Kwa viongozi wote ambao juu yao Kuna mamlaka kubwa kuliko mamlaka waliyonayo. Wajifunze katika kisa cha wafanyakazi wawili wa Farao, mnyweshaji na mwokaji.
Unapokisoma kisa hicho, soma kwa tafakari ya juu hasa kwenye ndoto walizoota.
Utagundua kwa nini mnyweshaji alirudishwa kazini na kwa nini mwokaji alikatwa kichwa.
Ukishindwa ya Biblia, Kuna kanuni za kibiblia zimeandikwa katika kitabu kisichofungama na Imani kinaitwa 48 laws of power.
Kiafrika Afrika, ukiwa ukiongozi na ujazingatia visa vya kiuongozi vya Biblia au hata vitabu vya kawaida, utakuwa na asilimia kubwa ya kuwa salama. Tofauti na hapo, utakuwa mithili ya mwokaji wa Farao.