Ndege ya Precision Air yapasuka matairi yote manne huko Arusha!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,213
2,000
Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.

Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.

DSC00607.JPG
 
Nebuchadnezzar

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
212
195
Tanzania (Africa) kila mtu ni mjanja-mjanja.

Mungu alituumba Waafrika tukiwa na roho ngumu kwasababu hata kuchuchumaa kwenye choo cha Kiswahili na kujisaidia inahitaji uwe na roho ngumu. Jambo kama hili lililotokea ni jambo la hatari lakini Waswahili tutalichukulia poa.

Poleni mliokumbwa na hayo maswahibu.
 
saragossa

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
2,151
2,000
Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.
Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.

View attachment 126474

Duh...hii balaa. Na ukizingatia ndio mwisho wa mwaka, ndo majanga kabisa. Poleni wasafiri wote mliokuwepo ndani ya ndege hiyo, na tumshukuru mungu kwa kuwanusuru na janga kubwa zaidi ya hilo ambalo lingeweza kutokea.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
13,424
2,000
Duh. Hivi hakuna mtu wa TCAA wa kukagua usalama wa magurudumu hayo kila mara kama wanavyokagua injini? Eti PakaJimmy, tupe ufafanuzi
 
Last edited by a moderator:

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,211
2,000
Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.
Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Matairi ya ndege huwa yanabadilishwa kutokana na idadi ya kutua na kuruka, na hata kama yanaonekana bado mapya yakifikisha idadi za kuruka na kutua yanatakiwa kubadilishwa. Sasa kama hawa jamaa wa Precision wamefikia hadi kuyatia viraka, ni hatari na wanastahili hata kufungiwa kwa kukiuka sheria za IATA za Usalama wa Ndege na Abiria. Ina maana hata kufuata "aircraft maintanance schedule" hawatafanya, na spea za ndege zinazobadilishwa kwa kuangalia masaa ya kuruka kwa ndege watakuwa hawazibadilishi.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,689
2,000
Hiyo ni Snag ya kawaida saana ktk usafili wa Anga,mambo ya tyre flatted si Tanzania tu bali ni sehemu mbalimbali Duniani
 
Vinci

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
2,642
2,000
Dah...kweli hapo kwenye red haiwezi kuingia watu akilini, hata matairi ya ndege nayo yanawekea viraka?:frusty: Poleni wote.
Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.
Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.

View attachment 126474
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,619
2,000
Wanajamvi

Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amenusurika kifo kufuatia ndege aliyopanda kupasuka magurudumu ya nyuma wakati ikitua uwanja wa ndege ARUSHA hivi punde.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom