Kabla ya kusifia ndege mpya au ya zamani, kwanini wanachangisha madawati? Pesa za ndege zingenunua madawati zaidi ya laki 2!!
Nyumbu zinashangilia ndege ilhali hospitali hakuna chanjo ya pepopunda. Na zinginezo.
Mi sijui nani anashauri hao wanaotawala. Ndege inalipiwa cash wakati kuna watu hawajalipwa madai yao hapohapo Atcl na kwenye utumishi wa umma.
Ni sawa na kijana alieanza kazi halafu ananunua gari (hata kama ni baby walker haili sana mafuta) ili nae aonekane anamiliki gari.
Wanasahau kabisa ukishakosea vipaumbele ndo unakaribisha mabalaa. Hiyo midege siipandi asilani (labda iwe ndo aina pekee ya usafiri ulobaki na ni lazima nisafiri wakati huohuo) maana kila nikiwa humo ndani ntakumbuka watoto wanaokaa chini bila madawati na watu wanaokosa chanjo za pepopunda.
Ufahari uko wapi ikiwa unajisifia ndege na huna madawa? Ikipata dharura hao watu unawatibia na nini?
Sitapongeza hili la ndege.