Nchimbi: Email iliyosambazwa mitandaoni ni ya Uongo, Nimeshaanza kuchukua hatua za Kisheria

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
Kufuatia eti yaliyodaiwa Mawasiliano hatari ya Nchimbi, Mwigulu na Zitto kuihujumu CHADEMA, mawasiliano yaliyosambazwa na Ben Saanane mitandaoni na hapa JF, Waziri Nchimbi ametoa kauli leo asubuhi kupitia Valid Account yake ya Facebook kuwa ni uzushi, ni uongo, na sheria sasa inaelekea kuchukua hatua yake dhidi ya mhusika liyeghushi na kusambaza ujumbe huo.

Nanukuu kutoka Account ya Emmanuel Nchimbi (Facebook)
"Tarehe 20 November 2013 watu wasiojulikana walipost mawasiliano ya email yaliyodaiwa kuwa ni mawasiliano ya email yaliyonaswa kati ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM mhe Mwigulu Nchemba na Mimi.

Tukidaiwa kula njama za kumsaidia Mhe zitto Kabwe.

Nililipuuza jambo hilo kwa sababu niliamini kila mwenye akili timamu atajua mawasiliano hayo ni ya kughushi. Lakini kutokana na wanachi wengi kutaka kujua kama yana Ukweli nimelazimika kusema kifupi.

KWANZA mimi na mwigulu hatujawahi kuwasiliana kwa Email katika maisha yetu.

PILI wenye chuki na mhe ZITTO sio lazima watumie email za kughushi ambazo zinachafua wasiohusika kwasababu tu ya wao kuitaka Shingo ya mhe Zitto.

TATU tunachukua hatua za kisheria ili waliohusika na kughushi email hizo na wanaozisambaza wafikishwe kwenye kwenye vyombo vya sheria ili Kukomesha tabia hii ambayo imeanza kuota mizizi."

Emmanuel John Nchimbi.
 
Kwanza sitaki kuamini haya maelezo ni ya waziri, ila kama ni kweli haya ni maelezo yake;

Waziri alipuuzia lile jambo???

Yawezekana kabisa tunawaamini watu wasiotakiwa kuaminiwa,sad!!!!!!

Acha majambazi watanue na kuua watakavyo asee,kitu kinaharibu taswira ya Taifa na mshikamano wa nchi kupitia siasa,waziri anasema alipuuzia!!!!!?????

Eeenh Mwenyezi Mungu tuonee huruma waja wako!!
 
hakuna kitu hapa ni siasa tu za maji taka, kwanza yeye mwenyewe ajitakase na makosa makubwa anayoyafanya ofisi kwake kupitia msangi na damu ya mvungi itaendelea kutesa wengi RIP DR MVUNGI
 
Ben saanane ni MTU wa kutafuta sifa kupitia mitandao nani asiyemjua baada ya kuona single ya zitto imemtoa jasho akaona amtumie nchimbi name mwigulu apate sifa.yupo tayari kutunga uwongo ilimradi apate sifa eti kijana makini
 
Na wewe unatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwakuwa umeghushi hayo maelezo kuwa ni ya waziri Nchimbi wakati ni yako,

Nchimbi akitaka kutoa maoni ama kauli yake asingetumia fb ambayo kwanza haiaminiki kuwa ni a/c yake halisi,

Nikiyatazama kwajicho la tatu maneno yote yaliyo kwenye andishi hilo nayaona ni ya kundi la Zitto Kabwe na sio Nchimbi Emanuel, labda nchimbi wa mwandiga.

Uzushi wako peleka hukohuko fb
 
Tumesubiri kwa muda mrefu? alikuwa anaweka mambo sawa nini?
Hii serikali bwana!
Halafu kuna hili la taarifa za siri ambazo Zitto na Kitila wanaziita hekaya. TISS wametuhumiwa tuhuma nzito sana ndani ya ile taarifa. Lakini anayeonekana kuhangaika ni Zitto tu, vipi TISS nao wamepuuzia?
 
"Kwa sababu tu ya wao kuitaka Shingo ya mh. Zitto"..Nukuu ya Emmanuel Nchimbi.
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba Mhe. Waziri Nchimbi ataenda mahakamani. Alisema hivyo hivyo wakati wa kitabu cha MAFISADI wa Elimu lakini hadi leo hajatia mguu mahakamani.

Ni Waji.nga tu ndio watamuani Nchimbi kwamba atakanyaga katika corridor za kimahakama kwenye issue hii.

BTW, hivi waziri Nchimbi ni mtu makini kweli? Habari hizi ambazo ni shutuma kubwa anazitolea afanunuzi FACE BOOK?! Please give me a break Mr. Minister
 
Wanasiasa kutishia kwenda mahakamani ni wimbo tuliouzoe kiasi kwamba sasa umechuja na hauna mvuto tena kwenye masikio.
 
Huyu Nchimbi ukitaka kumkomesha mwambie aongee kiingereza, ni kichekesho. Utasikia zea zea, zisi, zozi na kigugumizi kibao. Watu wenye elimu ya kufoji kama Nchimbi ni vigumu sana kutumia akili kwenye mawasiliano ya siri ndio maana wahuni wamemuumbua mtandaoni. 2016 damu za akini Dr Mvungi, Mwangosi na wengine wengi zitakuwa juu ya huyu jamaa kule Segerea...
 
Ben saanane ni MTU wa kutafuta sifa kupitia mitandao nani asiyemjua baada ya kuona single ya zitto imemtoa jasho akaona amtumie nchimbi name mwigulu apate sifa.yupo tayari kutunga uwongo ilimradi apate sifa eti kijana makini

safari hii lazima akojoe dagaa,viherehere ndo vinamponza,na njaa zake zinazomtuma kusaka madaraka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom