"Tarehe 20 November 2013 watu wasiojulikana walipost mawasiliano ya email yaliyodaiwa kuwa ni mawasiliano ya email yaliyonaswa kati ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM mhe Mwigulu Nchemba na Mimi.
Tukidaiwa kula njama za kumsaidia Mhe zitto Kabwe.
Nililipuuza jambo hilo kwa sababu niliamini kila mwenye akili timamu atajua mawasiliano hayo ni ya kughushi. Lakini kutokana na wanachi wengi kutaka kujua kama yana Ukweli nimelazimika kusema kifupi.
KWANZA mimi na mwigulu hatujawahi kuwasiliana kwa Email katika maisha yetu.
PILI wenye chuki na mhe ZITTO sio lazima watumie email za kughushi ambazo zinachafua wasiohusika kwasababu tu ya wao kuitaka Shingo ya mhe Zitto.
TATU tunachukua hatua za kisheria ili waliohusika na kughushi email hizo na wanaozisambaza wafikishwe kwenye kwenye vyombo vya sheria ili Kukomesha tabia hii ambayo imeanza kuota mizizi."
Emmanuel John Nchimbi.
mpeleke kapuya kwanza au yule binti!
Ben saanane ni MTU wa kutafuta sifa kupitia mitandao nani asiyemjua baada ya kuona single ya zitto imemtoa jasho akaona amtumie nchimbi name mwigulu apate sifa.yupo tayari kutunga uwongo ilimradi apate sifa eti kijana makini
mpeleke kapuya kwanza au yule binti!