Nchimbi atambika kwenye kaburi la Gama

Nchimbi atambika kwenye kaburi la Gama

Mkuu......nakuomba umuache Mzee Gama (RIP) apumzike kwa amani.......usiandike mambo kwa kusimuliwa kuhusu sera za serikali za wakati huo kuhusu vijiji vya ujamaa......

- Duh leo wamekugusa na wewe kaka mkubwa maana huwa ni bingwa sana wa kutukana wengine, ha! ha! ha! ndio raha ya JF watakubana mbavu mpaka utaonyesha ukweli wako siku moja!! ha! ha! ha!

Le Mutuz
 
ukiua kwa upanga na wewelazima kwa upanga utauawa
 
hili jimaa lilipokuwa waziri lilikuwa linaongea kwa dharau,macho yake ya ukatili yanaonyesha keshato a roho nyingi,kwa ufupi it's like the guy is seeing things,sio mzima kichwani,kila neno linachekacheka.Damu za watu nzito sana.
 
Huyo Nchimbi amepotea maboya. Nafuu angeenda kwenye kaburi la Mwangosi na kumalizia kwenye kaburi la Dr Mvungi!

Well said! Siku Nchimbi akienda kwenye kaburi la Mwangosi na la Dr. Mvungi ndipo atakapopata utakaso na msamaha wa kweli.
 
View attachment 137048 View attachment 137049 View attachment 137051
Picha kulia Gama na kati James Komba na kushoto Nchimbi

Songea huko kuna vituko, maana hayati Laurence Gama si la Emmanuel Nchimbi tu ndilo lililomsumbua kichwani hadi kifo chake, lipo jingine watu wa Songea wanalijua nalo lina mahusiano na hayati Archbishop James Yefunani Komba.

Kuna kitu ambacho walipishana wakati Askofu Mkuu Yefunani Komba alipomwangalisha Gama kimwenendo ujue Gama alikuwa Mkatoliki hali kadhalika Askofu Komba alikuwa mwazi sana na wa kujiamini. Gama akaja juu kwamba yeye ni mtu mkubwa kiserikali anatakiwa aheshimiwe na hivyo atamshikisha adabu Askofu Mkuu Yefunani Komba. Gama akaamrisha kikosi chake kwenye kijiji cha Lituhi kando ya mto Luhuhu mwambao wa Ziwa Nyasa alikozaliwa Askofu Mkuu Yakobo (James) Komba. Palikuwa na hospitali kubwa iliyokuwa inahudumia mwambao wa Ziwa Nyasa, akaifunga pale hospitali, parokia Lituhi akaifunga, shule na kila kitu kisha kuhamishia kwa nguvu wanakijiji wote kwenda kuwamwaga vijiji vya huko karibu na Rwanda, Litumba, Litumbadyosi, Mgazini nk. ikumbukwe hiyo ni kipindi cha Mwinyi wakati operation ya vijiji ilishasahaulika. Akalazimisha hospitali iliyokuwa inahudumia mwambao wa Ziwa Nyasa iwe kijiji cha Rwanda ambao ni pua na mdomo na Hospitali Misheni ya Peramiho na Songea.

Ukawapo uhasama mkubwa na hili lilitokea kipindi cha uongozi wa Ali Hassan Mwinyi, lakini Rais pamoja na kupelekewa malalamiko hayo hakuchukulia hatua na kuacha mambo yalivyo, hivyo uadui kati ya wawili hao ukaongezeka.

Gama na Askofu Komba hawakuombana maji wala kutembeleana kama ilivyokuwa kawaida ingawa Gama alikuwa kipenzi cha viongozi wengine wa dini jimboni Songea.

CCM ilipoadhimishwa kitaifa Songea siku kama 3-4 kabla ya kilele chake Askofu Komba alialikwa kuwa mgeni wa heshima wa siku hiyo Uwanja wa Majimaji ambapo kulikuwa na halaiki nzuri isiyo ya kawaida. Askofu Komba alikubali mwaliko kwa heshima ya Rais Mwinyi aliyekuwepo katika tukio hilo. Hapo ilikuwa nafasi ya kuwakutanisha mahasimu hao wawili na hakuwa na jinsi ilibidi Askofu Komba alipofika jukwani kama geni wa heshima alipaswa kusalimiana na viongozi wote waliokuwapo jukwani kuanzia Rais Mwinyi, Gama na wengineo, na ilikuwa nafasi pekee hao wawili Gama na Askofu Komba kusalimiana kwa mikono kushikana, na kumbe mmoja kati yao alikuwa na afya ya kuungaunga, mapigo ya moyo yakabadilika ghafla.

Askofu aliaga mapema na kuondoka kwenye tukio alasiri hiyo, na alipofika maskani yake kwenye kanisa Kuu la St Mathias Mulumba, mjini songea karibu kabisa na Songea bus Terminal hali ilimzidia. Baada ya saa chache tu majira ya saa mbili jioni siku hiyo hiyo Naibu Askofu Mlelwa alitangaza rasmi kuwa Askofu Mkuu Yakobo (James) Yefunani Komba amemwendea baba wa milele.

