika la ndege
la Precision aina ya ATR ilipata
tatizo hili wakati ikitua Arusha
ambapo Matairi yote manne ya
nyuma yanaripotiwa kupasuka na
kusababisha taharuki kwa abiria.
Jumla ya watu 41 waliokua kwenye
ndege hiyo, abiria 39 na
wafanyakazi 4 wametoka salama.
Sikujua kwamba uchaguzi wa rais wa mwaka 2015 umeshafanyika.
 
Aiisee,binafsi nashukuru Mungu kwa abiria wote ,kwani wametoka salama,kitu ambacho ni nadra hasa kwa safari za ndege kwa nchi changa kama yetu.......
 
watz tutakuwa tumeishiwa kama tutampa kura ya urais Lowasa 2015!!
 
Back
Top Bottom