Ndani ya nchi yetu fisadi ni mtu mmoja tu ambaye serikali imeshindwa kumchukulia hatua ?

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,932
5,560
Heshima kwenu wana JF,

Kwa muda mrefu kumekuwa tuhuma zinaendelea kwenye mtandao ya kijamii hasa humu JF. Kuhusu tuhuma za ufisadi ambazo muhusika anasemwa sana Lowassa.Nakumbuka wakati Lowassa akitangaza nia ya kugombea urais wakati akiwa CCM katika uwanja stadium Arusha alisema mwenye ushahidi yeye ni fisadi aende mahakamani na kama huna ushahidi nyamaza kimya.

Baaada ya mchakato wa Lowassa kuhamia CHADEMA kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaofanywa vijana wa Lumumba wakiongozwa na Lizaboni kuhusu Lowassa.

Nchi ipo kwenye hali mbaya kutokana uhaba mkubwa wa sukari nchini bado watu wamekuwa wakileta mambo ya siasa mpaka kwenye kumtuhumu wafanyabiashara ambao wameficha sukari ni marafiki zake Lowassa, je serikali imeshindwa kuwachukulia hatua hao marafiki zake Lowassa?

Tuweke itikadi za vyama pembeni tujadili swala hili fisadi mkubwa ndani ya nchi yetu ni Lowassa tu? Serikali imeshindwa kumchukulia hatua mtu mmoja?
 
Pale mbeya kipindi cha kampeni mwakyembe alisema ana ushahidi wote kuwa Lowasa ni fisadi na aliahidi kufungua kesi Muda wowote kabla ya siku ya uchaguzi ambayo ilikua Oct 25. Mpaka Leo ni miezi sita imepita mwakyembe yupo kimya sasa sijui kwanini serikali ya ccm imeshindwa kumkamata huyo Lowasa toka 2008 hadi Leo. Katika utumbuaji wa yanayoitwa majibu (mimi sipendi jina hili) wanaotumbuliwa ni wengine lakini Lowasa hajaguswa zaidi ya kelele za akina Lizaboni, singidadodoma, Ritz, simiyu yetu na sampuli nyingine kama hizo hapa jf.
 
Si kweli hao walikuwa wanachukua pesa za watumishi hewa wamefanywaje au tumeishia kujua idad ya watumishi hewa ni wangapi? Je wahusika wamewajibishwa kwa kuiibia serikal?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Si kweli hao walikuwa wanachukua pesa za watumishi hewa wamefanywaje au tumeishia kujua idad ya watumishi hewa ni wangapi? Je wahusika wamewajibishwa kwa kuiibia serikal?
Mkuu sijui hata kama wahusika wamekamatwa kila kitu naona kama usanii tupo hao watumishi hewa dili zao wenyewe
 
Mkuu sijui hata kama wahusika wamekamatwa kila kitu naona kama usanii tupo hao watumishi hewa dili zao wenyewe
Hamna kitu hapo kwenye sukari kwenyewe tumeambiwa wasumbufu hawazidi kumi sasa mbona mpaka Leo sukari iko juu, au hao kumi haishi humu nchini?
 
Mkuu nakukatalia ndani ya nchi Yetu iliyochini ya chama mahili CCM mafisadi ni wengi sana ambao Mh.Magufuli anahangaika nao Na wote ni wana CCM DAMU
 
Hamna kitu hapo kwenye sukari kwenyewe tumeambiwa wasumbufu hawazidi kumi sasa mbona mpaka Leo sukari iko juu, au hao kumi haishi humu nchini?
mkuu kuhusu sukari mtumbua vipele alikurupuka kuzuia kuingizwa sukari nchini bila kujipanga wiki mbili zimepita alisema walioficha sukari kule mbagala anawajua mbona sukari bado hajapatikana hakuna kitu kibaya kama kukurupuka
 
Mtumbuaji wa majipu mwenyewe kama ni jipu unategemea nini?
 
mkuu kuhusu sukari mtumbua vipele alikurupuka kuzuia kuingizwa sukari nchini bila kujipanga wiki mbili zimepita alisema walioficha sukari kule mbagala anawajua mbona sukari bado hajapatikana hakuna kitu kibaya kama kukurupuka
nkisikia swala la sukari nashikwa na hasira sana
 
Back
Top Bottom