Gama tangu wakati huo hakuwa na raha, amekuwa mtu asiye tulia licha nafasi kadhaa alizopata, kwani kabla yakifo chake Askofu Mkuu Yakobo Komba ambaye alijulikana na wengi kuwa na kauli nzito anazotole na zikatekelezeka alisema kamwe Gama hatafanikiwa katika maisha yake ya kisiasa kwa sababu ya usaliti, kisasi na unyama aliwatendea wananchi wa Lituhi mwambao wa ziwa Nyasa wasio na hatia.

Gama hata alipohama Songea, nakumbuka Tabora akawa hata hafiki kusali Kanisa Kuu la Mt Teresya ambapo kiongozi wa wakati huo alikuwa hayati Askofu Mkuu Mario Abdalah Mgulunde, alikuwa anapitiliza kwenda kusali kanisa la Makokola njia iendayo urambo, nilikuwa na kawada mara fulani kusali huko tukawa tunakutana kwa vile tulifahamiana.

Ujio wa Pope hakuwa na jinsi kwa vile Gama kiserikali ndiye aliyekuwa mkaribishaji wa wageni wote kiserikali na kikanisa, nilimwona siku hiyo akijitahidi kusimama muda mrefu pale makao makuu ya Askofu Mkuu Tabora ilipokuwa St Mary's shule aliyofundisha Nyerere enzi hizo, siku za kawaida hakuwa na kawaida ya kusogelea makazi ya maaskofu kutokana na kilichojilia alichomfanyia mwenzao Hayati Komba. Niliwahi kusafiri na Hayati Askofu Mkuu Mgulunde once safari ndefu kidogo aliyekuwa Askofu Mkuu wakati huo pale Tabora tulijadili sana jambo hilo na kuona namna maaskofu walivyokuwa na mtazamo juu ya Gama.

Suala la Gama asitupiwe Nchimbi pekee lawama ni mchanganyiko wa Mengi

  • Nchimbi
  • Askofu Mkuu Yakobo Komba
  • Rais Kikwete ambaye alipishana naye nafasi ya kugombea urais
Hayo kwa vyo vyote yaliweza kumletea fikra nyingi Gama na pengine ndiyo yaliyokatisha haraka maisha yake ingawa alionekana kabla kama mtu mwenye siha nzuri.

CC;
Pasco
Nayakumbuka yote kwani mwaka huo ulikuwa ni 1992 wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya CCM yaliyofanyika kitaifa Songea.Nilikuwa Songea wakati wote wa maandalizi na maadhimisho.
 
Nakubaliana na wewe kwamba Nchimbi ni mwanasiasa ambaye ametumia njia za mkato na kuumiza wengi kuanzia UVCCM,CCM na Serikalini. Ni mwanasiasa muhuni na hasiye na aibu wala huruma yeyote.

Naamini mpaka leo watu kama Frank Uhahula watakua wanauguza maumivu kwa umafia aliyo wafanyia Nchimbi na rafiki yake balozi Kamala. Ktk uchaguzi mkuu wa 2005,Kamala aligombea ubunge ktk jimbo la Nkenge mkoani Kagera. Alipotambua mpizani wake Wakili Ndyanabo kupitia NCCR Mageuzi anakubalika zaidi yake,akamhonga meneja wa kampeni wa mpinzani wake akaharibu makusudi orodha ya wadhamini. Kamala akapita bila kupingwa!! Uchaguzi wa 2010 wananchi wa Nkenge wakampiga chini! Ni watu waliokuwa wamezoea siasa za kihuni na umafia!
Mkuu hao vijana (nawaita vijana kwa vile ni wadogo kwangu) huwa wanasahau kule walikotoka.
Mwaka 2005 nimekutana nao wote pale joint ya Mbunge fulani Morogoro, hata ukiwasalimia ilikuwa nyodo kwa kwenda mbele, ingawaje katika shula za msingi tulizo soma walikuwa hata kindergatten hawajaanza.
Nimekutana tena na Kamala kwenye ndege pale Kigali miezi kadhaa iliyopita(baada ya kumwagwa uwaziri), sasa ndo wanaanza kuguktuka kusalimia kila mtu.


Cheo ni dhamana , ukikipata kwa dhuluma utawadharau wengine kwa kujiona mjanja. Lakini matatizo yakikurudisha kwa waswahili wale wale ulioowaacha , ni kuomba radhi tu, hasa kwa wale mtu uliowaumiza.
Kutambika makaburini, hilo litakuwa kwa maagizo ya waganga, na huo ni ushirikina.

Katika siasa matawi ya juu is only temporary!
 
- Lowassa sio ishu ndani ya CCM huenda ni ishu kwenu mnaomuogopa kwetu CCM ni mwanachama kama wengine siku ya siku ikifika atahahukumiwa kama wanachama wengine wote angekuwa hakamatiki angempa ubunge mkwe wake kaka, ule ulikuwa ni mtihani tosha wa aliposimama kisiasa, kama hakusoma pale basi hakuna tena mtihani mwingine!!

