Ndege ya Jeshi yaanguka airport Dar

Wengine hapa huwa hatuandiki kejeli au kwa dhana. Hupenda kuandika kwa reference. Nimekueleza wazi udhaifu wa Jeshi la Tanzania. Rejea wikipedia utaliona hilo na pitia references mbalimbali zilizotajwa. Pia unaweza kuangalia hapa EAST AFRICA: An Idi-otic Invasion - TIME utashangaa namna Watanzania walivyozitungua ndege zao wenyewe. Tanzania ilishinda vita vile, lakini madhara yake kutokana na jeshi dhaifu hayajaisha hadi leo hii. Kutaja platoon hakujustify umaridadi wa jeshi. Labda ungeweka facts ingependeza zaidi.
Jeshi dhaifu haliwezi kushinda vita! Hayo mambo unayoelezea kwenye vita ni kitu kisichokwepeka. Au hufuatilii vita vya majeshi ya nchi zilizoendelea? Waamerika wameuana wenyewe kwa wenyewe sehemu nyingi tu....
Anyway naona uelewa wako wa mambo ya military sio mzuri....
 
He kudungua ndege tano kwenye nchi masikini kama yetu halafu unasema jeshi liko organised? Hata kama uelewa wetu wa mambo ya military siyo mzuri hiyo haikukaa sawa, kuna kauzembe fulani ulifanyika au ukosefu wa taaluma husika.

Tusilaumu ya Mbagala na GOMs basi.
 
Jeshi dhaifu haliwezi kushinda vita! Hayo mambo unayoelezea kwenye vita ni kitu kisichokwepeka. Au hufuatilii vita vya majeshi ya nchi zilizoendelea? Waamerika wameuana wenyewe kwa wenyewe sehemu nyingi tu....
Anyway naona uelewa wako wa mambo ya military sio mzuri....
Hivi unafaham wengi ambao wanakuwa recruited jeshini wanauwezo gani? Halafu unafaham idadi ya ndege ya jeshi la Tanzania wakati huo zilikuwa ngapi?
 
wadau nimesikia kuna ndege ya jeshi leo mchana imeanguka baada ya kushindwa kutoa matairi wakati wa kutua na kuangukia tumbo; wanajeshi wachache waliokuwemo humo wameumia. Taarifa hizi nimezipata kutoka kwa mdau chuo cha zima moto na uokozi;

Naanza kutilia shaka utendaji wa Jenerali Mwamunyange! Je kuna mdau wa JF mwenye wasifu wake? Weka tuuone
 
hizi si tetesi ni kweli na mimi pia nilikuwa ni kati watu wa mwanzo kushuhudia hili ...nikiwa kwenye ndege inayotua ....tulitua kabla ya hizo ndege....

well sio ishu kubwa sana .....ni zile ndege za wanafunzi wa urubani jeshi[yellow].....zilikuwa tatu walikuwa wapo kwenye routine training,,,,katika kutua aliyetangulia kutua alitua upande na tairi moja badala ya kutumia matairi yote mawili...kwa hiyo ile ndege ikavutwa nje ya runway...huyo afisa mwanafunzi alijitahidi kiasi kuidhibiti...kwani angepanic ingebinuka.....ilipofika kwenye majani ikasimama...haapakuwa na madhara makubwa ...inaweza kukarabatiwa na kuruka tena kwa urahisi tu.....ikumbukwe tukio hili la ndege za wanafunzi ni kama la ile ndege iliyotua barabarani.....na watu pale walitueleza kuwa jeshi lilikuwa na ndege nne za kufundishia zinazoruka.....baada ya ile iliyogongwa na gari ..walitegemea wanunuliwe ndege mpya za jet fighter school -moro..lakini hawajapata....kwenye training jambo lililotokea ni la kawaida sana....ndio maana mjuwe gharama za kumfundisha rubani vita ni kubwa sana.........
 
Back
Top Bottom