Ama kweli kua uyaone:
Miaka kati ya 70-80 nakumbuka nikiwa mdogo hadi naingia shule ya msingi, Jeshi letu lilikuwa madhubuti saaana kupita maelezo.
Jeshi enzi hizo, lilikuwa na wanajeshi shupavu, wenye misuli na warefu.
Jeshi pia lilikuwa na vifaa vingi, km magari, Ndege n.k.
Jeshi lilikuwa likiendehs Hospitali zake karibu katika kila Kambi yake na tena dawa zilikuwa zinapatikana bureeee. Madaktari wa jeshi walikuwa wanaaminika sana kwa kuchapa kazi.
SASA JESHI LA LEO
Jeshi la sasa limeingiliwa na maradhi ya mdondo! Nathubutu kusema hivi sababu hao wanajeshio wenyewe ukiwaon utawaonea huruma:
Yaani MICHANGANYO KALETE!- humo wamo Mbilikimo, kina magagula, kina yomba yomba, kina tendegu, kina YAHEEEEE n.k
HAPA NAONA KICHEFU CHEFU TU.
Halafu wengi wao wagumu kishenzi kuelewa, wakikomalia jambo ndio hilo hiloooo mpaka kunakucha.
Jeshi halina vifaa na wanajeshi wanaishi URAIANI, hii si aibu?
Hospitali za jeshi nyingi zimezimika kama mshumaa!
Jeshi limekuwa shabiki wa chama tawala na viongozi wake!
Wanaofaidi ni wale wakubwa tu wa chini kazi yao kwata na sherehe za kitaifa, jasho linawatoka na wanaambulia soda au chupa ya maji tu.
nadhani imefika wakati kujifunza na kurudisha heshima ya jeshi letu.
Tuwe na jeshi dogo lenye nidhamu na la wasomi na siyo kuona kama jeshini ni sehemu ya kuajiri mtu yeyote hata kina CHAKUBIMBI!