Le Mutuz

Lowasa asingekuwa issue ccm baba yako malechela asingetokwa na mapovu bila sababu.

Lowasa ndio mwanaume wa shoka ccm hutaki unaacha, halafu ushauri huu kampe baba yako anayetokwa na mipovu akisikia jina la Lowasa.
 
Wacha kuongea utumbo wewe mtumzima,utamteteaje muuaji au kwa sababu ni mmoja wa mabuzi yako?sishangai kwa sababu hata watu wabakaji unawatetea,watu wan CYMERA_20140128_225635.jpgCYMERA_20140204_175600.jpgCYMERA_20140204_175519.jpgaomtukana baba yako ndio masuperfriends wako,grow up hizi tabia za kimombasa uache.
 
- Duh leo wamekugusa na wewe kaka mkubwa maana huwa ni bingwa sana wa kutukana wengine, ha! ha! ha! ndio raha ya JF watakubana mbavu mpaka utaonyesha ukweli wako siku moja!! ha! ha! ha!

Le Mutuz

Mkuu ni wapi huko nilipotukana wengine........Mzee wako namheshimu sana.....hata ukiangalia posts zangu zote huwezi kukuta nimemtukana Mh........Kaka yako (RIP) aliyefariki kwenye ajali ya Gari pale karibu na St' Peter alikuwa rafiki yangu sana.......
 
Wacha kuongea utumbo wewe mtumzima,utamteteaje muuaji au kwa sababu ni mmoja wa mabuzi yako?sishangai kwa sababu hata watu wabakaji unawatetea,watu wanView attachment 137153View attachment 137154View attachment 137155aomtukana baba yako ndio masuperfriends wako,grow up hizi tabia za kimombasa uache.

- Unatakiwa kuwa na Tabia za kimombassa kwanza so mkuu kumbe ndio zako hizo! ha! ha! ha! ha! wewe unafikiri mimi natishika na picha za kutengenza kumbe ninawatesa kiasi hiki saafi sana sasa ndio nitazidisha fimbo kaka, waulize wanaoninijua vizuri watakwambia sitishiki na picha za kutengeneza, so kaa mkao wa kula kaka maana sasa nataka kuanza upya na fimbo hapa!! ha! ha!

- Viongozi wote wamepokea hela za rushwa kaka toka kwa Mkono na Rostam, sema kama ni uongo? ha1 ha!

Le Mutuz
 
Lowasa asingekuwa issue ccm baba yako malechela asingetokwa na mapovu bila sababu.

Lowasa ndio mwanaume wa shoka ccm hutaki unaacha, halafu ushauri huu kampe baba yako anayetokwa na mipovu akisikia jina la Lowasa.

- Sasa ina maana kaka umekata tamaa kabisa na kushika Dola sasa unawalilia watu wa CCM, saafi sana nilidhani utalilia chama chako sasa unamlilia Lowassa saafi sana!!, chezea CCM wewe!!

Le Mutuz
 
candid! Asante historia nzuri. Nakumbuka mwaka .1982-84 nilikuwa Karibu na kijiji cha Paradiso ambacho walihamia hawa wamanda wa lituhi, tulikula sana "mabuluga na mafuta ya kwenye makopo" wakibadilisha kwa mihogo. Babu aliwahi niambia wengi walikufa hapo Paradiso nafikiri kutokana na kubadili mazingira. Walikuwa na tajiri mmoja akiitwa Ndundandunda alikuwa na mshine ya kusaga na landrover,mkiwa kwenye bas songea to ndongosi hawa wamanda wanaongea wao tu, mwingine mbele na mwingine nyumaaa.. vichwa sana hawa jamaa.
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa kura za maoni huyu jamaa si alichukua wajumbe waliokuwa wanajulikana kumuunga mkono Gama, akajifanya kwenda kupiga kampeni kwao, akawafungia ndani kwa kufuli hadi upigaji kura ukaisha...

Watu wanadhani wataishi milele...

Duh jamaa katili eheee
 
ndio maana Chadema wapo mpaka leo pamoja na kushindwa kila kitu toika waaanzishe chama chao ni kushindwa tu mpaka leo
- Lowassa sio ishu ndani ya CCM huenda ni ishu kwenu mnaomuogopa kwetu CCM ni mwanachama kama wengine siku ya siku ikifika atahahukumiwa kama wanachama wengine wote angekuwa hakamatiki angempa ubunge mkwe wake kaka, ule ulikuwa ni mtihani tosha wa aliposimama kisiasa, kama hakusoma pale basi hakuna tena mtihani mwingine!!

Le Mutuz
Mkuu, kuna contradiction kwenye hizi posts zako!

Kwani waliomnyima mkwe wa Lowassa Ubunge ni CCM au Chadema?
Unasema "siku ya siku ikifika atahahukumiwa" ni kina nani hao watamuhukumu? Ni wale wale wa Arumeru?
 
Back
Top Bottom