Taswira
JF-Expert Member
- Sep 23, 2012
- 1,198
- 447
Kufuatia eti yaliyodaiwa Mawasiliano hatari ya Nchimbi, Mwigulu na Zitto kuihujumu CHADEMA, mawasiliano yaliyosambazwa na Ben Saanane mitandaoni na hapa JF, Waziri Nchimbi ametoa kauli leo asubuhi kupitia Valid Account yake ya Facebook kuwa ni uzushi, ni uongo, na sheria sasa inaelekea kuchukua hatua yake dhidi ya mhusika liyeghushi na kusambaza ujumbe huo.
Nanukuu kutoka Account ya Emmanuel Nchimbi (Facebook)
Nanukuu kutoka Account ya Emmanuel Nchimbi (Facebook)
"Tarehe 20 November 2013 watu wasiojulikana walipost mawasiliano ya email yaliyodaiwa kuwa ni mawasiliano ya email yaliyonaswa kati ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM mhe Mwigulu Nchemba na Mimi.
Tukidaiwa kula njama za kumsaidia Mhe zitto Kabwe.
Nililipuuza jambo hilo kwa sababu niliamini kila mwenye akili timamu atajua mawasiliano hayo ni ya kughushi. Lakini kutokana na wanachi wengi kutaka kujua kama yana Ukweli nimelazimika kusema kifupi.
KWANZA mimi na mwigulu hatujawahi kuwasiliana kwa Email katika maisha yetu.
PILI wenye chuki na mhe ZITTO sio lazima watumie email za kughushi ambazo zinachafua wasiohusika kwasababu tu ya wao kuitaka Shingo ya mhe Zitto.
TATU tunachukua hatua za kisheria ili waliohusika na kughushi email hizo na wanaozisambaza wafikishwe kwenye kwenye vyombo vya sheria ili Kukomesha tabia hii ambayo imeanza kuota mizizi."
Emmanuel John Nchimbi.